Una Eneo Pembeni ya Barabara?, Ungependa Kuwa Millionaire au Bilionea?. Usiuze Eneo Lako!. Total Kutengeneza Ma Milionea na Ma Bilionea 100 wa DODO!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,601
Wanabodi,
Hii ni story ya kweli kabisa, true story ya jinsi mtu wa kawaida sana, mwenye eneo tuu pembezoni mwa barabara linalofaa kujenga kituo cha mafuta, anavyoweza kugeuka millionaire au bilionea kupitia fursa ya DODO inayotolewa na kampuni ya mafuta ya Total, ambayo imepanga kutengeneza mamilionea na mabilionea 100 wa Kitanzania kupitia mpango huo wa DODO.

Umasikini m-baya kabisa, ni umasikini wa fikra, umasikini wa roho, kuwa na roho ya kimasikini!.

Kuna Watanzania wenzetu wengi tuu, wanamiliki maeneo mazuri ya biashara pembezoni mwa barabara. Wengi wa wananchi hawa ni masikini wa kutupa na wanaishi katika Lindi la umasikini uliotopea kutokana na kukosa maarifa au kukosa fursa.

Hivyo wengi wa wananchi masikini hawa, bila kujua maeneo yao ni mtaji mkubwa wa utajiri mkubwa, wao wanayatumia kwa kilimo. Hivyo ukisafiri kwa njia ya barabara, huko njiani unakutana na maeneo mengi yenye potential ya utajiri, lakini yanatumika tuu kama mashamba na mengine yako idle kabisa!.

Wajanja walioshtukia fursa, huyanunua maeneo hayo kwa fedha ndogo sana kutoka kwa wamiliki wenyeji bila kuwaambia wenyeji wanataka kufanya nini!.

Wengi wa wenyeji, kutokana na kutokujua fursa za maeneo yao, na umasikini wao uliotopea, huyauza maeneo yao kwa fedha kidogo.

Wanunuzi hao huyatumia maeneo hayo kuweka vitegauchumi mbalimbali mbalimbali kama fremu za maduka, migahawa, guest houses na mahoteli, na vituo vya mafuta.

Wengi wa wenye biashara nyingi za pembezoni mwa barabara sio wenyeji wa maeneo hayo, bali ni wananunuzi.

Mchagga mmoja kwa jina la Eng. Frank Malle na mkewe, mwaka 2010, walinunua eneo fulani sehemu inayoitwa Mchigeni, pembezoni mwa barabara ya Goba, kwa lengo la kujenga makazi na na fremu za biashara kuwapangisha watu.

Huku wakiendelea kukusanya nguvu, ilipofika mwaka 2013, 2014 na 2015 kukaanza kujitokeza watu kutaka kununua eneo lao. Frank Malle na mkewe, wengekuwa watu wa njaa njaa na wasio maarifa, wangeuza na kupata pesa, lakini wao hawakuuza!.

Badala yake, walifanya upelelezi kwanini hao watu wanataka kulinunua eneo lao, wakati kuna maeneo kibao yanauzwa, si wakanunue huko!.

Ndipo wakabaini, wanaotaka kununua eneo lao, wanataka kujenga kutuo cha mafuta, ndipo wakafunguka macho na kujiuliza kama hao wanaotaka kununua eneo lao wajenge petrol station, kwanini na wao wajifanye hiyo biashara ya kituo cha mafuta.

Msikilize Eng. Frank Malle na mkewe.



Hivyo kuna Watanzania wengi wana maeneo fursa pembezoni mwa barabara ambapo huushia kuyauza, washaurini, wasiyauze maeneo yao kama alivyofanya Eng. Frank Malle na mkewe, na badala yake wachangamkie fursa ya Total Tanzania kutengenezea mamilionea na mabilionea 100 wa Kitanzania kupitia mpango wa DODO!.

Paskali
Rejea
Watanzania Tuchangamkie Fursa za Total. Kujenga Vituo 100 vya Mafuta vya Total Vitakavyomilikiwa na Watanzania kwa Mfumo wa DODO.

Total Tanzania promises it is in Tanzania to stay as it launches Total Mchinigani Service Station in Goba Dar Es Salaam

Kampuni ya Mafuta ya Total Tanzania yampongeza Rais Magufuli na kuipongeza Tanzania, kujenga mazingira bora ya biashara ya Mafuta, Uwekezaji

Total yatoa fursa vituo vya coco na codo kuzigeuza dodo! Kuwa umiliki kituo cha mafuta cha total
 
Walete Mkuranga Kiparang'anda barabara ya kwenda kusini watoe hayo ma milioni .
Am serious Ndugu Pasco
 
Ukiondoa huo umiliki wa eneo, vigezo gani vingine vinatakiwa ili niwe milionea wa hao jamaa zako TOTAL?
 
Hujafafanua mkuu pasco
Je wanajenga kituo kwa gharama zao wenyewe na kuleta mafuta?
Au inahitaji uwe na pesa za kufanya hayo nje ya kiwanja?
 
Kumbe mpaka eneo liwe strategic? Halafu kumbe ni bahati nasibu?
 
Back
Top Bottom