DC Shaka: Rais Samia amewaaibisha waliombeza

MTANZANIA620

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
105
Reaction score
116
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mhe. Shaka Hamdu Shaka, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewaibisha waliombeza waliokuwa wakidhani kuwa asingeliweza kuendeleza miradi ya kimkakati ya Taifa.

Shaka amesema wakati Mhe. Rais Samia anaingia madarakani, licha ya changamoto kubwa za UVIKO-19, ukame na mitikisiko ya kiuchumi duniani, hakuna mradi hata mmoja wa kimkakati uliokwama wala kusimamishwa. Kila mradi umeendelea kwa kasi na matokeo yake yako wazi na yanaonekana kwa macho ya kila Mtanzania.

"Ili kujenga Taifa lenye umoja na amani, Mhe. Rais Samia ameweka mwelekeo wa kutimiza malengo yanayoendana na vipaumbele vya kimkakati vya Taifa, ikiwemo Dira ya Maendeleo, Mipango ya Ukuaji wa Uchumi na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi," alisema Shaka.

Akizungumza katika Viwanja vya Uzinduzi wa Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma alipotakiwa kutoa maoni yake, Shaka amesema kuwa Mhe. Rais Samia ameithibitishia Dunia kuwa yeye ni kiongozi mchapakazi, mzalendo aliyepevuka kisiasa, mwenye uzoefu na ukongwe wa uongozi.

"Hahitaji siasa zisizo na afya, siasa za kupwaya na kukosa uvumilivu. Anahitaji siasa safi zinazoambatana na shauku ya kutekeleza miradi ya kimkakati ya maendeleo. Ushahidi ni kuzinduliwa kwa Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma. Huu si ujenzi tu wa majengo, bali ni ujenzi wa heshima na utambulisho wa Taifa letu," alisema Shaka.

Shaka amebainisha kuwa Watanzania wana kila sababu ya kumuunga mkono Dkt. Samia kwa asilimia 100. Ameonyesha uongozi wa vitendo kwa kuendeleza Dira ya Mwalimu Julius K. Nyerere na kutimiza ndoto ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

"Mji huu utaongeza ajira kwa vijana, utaleta huduma karibu na wananchi, na utaifanya Dodoma kuwa Jiji la kweli la Kidiplomasia. Haya yote yametokana na dhamira yake ya dhati, uthubutu, na uzalendo wa kweli," aliongeza.

Kwa mujibu wa Shaka, huo ni uthibitisho wa kweli kwamba Dodoma si Makao Makuu kwa maneno tu, bali ni kwa vitendo.

"Kwa hili, Mhe. Rais Dkt. Samia ameithibitishia Afrika na Dunia kuwa Watanzania tukiamua, tunaweza kwa kishindo na kwa mafanikio makubwa. Mji huu wa Serikali ni alama ya uwezo wa Mtanzania kujenga nchi yake mwenyewe," alihitimisha Shaka.

Pandikizi toka Mchambawima hilo, hstutegemei chochote toka kwao.
 
Kwani mema Hana unadhani?
Anayo sana.
Shida utekaji na kuwapa kesi watu wa upinzani ndo vinamuharibia.
 
Back
Top Bottom