Kipi kati ya hivi unakumbuka uliwahi kufanya ulipokuwa shule ya msingi

I am Groot

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,730
10,033
Unakumbuka haya enzi za shule?
Kama umesoma shule za msingi za serikali miaka ya '80 mpaka '90 utakuwa unayajua haya…

1. Unaenda shule umechelewa unakuta mwalimu anakamata wachelewaji unaamua urudi nyumbani.

2. Unachukua kimbegu cha ubuyu unasugua sakafuni halafu unamuunguza mwenzio.

3. Mkiruhusiwa tu unakimbia unataka uwe wa kwanza kwenye njia yenu ya kurudia nyumbani.

4. MTU akikukera unamfungia shule (mnapigana baada ya kufunga shule)

5. MTU akikunyima kitu chake unamwambia "Ahaa eeh utaona saa nne" siku ukipata chako hakika atajuta kwa nini alikunyima.

6. Wadada wembamba ndo wanaongoza kwa kusuta wenzao

7. Ukiibiwa daftari jipya unalia kuliko hata uliloandika.

8. Unajaza mapeni kwenye mkebe (compass) na mengine hayaandiki.

9. Vifaa vingine kwenye mkebe hujawahi hata kuvitumia mfano bikari labda utolee mwiba😂

10. Hakuna habari nzuri kama kuambiwa Leo hamna shule mwalimu hayupo.

11. Habari mbaya zaidi ni kurudi nyumbani kutoka shule una njaa halafu unaambiwa chakula mgeni kaja tumempa

12. Mtoto wa mwalimu utamgundua tu kwanzia sweta, begi na viatu vyake.

13. Usiombee umpige mtoto wa mwalimu utatamani uache shule

14. Unatengeneza kifutio cha ndala halafu unatishia eti kinafuta hadi peni😂
15. Ukaguzi na huna ufagio.. unaomba chelewa kwa watu halafu unaongeza kijiti katikati.

16. Siku ukienda na ufagio wanakagua maji, ukienda na maji wanakagua kuni au mbolea😆
😂

17. Kuweka Kioo chini ya Sketi...!!

Dah shule zetu hizi kiboko!!
Ipi umeipitia wewe...??
 
No 16 imenitesa sana aise😂
 
Nilikuwa mchelewaji mkuu shule na mpiga kelele namba moja darasani, kwa kunikomoa wakanipa kazi time keeper na u class monitor miaka mitatu mfululizo. Yaani kuanzia std 5 mpk 7. Kila nikilalamika nibadilishwe mwalim mkuu ananiambia ndio unatimiza malipizi kwa makosa uliyofanya. Dadeki ila nilinyooka. Mpk Leo nipo vizuri Sana kwenye time management.
 
Naona kama kuanzia 1 - 16 hujaandika kitu ila 17 tu ndio nimekuona mjanja,hapo kwenye 17 nami nilikuwa nina weledi
 
Tulikua na michezo mibaya sana tukiwa LA saba...

Tulikuwa tukirudi tuisheni jioni wavulana tunakaa mlangoni... Basi mademu wakipita tunawashika K... Dah...ilikuwa noma kinoma
 
Nilikuwa mchelewaji mkuu shule na mpiga kelele namba moja darasani, kwa kunikomoa wakanipa kazi time keeper na u class monitor miaka mitatu mfululizo. Yaani kuanzia std 5 mpk 7. Kila nikilalamika nibadilishwe mwalim mkuu ananiambia ndio unatimiza malipizi kwa makosa uliyofanya. Dadeki ila nilinyooka. Mpk Leo nipo vizuri Sana kwenye time management.
Yaan time keeper alafu mchelewaji. Daah kweli walikukomoa bablai😁
 
Unakumbuka haya enzi za shule?
Kama umesoma shule za msingi za serikali miaka ya '80 mpaka '90 utakuwa unayajua haya…

1. Unaenda shule umechelewa unakuta mwalimu anakamata wachelewaji unaamua urudi nyumbani.

2. Unachukua kimbegu cha ubuyu unasugua sakafuni halafu unamuunguza mwenzio.

3. Mkiruhusiwa tu unakimbia unataka uwe wa kwanza kwenye njia yenu ya kurudia nyumbani.

4. MTU akikukera unamfungia shule (mnapigana baada ya kufunga shule)

5. MTU akikunyima kitu chake unamwambia "Ahaa eeh utaona saa nne" siku ukipata chako hakika atajuta kwa nini alikunyima.

6. Wadada wembamba ndo wanaongoza kwa kusuta wenzao

7. Ukiibiwa daftari jipya unalia kuliko hata uliloandika.

8. Unajaza mapeni kwenye mkebe (compass) na mengine hayaandiki.

9. Vifaa vingine kwenye mkebe hujawahi hata kuvitumia mfano bikari labda utolee mwiba

10. Hakuna habari nzuri kama kuambiwa Leo hamna shule mwalimu hayupo.

11. Habari mbaya zaidi ni kurudi nyumbani kutoka shule una njaa halafu unaambiwa chakula mgeni kaja tumempa

12. Mtoto wa mwalimu utamgundua tu kwanzia sweta, begi na viatu vyake.

13. Usiombee umpige mtoto wa mwalimu utatamani uache shule

14. Unatengeneza kifutio cha ndala halafu unatishia eti kinafuta hadi peni
15. Ukaguzi na huna ufagio.. unaomba chelewa kwa watu halafu unaongeza kijiti katikati.

16. Siku ukienda na ufagio wanakagua maji, ukienda na maji wanakagua kuni au mbolea

17. Kuweka Kioo chini ya Sketi...!!

Dah shule zetu hizi kiboko!!
Ipi umeipitia wewe...??
18- siku tukiambiwa kwenda tumevaa nguo za nyumbani ilikuwa full shangwe.

19- kumuandikia demu barua ya kumtongoza unamwaga mistari kama yote unaiweka kwenye daftari lake la hesabu halafu mwalimu anaikamata, inasomwa mstarini........
 
Duuh hilo la kuweka mistari yako chini ya daftar lake ni noma.
 
Kunyoosha shati la shule na kuliwekea mistari mgongoni kwa kutumia pasi ya mkaa. Pasi yenyewe hadi ukaombe mtaa wa 7.

Kuvaa nguo safi ni j3 na alhamisi, siku nyingine majanga tupu.

Kipindi cha masika ni kupiga umande na kupambana na mbung'o njia nzima.

Hakika elimu tuliihangaikia wacha tuwe majizi wa mali za watanzania.
 
Mm na mwenzangu tulitumwa na mwl tukamnunulie nyama halaf tumpelekee kwake, sasa tulikua na njaaa.

Tukaandika ka memo 'WAPE CHAKULA HAO WANAFUNZI' tulivyofka tukampa mfanyakazi wake....
Dada wa watu sbb alikua hatarajii akaanza kutupikia ile ile nyama wanaume tukakaa seblen tunaangalia TV,
yaani hata kujiongeza kuanzia lunch mpk kengere ya kutoka tunasubr menu iive.
Ile anaweka tuu menu mezani Mwl huyu hapaa....

Aloooooooooo sasa mm nikachelewa kung'amua, m nilisikia tuu kuku wakipiga kelele huko njeee, kuchek mwenzangu siomuoni, kumbe zile kelele ni farangati
pale kwenye korido, yeye kuku na Mwl......

Aloooo kilichokeaaaa na kilichonikutaaa........yaani baada ya kusawazisha nikazidi kuharibuuu, katk harakat za kujikomboa kila ninapoenda naharibu/naangushua/napasua vyombo na vifaaaa.......nikapata gap shati likadakwa na kitasa nililiacha pale pale kipande.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom