Umuhimu wa kutozima Simu usiku

Mimi kabla ya kupanda kitandani nazim simu . Ndio utaratibu niliojiwekea. Naheshimu usingizi wangu.

BTW, kwani wazee wetu zamani hizo mbona waliishi bila simu na maisha yalisonga mbele.!?
 
Licha ya thawabu hata likitokea la Kutokea jirani ndo wa kwanza kukuhabarisha
Nakumbu Uncle alifariki usiku wa saa 6 pale sinza, mama mkubwa anakaa G'mboto, asbh kajiandaa anaenda zake Kisarawe ofisini kwake. Anafika minaki ndiyo anapatikana wakamuuliza vipi mbona hukupatikana usiku kucha. Akajibu nilizima simu wakati huo watu wa Moro wameshafika kitambo. Tukamuuliza unazimaje simu mtu mzima wewe umeona sasa.
 
Chezea simu weye, hata polisi jamiii wenyewe wanakuambia majirani mpeane namba za simu hata likitokea lolote usiku mnaamshana
 
Sizimi lakini naiweka silent. Ni sawa na kuzima tu. Ukipiga haunipati. Nikiacha sauti silali. Na huwa nikiamshwa usiku toka usingizini, huwa silali tena. Nisipolala kwa muda mrefu itaathiri afya yangu. Eti kwa kusubiri simu moja ya dharura katika miaka 10 ama 20. Kwa kweli ukinitafuta usiku hautanipata. Sorry.

Zamani wakati simu zimeanza kuingia kwa mara ya kwanza, nilikuwa naiacha on. Halafu wanafunzi wakawa wanapiga kusalimia saa 8, 9, 11, usiku kwa vile kupiga saa hizo ilikuwa bei rahisi kwao. Na wengine walikuwa wanapiga wrong number. Mtu anakuamsha saa 10 usiku, halafu haumjui ama eti anakusalimia. Imagine!
 
Yaani usizime simu kwa miaka 20 ili mtu mmoja akifa usiku saa 6 ktk miaka hiyo 20 upate taarifa muda huo? Kweli? Au kila baada ya siku 3 unapigiwa simu ya mtu kufariki saa 6 usiku?
 
Yaani usizime simu kwa miaka 20 ili mtu mmoja akifa usiku saa 6 ktk miaka hiyo 20 upate taarifa muda huo? Kweli? Au kila baada ya siku 3 unapigiwa simu ya mtu kufariki saa 6 usiku?
Kama nimekusoma umesema wanafunzi wanakupigia simu usiku, mimi boss wangu hawezi kunipigia simu usiku wala sina mwanafunzi.anipigiae usiku.Siku moja moja napiga simu huko kwenye asili yetu teeena mwisho saa tatu baada ya hapo simu ipo kimya ukiona sms ujue tigo au voda na matangazo yao mkuu.Na simu ya usiku ujue zaidi ya 3 au 4 ujue ni janga la haja siyo mchezo
 
Note: Nyumba yangu
 
Ishu niliyokujibu ni ya kuacha simu wazi ili kukiwa na msiba wa 6 usiku usikupite. Usijifanye kichaa.
 
Umeongea UPUPU
 
Nimepokea simu nyingi za matatizo ya ndugu na jamaa zangu muhimu USIKU. Kuna yale ambayo unajikuta wewe ndio msaada wao na yale ya KIFO ambayo yatakufanya uwahi sehemu ya tukio.
Mfano Muislam akifariki usiku basi mapema kesho yake anazikwa, unapozima simu taarifa hizo utapata wakati washazika na utajiona mjinga wakati ungewahi hata kuzika.
Kuzima simu USIKU NI UPUMBAVU.
 
Kuacha simu wazi kwa miaka 10-20 ili upate habari za msiba mmoja usiku, ni upumbavu zaidi. Labda kama huko kwenu kuna watu wanakufa usiku kila baada ya siku 2-3.
Kuzima simu USIKU NI UPUMBAVU.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…