Kuna jambo gani la maana umelibeba toka hapa Jamii Forums kwa 2023?

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,224
22,305
Pamoja na JF kuwa platform ya kutuondolea stress ila pia imekuwa na mambo mengi ya kutujenga kwenye maisha yetu.Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya 2023 kuisha, Binafsi nimejibebea mambo yafuatayo kwa mwaka huu 2023 toka hapa JF;

1. JF ndo sehemu pekee kwa sasa ninapoweza kupata ushauri mzuri kwa jambo lolote ninalohitaji kushauriwa. Kutokana na watu kuficha utambulishonwao hivyo hufunguka ushauri wote walio nao. Mbarikiwe sana.

2. Ujue kabisa jambo lolote utakaliandika JF linawafikia wafanya maamuzi wengi wa nchi hii akiwemo Rais mwenyewe. Kabla hujaandika tafakari sana.

3. Watanzania wanazidi kuamka. Kupitia JF kuna kuna ushahidi wa kutosha kuwa watanzania wa leo ni wazalendo kuliko inavyodhaniwa. Wanaipenda nchi yao na hawataki ujinga kabisa. Kuna baadhi ya nyuzi humu zimebebwa na serikali na kufanyiwa kazi au pengine kuna raia humu walikuwa na mawazo sawa na think tank ya serikali. Binafsi niliwahi kushauri kuhusu mikopo kwa vijana na haikuchukua muda mrefu nikaona tamko linaloendana na ushauri niliotoa.

4. Hili sio jambo jema kwa 2023 ila ni jambo zito. Kuna mwamko mkubwa wa vijana kuhamasishana kukataa ndoa hapa JF. Wanawake wamekuwa wahanga wa hili hasa single mothers. Tukijaliwa kuingia mwakani tuhamasishane kuoa. Nchi bila watu haiwezi endelea. Pia CCM inahitaji wapiga kura wengi zaidi. Hivyo tuoe kuongeza wapiga kura wa CCM.

5. WanaJF pia hawataki kudanganywa kuhusu mambo ya dini. Nyuzi nyingi watu wanajadili na kuchimba ukweli kuhusu imani zetu.

HAPPY CHRISTMAS AND MERRY NEW YEAR
 
Yapo mengi, ila kubwa ni taarifa ambazo siwezi kupata sehemu nyingine kwa haraka.
 
Back
Top Bottom