Unadhani kwanini Watanzania wengi wanamkubali Rais Samia?

Unadhani kwanini Watanzania wengi wanamkubali Rais Samia?

Binafsi sijawai kushuhudia mtu mtaani anasema anamkubali Samia. SIDANGANYI
mtaani?
hata tangu umejiunga JF miaka yote hiyo hukuwahi kumuona wala kukutana na JF members physically, kweli si kweli?🐒

Dr.Samia Suluhu Hassan, anazingumzwa sana kule zinakopatikana huduma msingi za kijamii kama vile afya,elimu, maji, kilimo, biashara n.k wanao nufaika na huduma za kwenye maeneo hayo huwezi mwambia kitu ingine 🐒

sasa maeneo uliyopo wew nadhani huenda yana walakini kidogo....
 
Rais Samia anapendwa na kukubalika na mamillioni ya watanzania kwa sababu amekidhi matarajio ya watanzania na kukata kiu waliyokuwa nayo juu ya aina ya kiongozi waliyekuwa wanamuhitaji.

Kwa ufupi Mama yetu mpendwa na kipenzi cha watanzania ni jibu na jawabu kwa mahitaji ya watanzania.
Hivi Mauzinda anaendeleaje?
 
Wewe ulitakiwa kumsadia Mama yetu kwenye facts, sio kujitoa ufahamu ili kutafuta wasiompenda. Acha ujuha.
Relax bas gentleman,

mihemko inakuexpose vibaya mkuu..

Jambo la muhimu na la maana sana, lililoko wazi kabisa mchana kweupe ni kwamba mapendo ya waTanzania kwa huyu mama hayapimiki na wala hayana kifani.

huo ndio ukweli na haina haja mtu mwingine kupata mihemko na kuumia moyo kwa hilo, japo ukweli mchungu na unauma 🐒
 
hapana,,nmefurahi nmekula ugal nkashiba ndii
kwa amani na Raha kama zote,

Amani na Utulivu unaenjoy ni jitihada za makusudi za Dr Samia Suluhu Hassan....
Anapendwa kwasabb anawapenda waTanzania pia 🐒
 
Acha unafki wewe chawa huyo mama hapendwi hata januari makamba alithibitisha kwamba hatumpendi wewe kidamoa mbangaizaji unayejifanya mh. Mbunge wa jf eti watanzania wengi wanampenda bi chura. Labda anapendwa tanzania zanzibar
 
Ni kwasababu ya makusudi, haja na nia yake thabiti, ya wazi na njema ya kutaka kuibadili tanzania kiuchumi, kijamii na kusiasa?

Au ni kwasababu ya umadhubuti wa sera, mipango, mikakati, jitihada, bidii na umahiri wake katika kutekeleza kwa weledi sana na kwa ufasisi mkubwa mno miradi mtambuka ya maendeleo inayogusa mojakwamoja maisha ya watanzania kama vile maji, afya, elimu, kilimo, viwanda, uvuvi, miundombinu, usafirishaji N.K?

Au ni kwasababu ya amani liliyopo, ulinzi, usalama, uhuru, haki, utulivu, usawa, uwazi na uwajibikaji wake katika kuongoza nchi kwa misingi ya utawala wa sheria na kwa kuzingatia katiba ya nchi?

Au ni kwasababu ya matumani makubwa waliyo nayo Watanzania kwake, kwamba ndie pekee kiongozi wa kisiasa nchini, anae weza kutimiza ndoto na matarajio yao, ya maisha bora?

Kwa maoni yako, unadhani ni kwanini Samia Suluhu Hassan, anapendwa na kuaminika kiasi hiki, kitaifa na kimataifa?
Nani anamkubali kama sio matahila wezako.angekuwa anakubalika si tiari tungekuwa na katiba mpya.
 
Back
Top Bottom