Unakumbuka breakup yako ya kwanza?

Unakumbuka breakup yako ya kwanza?

Ulimpenda baharia tatizo ila ubaya ni kwamba nawewe kuna mtu angekupenda kwa kiwango hiko hiko ungekuwa unamfanyia visa vya kishamba kama vya huyo baharia.

Mapenzi bana sijui yakoje, unaempenda hadi kufwa yeye wala hana habari nawewe same applies unapopendwa hadi haielezeki pia unazingua
Ila ukipenda unapopendwa,.. daah ni raha sana
 
Hivi huu uhakika huwa mnautoa wapi? Eti hakuna, yaani binadamu wote chini ya hili jua wameumizwa na mapenzi?
Ameropoka2 ila me kiukweli sijawahi kuumia sana sana me ndio nimewaumiza kama wawili. Ila naogopa kumcheka mamba wakati bado sijavuka mto
 
Ile msg ya Naona tuachane tu aisee nilihisi Gizaa flani hivi nikataka kuzimia..!! Sikuweza kuongea na mtu yani nililia kama mtoto ila mama akajua tatizo aisee alinitia moyo na kunipa shule kuhusu wanawake yani toka siku ilee mwanamke hawezi isumbua akili yangu hata Kama Nimpende vipii... akizingua namuacha dak sifuri kitu kingine siwezagi Kumbembeleza mwanamke kabisaa.
Unalia kisa manzi

Huu ni ushamba umeniangusha mwana kibaha

Uboyzin hatupo hivi
 
Nilipogundua anataka kuniacha nikamuwahi akajifanya bado ananipenda kumbe ananilia timing anifanyie suprise ya kuniacha, siku anataka kukamilisha mpango wake nilimtandika makofi hatosahau maishani

Yaani nikipiga upande huu narudia upande wa pili ndo nahesabu kofi moja.
You deserve a gold medal
 
Huwezi kusema umejipanga, nakuombea mdumu tu...Asije akapata mtu wa kumchocha pemben akadai talaka kinguvu...Tutakuzika na kilo zako ,🤣🤣🤣
Ahahahahahahah.Kwel Baba .halaf ile mshafanya maendeleo ya pamoja kwa kiasi kikubwa halaf aanze kudai talaka mzee lazima azikwe mtu.
Ndio maana jamaa aliamua ku apply gunia 2 za mkaa
 
Karibu rasmi sasa kwenye chama la malaya wa kiume tz.....
Hapa ndo nilithibithisha kua mapenzi ni yanauma,
Maumivu nilioyapata sijawai kuyapata tena na naomba yasijieudie, yan huumwi sehemu yoyote ya mwili lakini unaona dunia iko juu chini,
Kwa mara ya kwanza nikashindwa kula.
Chozi linatoka, lecture hazipandi.

Sikua mpenzi wa nyimbo ila nilijikuta nawafahamu kina Bruno Mars, Celine dion, ibra nation, Adele na wengine wengi.
Nilikua nikiangalia picha yake au nikiangalia call history nalia. Sema nilikua najikaza watu wasinione dhaifu.
Hakika haya mambo yasikie. Kwa ambae hayajamkuta hawezi kuelewa hii hali
 
Yale yale ya faiza ali
Yule ms*nge aliniacha jumapili ambayo jumatatu yake tulikuwa na test...sababu yake mammmae zake nikachafua CV ya kuzungusha ile paper (nilipata zero)

Nilikuwa siwezi kula
Siwezi kulia japo natamani kulia lakini machozi hayaji
Nilikuwa mchekaji mzuri lakini siku hizi sicheki kabisaaaa

Popote ulipo ama kama unasoma hapa ujue tu nakuchukia kuliko kawaida!!!na kwa taarifa yako ninae baby mpya nampenda sanaaaaaa

#povu

Halafu bado nakupenda
 
Nilimeza vidonge vya usingizi na usingizi sikupata
 
Back
Top Bottom