Unaishi vipi na mwanaume asiyepokea ushauri wa mwenza/ watu wengine?

mkushiOg

Member
Feb 17, 2024
52
122
Hellow JF Members,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza naomba maoni ya wadau. Unakuta mwenza ni mgumu sanaa kupokea ushauri hata wa kawaida tu na pale mambo yanapomuendea kombo juu ya jambo ulilomshauri anakurudia na anataka mshiriki wote kutatua.

Mfano anaweza fanya maamuzi ya kununua kitu fulani ukamwambia may b hapo siyo pazurii au hicho kitu unachotaka kununua kwa sasa hakina uhitaji mkubwa coz tuna mahitaji haya na hayaa ya msingi zaidii ni anakua mkaidi na kununua then kikiharibika anataka uchangie katika matengenezo nk.

Mfano mwingine mnaweza mkawa na ujenzi A unaendelea ghafla akaanzisha ujenzi B unamshauri kuwa hiyo pesa ya ujenzi B n heri tukamalizie kwanza ujenzi A then ndo uanzane na project B but atakaza fuvu ataenda anza ujenzi B mara paap pesa zinakataa hamna kitu ambacho kimekamilika as angemalizia ujenzi A basi hata mngepangisha then pesa ambazo zingepatikana hapo kutoka A zingeanza project B.yaan mifano ni mingi sanaaa sijui ni anakuwa na utemi ndani yake sielewi.

Naomba ushauri unadeal vipi na mtu wa tabia za mfanano huo??
 
Huyo sio kwamba hapokei ushauri kabisa kutoka kwa watu. Anapokea ushauri vizurii tu ila ushauri usio sahihi. Kitendo cha kuachana na Project A na kukimbilia kuanzisha nyingine hapo ni ushahidi kwamba kuna watu walimshauri ila huo ushauri haukuwa sahihi kwake.
 
Huenda mnashindana kuineshana usahihi au nani ni zaidi.

So anafanya kukuprove wrong kua yeye ni kichwa ila ndo ivo projects zinafeli, labda pia uwasilishaji wako wa ushauri huenda hauendani na akili ya mtu wako, mtu asiejiamini kama huyo kama unataka afate ushauri wako basi ujinyenyekeze na ujidogoshe.

Ukimshauri as if wewe ni architecture anaona umemdharau
 
Baadhi yetu sisi binadamu tunayo matatizo ya kukosa utulivu hasa tupatapo pesa /hela za mboga. Badala ya kutuliza akili tunakuwa na papara na kiherehere kwa kujiaminisha kwamba pesa ni Kila kitu, zikikata tu....ngebe zote kwishaaa

Huyo usimkatie tamaa endelea kutimiza wajibu wako kwa kumpa ushauri pengine ipo siku atabadilika
 
Kuna baadhi ya watu hawashauriki hata umpige panga, ushauri wako unapoteza bure.
Mmojawapo ni mimi nabeba risk ya kufanya maamuzi binafsi sihitaji ushauri na yakiharibika nitajua mwenyewe ila siwezi enda sumbua mtu kwa nilichoharibu, nitachora nianze moja.
 
Huyo sio kwamba hapokei ushauri kabisa kutoka kwa watu. Anapokea ushauri vizurii tu ila ushauri usio sahihi. Kitendo cha kuachana na Project A na kukimbilia kuanzisha nyingine hapo ni ushahidi kwamba kuna watu walimshauri ila huo ushauri haukuwa sahihi kwake.
Okaay umenifumbua macho,asante.!sasa naomba ushauri namna ya kudeal na hii tabia yake.
 
Asante boss,nmekupataa na umenipa njia ntaitumia.!ubarikiwe

Back
Top Bottom