Bishanga
JF-Expert Member
- Jun 29, 2008
- 15,321
- 10,075
Hivi ninavyofungua huu uzi kuna kijana jirani yangu yamemkuta. Yeye ni mmoja wa wale wanaoitwa 'watoto wa nje' (neno hili silipendi kabisa,kwangu mtoto ni mtoto tu). Mzee wake amefariki hakuacha wosia. Sasa mke wa marehemu na wanae wa kuzaa wamegangamala wanasema mtoto wa 'nje' kisheria hana haki ya kurithi chochote.It is too sad maana hata baba yake alikuwa anampenda sana kijana huyu na bado hajamaliza shule.Kwa wale watu wazima chonde chonde jamani tuandike will ili mali yetu tuigawe kulingana na utashi wetu. Na kwa vijana wakumbusheni wazazi wenu kuandika will wala msiogope kuwambia,ni kwa faida ya wanandugu wote na kupunguza mizozo isiyo na lazima.