Conspiracy theorist
JF-Expert Member
- Oct 24, 2017
- 395
- 310
Jiji la Dar es salaam limeshika nafasi ya 181 katika majiji 186 duniani kwenye rank za majiji yenye watu wenye furaha.
Dar es Salaam imepita majiji ya Juba (Sudan Kusini), Port -au Prince (Haiti),Gaza (Palestine) Sanaa (Yemen) na Kabul (Afghanistan).
Furaha ni kitu kikubwa sana kwenye maisha ya mtu yeyote, juhudi nyingi za mtu/watu ni ili aweze kupata furaha. Hata ukifanikiwa kiasi gani kama hauna furaha ni kazi bure.
Ni wakati sasa wana Dar es Salaam na Watanzania kujiuliza kwanini tumekuwa watu wenye huzuni na machungu hadi tunashuka mkia duniani na kuanza kuweka mikakati jinsi ya kutoka kwenye hali hii mbaya.