UN Happiness Report 2020: Dar es Salaam yashika mkia kwenye orodha ya majiji yenye watu wenye furaha duniani

Conspiracy theorist

JF-Expert Member
Oct 24, 2017
395
310
Jiji la Dar es salaam limeshika nafasi ya 181 katika majiji 186 duniani kwenye rank za majiji yenye watu wenye furaha.

Dar es Salaam imepita majiji ya Juba (Sudan Kusini), Port -au Prince (Haiti),Gaza (Palestine) Sanaa (Yemen) na Kabul (Afghanistan).

Furaha ni kitu kikubwa sana kwenye maisha ya mtu yeyote, juhudi nyingi za mtu/watu ni ili aweze kupata furaha. Hata ukifanikiwa kiasi gani kama hauna furaha ni kazi bure.

Ni wakati sasa wana Dar es Salaam na Watanzania kujiuliza kwanini tumekuwa watu wenye huzuni na machungu hadi tunashuka mkia duniani na kuanza kuweka mikakati jinsi ya kutoka kwenye hali hii mbaya.

Screenshot_20200323-063843.png
 
Ripoti ya Umoja wa Mataifa (UN) ya mwaka 2020 kuhusu furaha imewaorodhesha Wananchi wa Ukanda wa Afrika Mashariki kama baadhi ya watu wasiokuwa na furaha duniani.

Kenya iliorodheshwa nambari 121 kati ya 156 huku ikipata pointi 4.583 kwenye mizani ya pointi 10

Hata hivyo, ripoti hiyo iliyotolewa Ijumaa Machi 21, ilionyesha Kenya ndyo yenye watu walio na furaha zaidi ndani ya Afrika Mashariki.

Uganda walikuwa nambari 126, Burundi (140), Tanzania 148, Rwanda 150 na Sudan Kusini 152.

Ndani ya Afrika, Libya ndio nchi ambayo ina watu wenye furaha sana kwani ilikuwa nambari 80.

Wakenya wameorodheshwa nambari 121 kati ya mataifa 156 katika mizani ya furaha. Picha: John Ndichu

Ivory Coast nayo ilikuwa nambari 85, Benin 86, Congo 88, Ghana 91, Morocco 97 na Cameroon 98.

Afrika Kusini nayo ilishika nambari 109 ikiwa na pointi 4.814.

Kulingana na ripoti hiyo, Ufini ndiyo nchi yenye watu walio na furaha zaidi ulimwenguni ikifuatiwa na Denmark.

Wakenya hata hivyo wameorodheshwa kama watu wenye furaha sana Afrika Mashariki.

Marekani nayo iliorodheshwa nambari 18, Uingereza 13 Ujerumani 17, Italia nayo ikashikilia namabari 30.

Ripoti hiyo ilisema nchi zenye furaha zaidi zina hali nzuri ya mapato, uhuru wa wananchi, ukarimu, roho za kusaidiana kati ya mambo mengine.

Kwa taarifa zaidi soma;
 

Attachments

  • WHR20.pdf
    4.1 MB · Views: 1
miss zomboko, Siyo Ulimwenguni, edit uweke Duniani. Wanadamu tunaishi duniani ulimwengu ni kitu kingine kipana.
Tafadhali fanya marekebisho kwa faida ya wasomaji.
 
Utafiti km huu CCM hasa wasiojielewa huanza dhihaka utani na dharau. Ukweli ni kwamba awamu hii vitisho vimetawala kila kona. Watumishi kunyanyashwa na kutukanwa mbele za watu ni jambo la kawaida. Iweje wawe na furaha? Mtaani hawa wanaoitwa wanyonge mda wote wanalalamika maisha kuwa magumu.

Kwenye siasa ndio kabsa si nje wala ndani ya CCM hakuna amani. Ukihoji jambo tu unafukuzwa km sio kupewa kesi ya uhujumu uchumi au kutakatisha fedha. Hapo furaha itatoka wapi? Umeona wapi waziri anatukanwa hadharani km sio TZ tu? Nazani tunastahili kabsa kuwa kwenye hiyo nafasi bila ubishi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na amani na kujidai wasuluhishi vinara sisi Tz tunakaribiana na sudani kusini na rwanda. Na watatuacha maana hawana vita tena wanajipanga saivi
 
Wazungu washenzi wale!!!

Nchi kama Libya,ambayo watu wake hawana tumaini na Kesho Yao ndio inakuwa na watu wenye Furaha kuzizidi nchi za Africa mashariki siyo?

Kwa hiyo wanataka kutwaminisha kwamba Sisi huku tunaishi maisha yalivyo zaidi ya kuuwana siyo?
 
Unafahamu maana ya kushika mkia?,
si ajabu wewe ni mshika mkia huko shuleni kwenu.

Anyway, yaani Jiji LA Roma huko Italy na Wuhan nchini China yaliyokumbwa na Corona yawe na furaha kuliko Dar es salaam kweli?

Jiji LA Kigali, Kamapala na Nairobi ambayo yapo katika Karantini Hakuna kutoka wala kuingia yatuzidi furaha wana Daresalamu?

Kigezo cha kuzuia Shisha na Ushoga Dar es salaam ndipo Mabeberu wanatuaminisha kwamba Dar Hakuna Furaha wakati mabasi yote yanajaza watu Dar salaam, Treni, Meli na Ndege zote zinajaza kuingia Dar es salaam.

Dar ni Jiji LA Raha na furaha, tuachieni Jiji letu
Akili za kuambiwa changanya na zako.
 
Ipo tofauti kati ya Raha na Furaha.

Vitani wapo wenye furaha lakini hawana raha!

Kadhalika kuna tofauti kati ya mbwiga na kushika mkia

Mbwiga ni yule mwanafunzi wa mwisho darasani mfano wa 186 kati ya 186 NA kushika mkia ni kundi la mwisho kwa ufaulu kwa mfano wanaopata daraja sifuri kwenye mitihani au zile timu 4 zinazoshuka daraja kwenye ligi kuu.
 
Hawa waongo
Au itakua data za Libya zlichukuliwa kipind gadaph yupo madarakan

Ila sio hali ya sasa hiv
Ktu kingne hiz mamlaka sio za kuziamin saana sometimes wana spread propaganda kwa madhumuni yao

Aman ya Libya ya sasa hvi uwez fananisha hata ya uganda au nchi yeyote ya A. Masharik
 
Back
Top Bottom