Mr IQ
JF-Expert Member
- Jun 23, 2015
- 806
- 800
Nilitamani kusikia hatma ya yule manzi aliekuita nyumbu alliishia wapi??Naanza mimi hapa.
Kwanza hakuna kuchelewa kwenye maisha. As long as bado uko hai hakuna kuchelewa ama kuwahi kwenye maisha. Jambo lolote linaweza kutokea wakati wowote.
Mimi nilimaliza form four nikiwa na miaka 22, nikamaliza form six nikiwa na miaka 25. Leo hii vijana wanamaliza chuo kikuu na miaka 21 ama 22.
Baada ya kumaliza chuo form six nikakosa mkopo, ninarudi nyumbani nikawa nachimba dhahabu nikapata pesa ya kuanzia maisha chuo kikuu, mwaka uliofuata nikajiunga na chuo kikuu, nikasoma kwa tabu sana, kwa kuunga unga sana, kwa mbinde sana, nikamaliza chuo kikuu nina miaka 29. Ulikua ukiniona kama vile nina miaka 50, nimechoka, nimekongoroka, nimezeeka.
Nakumbuka kuna dada mmoja wa mtaani nilimtongoza akasema hawezi kutembea na nyumbu (kwamba naonekana kama nyumbu😂 ) vile nilivyopauka. Hakuniambia mimi wazi, alimwambia mwanangu mmoja jamaa akaja akaniambia achana na yule manzi anakudharau sana, anasema wewe ni nyumbu.
Baada ya kumaliza chuo kikuu nikakaa mtaani mwaka mzima, nilifanya kazi za ajabu ajabu ajabu sana hazielezeki. Mwaka mmoja baadae zali likanidondokea, nikapata kazi kwa kampuni moja ya wazungu, mshahara wa maana, namaanisha wa maana, gari ya kutembelea ya ofisi, pesa za vocha kwa mwezi kama mshahara wa mwalimu wa bongo😂, nyumba ya kuishi, safari nje na ndani ya nchi na marupurupu ya kufa mtu.
Ndani ya mwaka mmoja nikasahau machungu yote ya maisha niliyopitia. Nikabadili kabisa maisha yangu na maisha ya nyumbani kwetu, bahati mbaya sana kwangu mama yangu alifariki kabla sijamlipa fadhila zangu kwake.
Wale wazungu nilifanya nao kazi miaka 3 kabla ya Magufuli hajaingia, Magufuli alipokua Rais wakafunga ofisi na kuondoka ila kazi yao ilinipa maisha kama vile nimefanya kazi miaka 20.
Baada ya Magufuli kuingia na kule mkataba kuisha nikakaa tena kama mwaka kisha nikapata kazi mahala pengine.
Kufupisha stori, mtu hutakiwi kukata tamaa, haya maisha kifo tu ndio kikukatishe tamaa na kuzima ndoto zako ila kwa kua bado unaishi, usikate tamaa, jambo lolote linaweza kutokea wakati wowote na sio lazima sana uwe na godfather.
Una chochote cha kuwaambia watu waliokata tamaa? karibu.