God Forbid
Member
- Jan 6, 2024
- 14
- 81
Daah nimeandika nikafuta, nikaandika nimefuata., Tokea Wiki nilitaka kuandika hili, nikawa najaribu kusubiri huenda ningepata majibu ila kwa sasa nimeiona niyatoe ya moyoni!
Kwanza nikiri nimekuwa mtumiaji wa hili jukwaa Kwa muda mrefu, zaidi ya miaka 15!
Nimekuwa nikiona nyuzi tofauti za watu kuomba ushauri, wengine husaidia na wengine huishia kudhihaki, so kwenye jamii ndio hivyo!!
Ishu yangu kwa kweli nimekuwa nikipitia kipindi kigumu, hasa kwenye maisha tu ya kawaida ya kila siku!!
Nina familia changa inanitegemea, mke alimaliza chuo hana kazi, ni miaka sasa! Nina kazi ila sina furaha na kazi!
Nilijaribu kuchukua mkopo benki nikampa mke afungue biashara, Ile biashara iliteketea yote katikati ya mwaka Jana, hakuna kilichookolewa!
Na kuanzia hapo ikabidi tuanze upya, nikaingia kwenye madeni ambayo kwa sasa kuyalipa imekuwa tabu, wadeni wananiandama kila kukicha sina cha kuwalipa!
Mshahara umeshakatwa hadi mwisho, sikopesheki popote na hata nikikopa cha kulipa Sina!!
Ndani ya familia kumekuwa na migogoro kila siku isoyoeleweka, watoto hata ada imekuwa kipengele!
Nikiwaangalia watoto na mama yao nawaonea sana huruma, kwa namna nashindwa kuwapa mahitaji yao kwa wakati!!
Hizi sikukuu za mwisho wa mwaka, wife aliniambia marafiki zake wanamcheka kwanini amekuwa so rough ina maana mume ameshindwa hata kukupa 10k ya kusuka?
Daah, yaani hivi juzi yupo ndugu yangu alipata ajali amelezwa, umepitishwa mchango wa familia nimeshindwa kuchangia hata mia, nimeumia sana!!!
Haya maisha yamenikaba kweli kweli. Sijui nachomokaje!
Inakuja roho ya kutaka niache kazi nitokomee, ninakokujua!
Mara nyingine napata mawazo ya kujiangamiza kabisa,(ila nikimtazama mwanangu mdogo anaponitazama pia kwa huruma, ni kama anajua nina masaibu) basi naishia kutoka machozi na kusema yataisha!!
Hivi sasa nina zaidi ya miezi sita nimempiga chenga mwenye nyumba sijamlipa kodi yake!
Yaani nikitoboa huu mwezi, Mungu saidia!
Nipo nimepigwa ganzi tu!
Kuna baadhi ya wanaonidai, wamenipa vitisho kuwa watanifanyia kitu kibaya, kwamba Mimi tapeli mara watanipeleka mahakamani, wengine Kwamba wataenda Kwa waganga kunifanyia unyama, kwamba napewa masala kadhaa yaani, sijielewi Kwa kweli!
Likitokea suala la kijamii mtaani, kazini, n.k hata Kama mchango ni buku imekuwa kipengele Kwa Sasa!
Simu smartphone nimeuza, hata hapa nimeumia kifaa cha rafiki yangu mmoja ambaye ndio kidogo ananipush, ila naona ameshaanza kunichoka!
Bando lenyewe nililotumia nimelipata Kwa kuvuna point!
Haya ninayopitia omba yasikukute!!!