Umuhimu wa sensa kwa Rais Samia

Rashda Zunde

Senior Member
May 28, 2022
199
231
Kamisa wa sensa nchini, Anne Makinda amesema Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti, mwaka huu, itakapokamilika itaisaidia serikali na kumpa Rais Samia Suluhu Hassan picha halisi ya nchi anayoiongoza.

Alisema hayo alipokuwa akizungumza na wakufunzi wa sensa wa ngazi ya taifa wanaoendelea na mafunzo mjini Iringa.

Wakufunzi hao zaidi ya 400 watatumika kutoa mafunzo kwa wakufunzi wa ngazi ya mikoa na wilaya ili kufanikisha kazi hiyo Agosti 23, mwaka huu.

“Rais anataka aone nchi anayoiongoza inafananaje, kwa kupitia sensa hii atapata picha halisi itakayomsaidia kumuwezesha kufanya mambo yatakayomgusa kila Mtanzania na maendeleo yake na ya taifa,” alisema Makinda.
 
MZanzibar
Muislam
Mwanamke.
Raisi huyu ameletwa na mungu baada ya kupita kipindi cha giza!
Atapuuzwa sana ila mungu ni fundi
 
Back
Top Bottom