Unakumbuka nini enzi ulipokuwa msingi?

Unakumbuka nini enzi ulipokuwa msingi?

lyinga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2013
Posts
2,494
Reaction score
1,057
Mimi nakumbuka enzi hizo nipo shule ya msingi mengeni pr school marangu namkumbuka sana mwalimu wangu kiwoli msimu wa mahindi ya kukaanga ukifika unakuta jamaa kakaanga karibu nusu rambo lol ikifika kipindi cha mapumziko ukijichanganya tu kutoka nje unakuta mahindi yote yameliwa nakumbuka kipindi cha kufunga shule inabidi ukae vizuri usigombane na mtu manake lzm utasikia kuna ngumi sehemu bas wakati wa kutoka wanafunzi karibia woote siku hiyo watabadilisha njia kwenda kushuhudia ngumi ama kweli utoto raha wewe unakumbuka nini?
 
nakumbuka tulisoma kitabu hichi darasa la tatu
sikumuelewa mwalimu alimaanisha nini mpaka
sayansi kimu akaingia na kitabu hichi na
kuanza kutufundisha wakati hatuelewi chochote kipindi hicho
labda nyakati hizi za sasa hebu kione na wewe utaelewa hapa

kitabu.jpg
Mimi nakumbuka enzi hizo nipo shule ya msingi mengeni pr school marangu namkumbuka sana mwalimu wangu kiwoli msimu wa mahindi ya kukaanga ukifika unakuta jamaa kakaanga karibu nusu rambo lol ikifika kipindi cha mapumziko ukijichanganya tu kutoka nje unakuta mahindi yote yameliwa nakumbuka kipindi cha kufunga shule inabidi ukae vizuri usigombane na mtu manake lzm utasikia kuna ngumi sehemu bas wakati wa kutoka wanafunzi karibia woote siku hiyo watabadilisha njia kwenda kushuhudia ngumi ama kweli utoto raha wewe unakumbuka nini?
 
Duu ladyf umeamua kuweka na tangazo kabisa haya bana we inaelekea ulikuwa mtundu sana ndo maana ulikuwa hutaki kuelewa au wajuzi dt com siye enzi zetu tulikuwa tunafanya skm na s kilimo kwa vitendo tulikuwa na shamba darasa tunalima mahindi yanatoka kelikweli yakikomaa tunachemsha dhule nzima tunafaidi yanayobaki tunaenda uza sokoni sikilizia kuchakachua hela ya mauzo barabara yote utaona nyeupe chini vipande vya miwa hapo ndo utajua siku hiyo kuna shule imefanya mavuno kijijini raha bana asikuambie mtu
 
Nakumbuka wakati nipo darasa la sita kuna mwalimu alikuwa ametukusanya waschana wote kuanzia darasa la tano hadi la saba kwaajili ya kutufundisha masuala ya kuvunja ungo na akaja na pakti kibao za always.

Kwa kipindi hicho nilikuwa bado sijapasua masinia so always zilikuwa ngeni machoni pangu, kabla ya yote mwalimu akatuuliza swali, "mnaijua always?" tukaitikia "ndiyooooooo"
mwalimu... "anaejua anyoshe kidole atueleze"
mimi nilikuaga na kiherehere sana darasani cha kunyosha kidole, basi nikanyoosha huku nikisema "mimi mwalimu najua"
mwalimu nae bila hiyana akanipoint "haya tujibie"
mimi kwa sauti kubwa ya ujasiri kabisa huku nikivuta maneno nikajibu "mwaaalimuuuu alwayyyyyyys koookaaakkkooolaaaaa"
mwalimu akasema "nini?"
nikamwambia bila aibu ni cocacola mwalimu.

Yaani nilichekwa darasa zima hadi nikalia maana nilijiona niko sahihi kutoka na kibwagizo cha tangazo la cocacola "always cocacola"
 
hahahaaaaaaaaa mayo weeee,nahisi kiherehere kilishia hapo hapo.
 
Nakumbuka tukiwa darasa la saba alifika mwalimu(mpya) wa kike siku moja mchana akiwa anarudi toka lunch kama kawa wazee wa beki bencha waka mpigia kisi akajifanya hakusikia jamaa wakarudia mwalimu hana taimu alipo fika ofisini kawaambia walimu wakongwe tukaitwa wavulana wote tukaambiwa tutaje waliopiga kisi watu kimya tajeni watu kimya kumbe tunawaogopa bhana weee zikachukuliwa bakora walimu kumi walikuwepo ofisini @ mmoja bakora 2 weeeee ulikuwa mtafutano sikupenda tena kukaa beki bencha toka siku hiyo mimi zangu katikati hadi leo hii popote pale panapohusu masomo Lol!
 
Hahahahaha nakumbuka kachori tuu na sambusa kuna bibi flani alikua anauza anaitwa bi zainab🙂🙂🙂🙂😉😉😉
 
Nilishawahi kumpiga mtu speedo ya bega ile tip ya kuandikia ikabakia begani. Sikuonekana week nzima shule
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom