Una jambo gani la matumaini la kuwaambia watu waliokata tamaa kabisa?

Naanza mimi hapa.

Kwanza hakuna kuchelewa kwenye maisha. As long as bado uko hai hakuna kuchelewa ama kuwahi kwenye maisha. Jambo lolote linaweza kutokea wakati wowote.

Mimi nilimaliza form four nikiwa na miaka 22, nikamaliza form six nikiwa na miaka 25. Leo hii vijana wanamaliza chuo kikuu na miaka 21 ama 22.

Baada ya kumaliza chuo form six nikakosa mkopo, ninarudi nyumbani nikawa nachimba dhahabu nikapata pesa ya kuanzia maisha chuo kikuu, mwaka uliofuata nikajiunga na chuo kikuu, nikasoma kwa tabu sana, kwa kuunga unga sana, kwa mbinde sana, nikamaliza chuo kikuu nina miaka 29. Ulikua ukiniona kama vile nina miaka 50, nimechoka, nimekongoroka, nimezeeka.

Nakumbuka kuna dada mmoja wa mtaani nilimtongoza akasema hawezi kutembea na nyumbu (kwamba naonekana kama nyumbu😂 ) vile nilivyopauka. Hakuniambia mimi wazi, alimwambia mwanangu mmoja jamaa akaja akaniambia achana na yule manzi anakudharau sana, anasema wewe ni nyumbu.

Baada ya kumaliza chuo kikuu nikakaa mtaani mwaka mzima, nilifanya kazi za ajabu ajabu ajabu sana hazielezeki. Mwaka mmoja baadae zali likanidondokea, nikapata kazi kwa kampuni moja ya wazungu, mshahara wa maana, namaanisha wa maana, gari ya kutembelea ya ofisi, pesa za vocha kwa mwezi kama mshahara wa mwalimu wa bongo😂, nyumba ya kuishi, safari nje na ndani ya nchi na marupurupu ya kufa mtu.

Ndani ya mwaka mmoja nikasahau machungu yote ya maisha niliyopitia. Nikabadili kabisa maisha yangu na maisha ya nyumbani kwetu, bahati mbaya sana kwangu mama yangu alifariki kabla sijamlipa fadhila zangu kwake.

Wale wazungu nilifanya nao kazi miaka 3 kabla ya Magufuli hajaingia, Magufuli alipokua Rais wakafunga ofisi na kuondoka ila kazi yao ilinipa maisha kama vile nimefanya kazi miaka 20.

Baada ya Magufuli kuingia na kule mkataba kuisha nikakaa tena kama mwaka kisha nikapata kazi mahala pengine.

Kufupisha stori, mtu hutakiwi kukata tamaa, haya maisha kifo tu ndio kikukatishe tamaa na kuzima ndoto zako ila kwa kua bado unaishi, usikate tamaa, jambo lolote linaweza kutokea wakati wowote na sio lazima sana uwe na godfather.

Una chochote cha kuwaambia watu waliokata tamaa? karibu.
Nilitamani kusikia hatma ya yule manzi aliekuita nyumbu alliishia wapi??
 
Ndio ukweli,kwenye maisha tunapitia magumu mengi.baada ya form 4,nikaenda college,Wazazi walilipa nusu ada ya muhura wa kwanza,mwaka wa kwanza,ada yote mpaka namaliza,nili hustle mwenyewe,ukiniuliza nilimaliza vipi chuo,kwa kweli ni miujiza TU,nimemaliza chuo,nilipokuwa nakaa,anko wangu ananishuku nimemwibia,vituko kibao,hiyo ni 2006!hata simu Sina!
Ikatoka kazi gazetini,wenzangu wakaiona,nikatumiwa,nikapata kazi,maisha yakabadirika,
Cha msingi usikate tamaa,hatq kama mbele Ni Giza tupu,Mungu Huwa na namna anavyotwist mambo ili deal ikuangukie wewe.
 
Kila mtu akate alicho nacho. Kama ana tamaa aikate hiyo, kama ana mafanikio naye ayakate hayo. Mtu kakata tamaa unataka kumfanyaje? Akukate wewe?
Ahsante huu mchango wako unaendana na jina lako! Daaah nimejikuta nacheka tu
 
Wasihofu, mwisho wote tutakufa tu. Yote tunayofanya hapa duniani ni ubatili mtupu. Wako wapi walioishi mwaka 1507?
 
Imeandikwa: “

Mtumaini Bwana Mungu kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe, katika njia zako zote umkiri Yeye , Yeye atanyoosha mapito yako”

Pia Imeandikwa:

“Tumaini la Bwana halitahayarishi”

Tafakali kwa kina .
 
Naanza mimi hapa.

Kwanza hakuna kuchelewa kwenye maisha. As long as bado uko hai hakuna kuchelewa ama kuwahi kwenye maisha. Jambo lolote linaweza kutokea wakati wowote.

Mimi nilimaliza form four nikiwa na miaka 22, nikamaliza form six nikiwa na miaka 25. Leo hii vijana wanamaliza chuo kikuu na miaka 21 ama 22.

Baada ya kumaliza chuo form six nikakosa mkopo, ninarudi nyumbani nikawa nachimba dhahabu nikapata pesa ya kuanzia maisha chuo kikuu, mwaka uliofuata nikajiunga na chuo kikuu, nikasoma kwa tabu sana, kwa kuunga unga sana, kwa mbinde sana, nikamaliza chuo kikuu nina miaka 29. Ulikua ukiniona kama vile nina miaka 50, nimechoka, nimekongoroka, nimezeeka.

Nakumbuka kuna dada mmoja wa mtaani nilimtongoza akasema hawezi kutembea na nyumbu (kwamba naonekana kama nyumbu ) vile nilivyopauka. Hakuniambia mimi wazi, alimwambia mwanangu mmoja jamaa akaja akaniambia achana na yule manzi anakudharau sana, anasema wewe ni nyumbu.

Baada ya kumaliza chuo kikuu nikakaa mtaani mwaka mzima, nilifanya kazi za ajabu ajabu ajabu sana hazielezeki. Mwaka mmoja baadae zali likanidondokea, nikapata kazi kwa kampuni moja ya wazungu, mshahara wa maana, namaanisha wa maana, gari ya kutembelea ya ofisi, pesa za vocha kwa mwezi kama mshahara wa mwalimu wa bongo, nyumba ya kuishi, safari nje na ndani ya nchi na marupurupu ya kufa mtu.

Ndani ya mwaka mmoja nikasahau machungu yote ya maisha niliyopitia. Nikabadili kabisa maisha yangu na maisha ya nyumbani kwetu, bahati mbaya sana kwangu mama yangu alifariki kabla sijamlipa fadhila zangu kwake.

Wale wazungu nilifanya nao kazi miaka 3 kabla ya Magufuli hajaingia, Magufuli alipokua Rais wakafunga ofisi na kuondoka ila kazi yao ilinipa maisha kama vile nimefanya kazi miaka 20.

Baada ya Magufuli kuingia na kule mkataba kuisha nikakaa tena kama mwaka kisha nikapata kazi mahala pengine.

Kufupisha stori, mtu hutakiwi kukata tamaa, haya maisha kifo tu ndio kikukatishe tamaa na kuzima ndoto zako ila kwa kua bado unaishi, usikate tamaa, jambo lolote linaweza kutokea wakati wowote na sio lazima sana uwe na godfather.

Una chochote cha kuwaambia watu waliokata tamaa? karibu.
Nyakati ngumu hazidumu, usife moyo yatapita.
 
Usijal maisha ni mapambano hakuna kukata tamaaa
Mtegemee mungu , pale unapodondoka inuka endelea na safari,changamoto zinatokea kwny maisha ili kutufunza na kutuimarisha ,, wakati wa Mungu ni sahihi
 
09f0811353cc0255c81cb7b7619278cc.jpg
 
Maisha ukiyafanya siriaz sana yatakupeleka makosaa..
Mimi kila nnavyoona sitoboi ndio nikawa naona milango iko wazi.sikutumia nguvu nyingi sana life likaja vizuri tuu.

All in all naamini maisha ni bahati tu na kila mtu anaye ya kwake!haitakupita itakuja kama vile riziki mafungu saba.

Hapo ikija ndio kuna msemo.

Uendelee au usiendelee!
Hilo ni jukumu lako wala usije kumlaumu mtu baadae wala usijilaumu nafsi yako
Umenena vyema
 
Kwenye haya maisha, ili utie huruma make sure wapo watu wa kukuonea hiyo huruma, tofauti na hapo option ni moja tu "Kukaza"

Usimlaumu mtu yeyote kwa hali yoyote ngumu utakayokuwa unapitia. Never feel too comfortable.
 
Kuna wakati tunakata tamaa haswa tunapojaribu kujipambania nakufeli mara nyingi na kila ukitafuta wakukupa mkono hakuna upo mwenyewe katika vita usiojua utaishinda vipi na lini
Broh maisha yako ni yako. Hata hao unaotamani wakushike mkono, nao wanahitaji kushikwa mkono hivyo hawawezi kukuangalia wewe muda wote.

Ukishaona huna mtu wa kukupa back up, inabidi ikusaidie kujua future yako inadepend kwako 100%. Wengi wamechelewa kufika kwa kusubiria support toka kwa wengine. Make sure hukati tamaa broh
 
Back
Top Bottom