SoC03 Umuhimu wa kamera za ulinzi (cctv camera) katika vyombo vya usafiri wa umma na vituo vyake hapa nchini

Stories of Change - 2023 Competition

Kaka Ibrah

Member
Sep 6, 2022
83
63
UTANGULIZI
Suala la usalama wa abiria ndani ya vyombo vya usafiri ni muhimu sana na linapaswa kupewa kipaumbele zaidi tofauti na jinsi ambavyo limekuwa likisimamiwa na mamlaka husika (Road traffic police), maana abiria ni watu na watu ndiyo nguvu kazi ya taifa letu katika mambo yote. Lakini si tu kwaajili ya usalama wa abiria ndani ya vyombo vya usafiri, la, bali pia kwa ajili ya usalama wa raia watembeao kwa miguu.

IMG_4660.jpg

Chanzo picha: www.backyardscrystals.com

Kufuatia ongezeko kubwa la idadi ya watu hapa nchi, imepelekea pia kuongezeka kwa vyombo vya usafiri binafsi na vyombo vya usafiri wa umma ili kukidhi suala la usafirishaji wa abiria na mali zao. Tofauti na zamani, sasa twashuhudia idadi kubwa ya abiria katika vituo vya usafiri (bus stations), msululu mkubwa wa magari na pikipiki barabarani katika miji mikubwa katika mizunguko ama wakati wa kuingia na kutoka mjini. Vilevile pia katika barabara au njia kuu magari ni mengi sana siku hizi. Hali hii imepelekea kuwepo kwa hofu ya uhakika wa usalama katika safari za watu.

foleni.jpg

Chanzo picha: www.mtanzania.co.tz

Hofu ya kutokuwepo kwa uhakika wa usalama katika safari za watu ama abiria imekuwa ni kubwa sana, na hii imechangiwa na mambo mbalimbali, mfano:
Mashindano kati ya madereva barabarani; Madereva wa magari hasa waendeshao magari ya abiria (buses), wengi wao imekuwa ni desturi kwao kufanya michezo ya kuendesha kwa mashindano magari hayo kwa lengo la kujitafutia sifa na umaarufu kwa abiria na baadhi ya mashabiki wao walio katika baadhi ya vituo vya mabasi. Si rahisi kuamini lakini ni kweli iko hivyo. Maana mashabiki wa madereva hao katika vituo vya mabasi hufanya mchezo wa kubashriri basi gani itakuwa ya kwanza kufika hapa kuanzia saa flani kisha kujipatia fedha, na kisha kumpongeza dereva kwa kiasi cha fedha kama pongezi kwa speed kali. Hii ni hatari sana kwa usalama wa abiria, na ndiyo maana twashuhudia ajari nyingi za barabarani huhusisha haya magari ya abiria.

Chanzo vidio: Vimba Media TV Online

Kujaza abiria ndani ya gari kupita idadi inayotakiwa; Tamaa ya fedha imekuwa ni chanzo cha dereva, konda na miliki nzima ya kampuni ya gari husika kujaza abiria ndani ya gari tofauti na uwezo wa basi jenyewe. Hii imepelekea kutozuilika kwa vifo vya abiria hasa pale inapokuwa imetokea ajari maana wengine hukutwa wakiwa hawajafunga mikanda ya usalama.

EUbox_CXYAAzTHF.jpg

Chanzo picha: Voice of Bongo on Twitter

Ubovu wa miundo mbinu ya barabara kwa baadhi ya maeneo; Kwa kiwango kikubwa serikali yetu imefanya jitihada kubwa katika kuboresha miundombinu ya barabara, lakini bado kuna mambo kadhaa ya kuboresha. Kwamfano; kupanua barabara ambazo ni finye, hasa zili zilizokuwa zikitumika zama za ukoloni. Barabara hizi huleta shida wakati wa kupishana na kupelekea ajari. Madaraja mabovu, pia ni vyema vyote vikarabatie kwa usalama wa watumiaji.

chncdhaHR0cDovL3dpa3JleHBvcnQuY29tL3dwLWNvbnRlbnQvdXBsb2Fkcy8yMDE2LzA4L3JvYWRzLWFmcmljYS10ZXJy...jpg

Chanzo picha: www.muungwana.co.tz

Imani za kishirikina kutumika barabarani; Japokuwa serikali ya nchi yetu haiamini katika imani za ushirikina, lakini Wakristo wanaamini kuwa ushirikina upo, waislamu nao, vivyo hivyo pia kwa wapagani. Lakini wapo watu ambao huamini na kuzisujudia imani za kishetani. Huenda katika njia kuu au njia panda za mabarabara kwa lengo la kupindua magari hasa ya abiria kwa lengo la kutoa kafara kwaajili ya kuipatia miungu yao sadaka ya damu kwa lengo la kuongeza mali au kutoa mikosi. Ni wajibu kwa kila amuabuduye Mungu kufanya sala dhidi ya ajari za barabarani kwa hakika na amina.

Japokuwa ni kweli tuna jeshi la polisi wa usalama barabarani nchini (Road Traffic Police) ambalo linafanya kazi yake kwa weledi kulingana na mafunzo waliyopatiwa ili kupambana ama kudhibiti utokeaji wa ajari za barabarani, ili kuwalinda abiria pamoja na watembeao kwa miguu, lakini bado kunaulazima wa kuwepo kwa njia zingine mbadala ambazo zitatoa mchango mkubwa zaidi wa kuwasaidia askari wa usalama barabarani ili kufanya kazi hii vizuri na kuhakikisha usalama wa abiria watu barabarani unakuwepo wa kutosha. Njia iliyo kuu ni "Kufungwa kwa kamera za ulinzi (CCTV Camera) katika vyombo vya usafiri hasa wa umma pamoja na vituo vyake vyote".

Ongezeko la watu limepelekea pia kuongezeka kwa vyombo vya usafiri kama vile magari, pikipiki, na baiskeli hali ambayo imepelekea kuwepo kwa msongamano mkubwa wa vyombo vya usafiri pamoja na msululu wa watembeao kwa miguu barabarani. Jeshi la usalama barabarani si rahisi kuweza kumudu jambo hili pekeyao, jeshi linahitaji liwe na msaada mbadala. Na msaada huu ni kuwepo kwa kamera za ulinzi katika maeneo yote muhimu. Maeneo hayo ni kama vile; katika vituo vya magari (bus stations), katika vituo vya kuongozea magari kwa njia ya taa, katika njia panda (round about), barabarani, katika vituo vya kukagulia magari ya abiria na hata ya mizigo (mizani), katika barabara mahali pa siri ambako hakuna usimamizi wa traffic, pia ulazima wa kufungwa kwa kamera za ulinzi ndani ya magari ya abiria, sambamba na uwepo wa kituo kikuu cha kusimamia mambo yote yanayokuwa yakiendelea katika mfumo mzima huu wa kamera za ulinzi (CCTV Camera).

Kamera za ulinzi ndani ya vyombo vya usafiri wa umma; Suala la kamera za ulinzi katika vyombo vya usafiri wa umma linapaswa kuwa ni la lazima. Wamiliki wote wa magari ya umma wanapaswa kushinikizwa kufunga kamera za ulinzi katika magari yao. Hili lapaswa lisimamiwe kikamilifu na kitengo cha jeshi la usalama barabarani. Iwapo hili litazingatiwa na kusimamiwa kikamilifu, itasaidia sana na kuondoa uwezekano wa kutokea ajari za barabarani maana magari hayatajaza abiria kupita kiasi kwa kuogopa adhabu kali kama vile faini ama kufungiwa kazi.

Flybus-internal-768x500.jpg

Chanzo picha: www.journeo.com

Kamera za ulinzi katika vituo vya magari ya abiria; Kamera za ulinzi katika vituo vya mabasi na daladala ni muhimu kufungwa kwa ajili ya kulisaidia jeshi la usalama barabarani kuweza kujihakikishia kuwa kunakuwa na usalama wa wasafiri na watu wote wanaokuwa wakiingia na kutoka ndani ya eneo hilo. Hii itahakikisha usalama kuwepo kwani itasaidia watu kuwa na hofu dhidi ya kutaka kufanya uhalifu kama vile vurugu, uporaji mali na hata watu kupamiana kwa magari, wakiamini kuwa mkono wa sheria unawaona.

2018_2$largeimg06_Tuesday_2018_010705024.jpg
CCTV-.jpg

Chanzo picha: www.tribuneindia.com

Kamera za ulinzi katika sehemu za mataa ya kuongozea vyombo vya moto; Pamoja na kuwepo kwa mataa ya kuongozea magari na vyombo vya moto vyote barabarani, lakini bado matukio ya ajari yamekuwa ni changamoto kukoma katika maeneo hayo. Zipo sababu mbalimbali ambazo zimekuwa ni muendelezo wa kutokea kwa matukio ya ajari, mfano; itirafu katika mfumo wa taa za kuongozea, lakini pia utakuta ni kiburi tu cha baadhi ya madereva kuwapamia wengine na kusababisha ajari dhidi ya wengine. Hili linaweza kuzuilika kwa urahisi iwapo kama kamera za ulinzi zitafungwa katika maeneo hayo, kwani itawasaidia askari kuweza kunasa namba za usajili wa chombo husika ambacho kinakuwa kimekiuka sheria za barabarani kisha kutoa adhabu.

2022_2$largeimg_478296110.jpg

Chanzo picha: www.tribuneindia.com

Kamera za ulinzi katika barabara kuu; Ni muhimu pia kufungwa kwa kamera za ulinzi katika barabara kuu ambako magari na vyombo vingine vya moto huenda kasi. Katika maeneo kama haya madereva huenda kasi na kuacha kujali sheria zinginezo zilizo wekwa huko kwa alama za barabarani, jambo ambalo hupelekea kutokea kwa ajari ambazo kwa namna moja ama nyingine zingeweza kuepukika. Lakini uwepo wa kamera za ulinzi barabarani utalisaidia jeshi hilo kutambua makosa na kutekeleza majukumu yake kwa weledi.

1687184352260.png

Chanzo picha: www.alamy.com

Lakini pamoja na kufungwa kwa kamera za ulinzi pasipo kuwa na vituo vya usimamizi, itakuwa ni sawa na bure. Vituo vya jeshi la usalama barabarani ndivyo vitakavyo wajibika ikiwa ni kama jukumu lao. Na kwa maana hiyo basi, vituo vyote hivyo vitalazimika kutengenezewa hiyo teknolojia kwa msaada wa serikali ili kufanya kazi hii kwa ufanisi zaidi. Uwepo wa vituo hivyo utasaidia askari hao kuweza kuwasiliana na kufanya kazi yao kwa uhakika zaidi kwa kuhakikisha wasafiri wote ndani ya vyombo vya moto wako salama na hata waendao kwa miguu.

1345878223222.jpg

Chanzo picha: www.timesofindia.com

Uwepo wa hivi vituo vya kusimamia usalama barabarani kwa njia ya kutumia kamera za ulinzi, ni lazima uambatane na mawasiliano kati ya maaskari (CCTV Camera Police Control Room) na madereva wote wa magari ya abiria. Kama itashindikana kwa magari yote, basi walau hata kwa magari ya abiria yaendayo mkoa mmoja hata mwingine. Na ni vyema mawasiliano atakayokuwa nayo dereva wa basi husika isiwe ni simu yake binafsi, bali iwe ni namba rasmi ya simu ya basi hilo kwa ajili ya kupokea muongozo kutoka kwa maafisa wa usalama barabarani wanaomuongoza mwendo wake katika kamera za ulinzi, kwa lengo la kumpa tahadhari pengine pindi anapokuwa anajisahau.

FAIDA NA UMUHIMU WA KAMERA ZA ULINZI KATIKA MAENEO HAYA

(a) Italisaidia jeshi la usalama barabarani kufanya kazi yake kikamilifu.
(b) Itasaidia kupungua ama kukomesha kabisa ajari za barabarani.
(c) Itasaidia kuondokana na mfumo duni wa kizamani ambao huleta usumbufu mkubwa katika kupata taarifa muhimu za wanaokiuka sheria na taratibu za barabarani.
(d) Hii itaweka ukuta kwa madereva kenge wote kuendesha magari na pikipiki kwa matanuzi ya hovyo.
(e) Itasaidia kuthibitisha ushahidi wa kweli wakati wa kutoa adhabu dhidi ya wahalifu.
(f) Pia itasaidia kukomesha rushwa kwa maafisa wa usalama barabarani.

HITIMISHO
Badala ya jeshi la usalama barabarani (traffic police) kuondokana na dhana potofu iliyopitwa na wakati ya kusubili kupongezwa na serikali kwa kukusanya kiwango kikubwa cha fedha kitokanacho na faini za makosa ya waendesha vyombo vya moto barabarani; sasa nchi yetu itajikusanyia fedha tele za kigeni kutoka kwa watalii, hivyo kuvuta wawekezaji wengi zaidi ndani ya Tanzania kutoka nnje ya nchi, kwani amani na usalama wa usafiri utawapa uhakika wao wa kufanya biashara zao vyema pindi watakapo kuja nchini.

Wimbo huu hapa chini, unazungumzia masuala ya usalama barabarani kutoka kwa ("Afande Sele" akiwa amemshirikisha "Bullet" pamoja na "Dyna Nyange");
Chanzo cha wimbo: Flexible Entertainment Company Online TV
 
Attachments

  • Flybus-internal-768x500.jpg
    Flybus-internal-768x500.jpg
    77.9 KB · Views: 18
  • iStock-1136133554.jpg
    11.9 MB · Views: 19
  • photo.png
    photo.png
    325.4 KB · Views: 18
Andiko liko hapo juu, kura zenu ni muhimu jamani ili tuweze kulifikisha hili swala kwa mamlaka husika maana kwa hali hii tutaisha na machozi hayatakoma machoni mwetu! 😢😢😢
 
UTANGULIZI
Suala la usalama wa abiria ndani ya vyombo vya usafiri ni muhimu sana na linapaswa kupewa kipaumbele zaidi tofauti na jinsi ambavyo limekuwa likisimamiwa na mamlaka husika (Road traffic police), maana abiria ni watu na watu ndiyo nguvu kazi ya taifa letu katika mambo yote. Lakini si tu kwaajili ya usalama wa abiria ndani ya vyombo vya usafiri, la, bali pia kwa ajili ya usalama wa raia watembeao kwa miguu.

View attachment 2662464
Chanzo picha: www.backyardscrystals.com

Kufuatia ongezeko kubwa la idadi ya watu hapa nchi, imepelekea pia kuongezeka kwa vyombo vya usafiri binafsi na vyombo vya usafiri wa umma ili kukidhi suala la usafirishaji wa abiria na mali zao. Tofauti na zamani, sasa twashuhudia idadi kubwa ya abiria katika vituo vya usafiri (bus stations), msululu mkubwa wa magari na pikipiki barabarani katika miji mikubwa katika mizunguko ama wakati wa kuingia na kutoka mjini. Vilevile pia katika barabara au njia kuu magari ni mengi sana siku hizi. Hali hii imepelekea kuwepo kwa hofu ya uhakika wa usalama katika safari za watu.

View attachment 2662467
Chanzo picha: www.mtanzania.co.tz

Hofu ya kutokuwepo kwa uhakika wa usalama katika safari za watu ama abiria imekuwa ni kubwa sana, na hii imechangiwa na mambo mbalimbali, mfano:
Mashindano kati ya madereva barabarani; Madereva wa magari hasa waendeshao magari ya abiria (buses), wengi wao imekuwa ni desturi kwao kufanya michezo ya kuendesha kwa mashindano magari hayo kwa lengo la kujitafutia sifa na umaarufu kwa abiria na baadhi ya mashabiki wao walio katika baadhi ya vituo vya mabasi. Si rahisi kuamini lakini ni kweli iko hivyo. Maana mashabiki wa madereva hao katika vituo vya mabasi hufanya mchezo wa kubashriri basi gani itakuwa ya kwanza kufika hapa kuanzia saa flani kisha kujipatia fedha, na kisha kumpongeza dereva kwa kiasi cha fedha kama pongezi kwa speed kali. Hii ni hatari sana kwa usalama wa abiria, na ndiyo maana twashuhudia ajari nyingi za barabarani huhusisha haya magari ya abiria.

View attachment 2662503
Chanzo vidio: Vimba Media TV Online

Kujaza abiria ndani ya gari kupita idadi inayotakiwa; Tamaa ya fedha imekuwa ni chanzo cha dereva, konda na miliki nzima ya kampuni ya gari husika kujaza abiria ndani ya gari tofauti na uwezo wa basi jenyewe. Hii imepelekea kutozuilika kwa vifo vya abiria hasa pale inapokuwa imetokea ajari maana wengine hukutwa wakiwa hawajafunga mikanda ya usalama.

View attachment 2662521
Chanzo picha: Voice of Bongo on Twitter

Ubovu wa miundo mbinu ya barabara kwa baadhi ya maeneo; Kwa kiwango kikubwa serikali yetu imefanya jitihada kubwa katika kuboresha miundombinu ya barabara, lakini bado kuna mambo kadhaa ya kuboresha. Kwamfano; kupanua barabara ambazo ni finye, hasa zili zilizokuwa zikitumika zama za ukoloni. Barabara hizi huleta shida wakati wa kupishana na kupelekea ajari. Madaraja mabovu, pia ni vyema vyote vikarabatie kwa usalama wa watumiaji.

View attachment 2662525
Chanzo picha: www.muungwana.co.tz

Imani za kishirikina kutumika barabarani; Japokuwa serikali ya nchi yetu haiamini katika imani za ushirikina, lakini Wakristo wanaamini kuwa ushirikina upo, waislamu nao, vivyo hivyo pia kwa wapagani. Lakini wapo watu ambao huamini na kuzisujudia imani za kishetani. Huenda katika njia kuu au njia panda za mabarabara kwa lengo la kupindua magari hasa ya abiria kwa lengo la kutoa kafara kwaajili ya kuipatia miungu yao sadaka ya damu kwa lengo la kuongeza mali au kutoa mikosi. Ni wajibu kwa kila amuabuduye Mungu kufanya sala dhidi ya ajari za barabarani kwa hakika na amina.

Japokuwa ni kweli tuna jeshi la polisi wa usalama barabarani nchini (Road Traffic Police) ambalo linafanya kazi yake kwa weledi kulingana na mafunzo waliyopatiwa ili kupambana ama kudhibiti utokeaji wa ajari za barabarani, ili kuwalinda abiria pamoja na watembeao kwa miguu, lakini bado kunaulazima wa kuwepo kwa njia zingine mbadala ambazo zitatoa mchango mkubwa zaidi wa kuwasaidia askari wa usalama barabarani ili kufanya kazi hii vizuri na kuhakikisha usalama wa abiria watu barabarani unakuwepo wa kutosha. Njia iliyo kuu ni "Kufungwa kwa kamera za ulinzi (CCTV Camera) katika vyombo vya usafiri hasa wa umma pamoja na vituo vyake vyote".

Ongezeko la watu limepelekea pia kuongezeka kwa vyombo vya usafiri kama vile magari, pikipiki, na baiskeli hali ambayo imepelekea kuwepo kwa msongamano mkubwa wa vyombo vya usafiri pamoja na msululu wa watembeao kwa miguu barabarani. Jeshi la usalama barabarani si rahisi kuweza kumudu jambo hili pekeyao, jeshi linahitaji liwe na msaada mbadala. Na msaada huu ni kuwepo kwa kamera za ulinzi katika maeneo yote muhimu. Maeneo hayo ni kama vile; katika vituo vya magari (bus stations), katika vituo vya kuongozea magari kwa njia ya taa, katika njia panda (round about), barabarani, katika vituo vya kukagulia magari ya abiria na hata ya mizigo (mizani), katika barabara mahali pa siri ambako hakuna usimamizi wa traffic, pia ulazima wa kufungwa kwa kamera za ulinzi ndani ya magari ya abiria, sambamba na uwepo wa kituo kikuu cha kusimamia mambo yote yanayokuwa yakiendelea katika mfumo mzima huu wa kamera za ulinzi (CCTV Camera).

Kamera za ulinzi ndani ya vyombo vya usafiri wa umma; Suala la kamera za ulinzi katika vyombo vya usafiri wa umma linapaswa kuwa ni la lazima. Wamiliki wote wa magari ya umma wanapaswa kushinikizwa kufunga kamera za ulinzi katika magari yao. Hili lapaswa lisimamiwe kikamilifu na kitengo cha jeshi la usalama barabarani. Iwapo hili litazingatiwa na kusimamiwa kikamilifu, itasaidia sana na kuondoa uwezekano wa kutokea ajari za barabarani maana magari hayatajaza abiria kupita kiasi kwa kuogopa adhabu kali kama vile faini ama kufungiwa kazi.

View attachment 2662265
Chanzo picha: www.journeo.com

Kamera za ulinzi katika vituo vya magari ya abiria; Kamera za ulinzi katika vituo vya mabasi na daladala ni muhimu kufungwa kwa ajili ya kulisaidia jeshi la usalama barabarani kuweza kujihakikishia kuwa kunakuwa na usalama wa wasafiri na watu wote wanaokuwa wakiingia na kutoka ndani ya eneo hilo. Hii itahakikisha usalama kuwepo kwani itasaidia watu kuwa na hofu dhidi ya kutaka kufanya uhalifu kama vile vurugu, uporaji mali na hata watu kupamiana kwa magari, wakiamini kuwa mkono wa sheria unawaona.

View attachment 2662282View attachment 2662283
Chanzo picha: www.tribuneindia.com

Kamera za ulinzi katika sehemu za mataa ya kuongozea vyombo vya moto; Pamoja na kuwepo kwa mataa ya kuongozea magari na vyombo vya moto vyote barabarani, lakini bado matukio ya ajari yamekuwa ni changamoto kukoma katika maeneo hayo. Zipo sababu mbalimbali ambazo zimekuwa ni muendelezo wa kutokea kwa matukio ya ajari, mfano; itirafu katika mfumo wa taa za kuongozea, lakini pia utakuta ni kiburi tu cha baadhi ya madereva kuwapamia wengine na kusababisha ajari dhidi ya wengine. Hili linaweza kuzuilika kwa urahisi iwapo kama kamera za ulinzi zitafungwa katika maeneo hayo, kwani itawasaidia askari kuweza kunasa namba za usajili wa chombo husika ambacho kinakuwa kimekiuka sheria za barabarani kisha kutoa adhabu.

View attachment 2662399
Chanzo picha: www.tribuneindia.com

Kamera za ulinzi katika barabara kuu; Ni muhimu pia kufungwa kwa kamera za ulinzi katika barabara kuu ambako magari na vyombo vingine vya moto huenda kasi. Katika maeneo kama haya madereva huenda kasi na kuacha kujali sheria zinginezo zilizo wekwa huko kwa alama za barabarani, jambo ambalo hupelekea kutokea kwa ajari ambazo kwa namna moja ama nyingine zingeweza kuepukika. Lakini uwepo wa kamera za ulinzi barabarani utalisaidia jeshi hilo kutambua makosa na kutekeleza majukumu yake kwa weledi.

View attachment 2662418
Chanzo picha: www.alamy.com

Lakini pamoja na kufungwa kwa kamera za ulinzi pasipo kuwa na vituo vya usimamizi, itakuwa ni sawa na bure. Vituo vya jeshi la usalama barabarani ndivyo vitakavyo wajibika ikiwa ni kama jukumu lao. Na kwa maana hiyo basi, vituo vyote hivyo vitalazimika kutengenezewa hiyo teknolojia kwa msaada wa serikali ili kufanya kazi hii kwa ufanisi zaidi. Uwepo wa vituo hivyo utasaidia askari hao kuweza kuwasiliana na kufanya kazi yao kwa uhakika zaidi kwa kuhakikisha wasafiri wote ndani ya vyombo vya moto wako salama na hata waendao kwa miguu.

View attachment 2662434
Chanzo picha: www.timesofindia.com

Uwepo wa hivi vituo vya kusimamia usalama barabarani kwa njia ya kutumia kamera za ulinzi, ni lazima uambatane na mawasiliano kati ya maaskari (CCTV Camera Police Control Room) na madereva wote wa magari ya abiria. Kama itashindikana kwa magari yote, basi walau hata kwa magari ya abiria yaendayo mkoa mmoja hata mwingine. Na ni vyema mawasiliano atakayokuwa nayo dereva wa basi husika isiwe ni simu yake binafsi, bali iwe ni namba rasmi ya simu ya basi hilo kwa ajili ya kupokea muongozo kutoka kwa maafisa wa usalama barabarani wanaomuongoza mwendo wake katika kamera za ulinzi, kwa lengo la kumpa tahadhari pengine pindi anapokuwa anajisahau.

FAIDA NA UMUHIMU WA KAMERA ZA ULINZI KATIKA MAENEO HAYA

(a) Italisaidia jeshi la usalama barabarani kufanya kazi yake kikamilifu.
(b) Itasaidia kupungua ama kukomesha kabisa ajari za barabarani.
(c) Itasaidia kuondokana na mfumo duni wa kizamani ambao huleta usumbufu mkubwa katika kupata taarifa muhimu za wanaokiuka sheria na taratibu za barabarani.
(d) Hii itaweka ukuta kwa madereva kenge wote kuendesha magari na pikipiki kwa matanuzi ya hovyo.
(e) Itasaidia kuthibitisha ushahidi wa kweli wakati wa kutoa adhabu dhidi ya wahalifu.
(f) Pia itasaidia kukomesha rushwa kwa maafisa wa usalama barabarani.

HITIMISHO
Badala ya jeshi la usalama barabarani (traffic police) kuondokana na dhana potofu iliyopitwa na wakati ya kusubili kupongezwa na serikali kwa kukusanya kiwango kikubwa cha fedha kitokanacho na faini za makosa ya waendesha vyombo vya moto barabarani; sasa nchi yetu itajikusanyia fedha tele za kigeni kutoka kwa watalii, hivyo kuvuta wawekezaji wengi zaidi ndani ya Tanzania kutoka nnje ya nchi, kwani amani na usalama wa usafiri utawapa uhakika wao wa kufanya biashara zao vyema pindi watakapo kuja nchini.

Wimbo huu hapa chini, unazungumzia masuala ya usalama barabarani kutoka kwa ("Afande Sele" akiwa amemshirikisha "Bullet" pamoja na "Dyna Nyange");
View attachment 2662553 Chanzo cha wimbo: Flexible Entertainment Company Online TV
Napigia wapi kura nimeipenda hii
 
Hawa wataipiga vita hiyo teknolojia kwakuwa itafichua maovu yao

1687343277607.png
 
Napigia wapi kura nimeipenda hii
Asante, sehemu ya kupigia kura ni hapo chini mwisho wa andiko, kuna sehemu imeandikwa "Vote" halafu kuna kivuli cha kijani ndani yake. Bonyeza hapo kisha kitabadilika rangi na kuwa chekundu na unakuwa umepigia kura kusaidia chapisho hili kuifikia mamlaka husika pamoja na serikali yetu.
 
Nimevote👍
Naendelea kushawishi na wengine
 
Hawa wataipiga vita hiyo teknolojia kwakuwa itafichua maovu yao

View attachment 2664261
Moyo wangu umejawa majonzi ndiyo maana nikaleta andiko hili, ili kuieleza serikali yetu kutokomeza kabisa tabia hiyo, kwani rushwa ni moja kati ya chanzo cha ajari za barabarani. Kwanini na sisi tusiwe mfano wa kuigwa katika hili kwa mataifa mengine jirani na yale ya mbali? Hebu ona wenzetu Rwanda walivyo piga hatua chanya katika usalama wa raia ama abiria barabarani!
 
Back
Top Bottom