SoC03 Usafiri wa barabara katika miji/majiji kwa maendeleo endelevu (mfano kazi jiji la Dar Es Salaam)

Stories of Change - 2023 Competition
Jul 17, 2023
2
1
A: UTANGULIZI.
Usafiri ni hali ya kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa madhumuni mbalimbali.
Maendeleo ni hali ya kukua kifikra, kiuchumi, siasa, kijamii au kiutamaduni kutoka hali duni kwenda hali bora kuliko awali.

Maendeleo endelevu ni maendeleo ambayo kutokea kwake hayana athari kwa ustawi wa jamii na mazingira kwa ujumla.

Miji ni maeneo ya kimakazi, biashara au utawala ambayo huwa na watu zaidi ya elfu mbili na wasiozidi elfu khamsini ambazo huambatana na huduma za kijamii za hadhi ya kati. Mfano Musoma au Bukoba

Majiji ni maeneo ya kimakazi, biashara na utawala ambayo huwa watu zaidi ya laki moja. Mfano Dodoma, Arusha, Dar es Salaam na Mbeya

Usafiri wa barabara ni uhamisho wa watu, bidhaa au malighafi kutoka sehemu moja kwenda nyingne kwa njia ya barabara kwa kutumia vipando vya moto au visivyo vya moto.

Katika nchi yetu ya Tanzania kuna kuna miji na majiji yanayokua kwa kasi ambayo miundombinu yake ya barabara si himilivu kutokana na ukuaji wake au idadi ya watumiaji, mfano wa majiji ni kama Dar es salaam, Arusha , Mwanza na Mbeya.

Hitajio la usafiri katika majiji haya hutofautiana kulingana na siku wengi hutumia usafiriri kulingana na nyakati za shinikizo la hitajio la usafiri ambao ni saa 12:30 asubuhi hadi saa 4:00 asubuhi na wakati wa alasiri kuanzia saa 9:00 hadi saa 3:00 usiku khaswa kwa jiji la Dar es salaam.

Katika majiji foleni imeonekana kuwapa changamoto inayotatiza japokuwa si changamoto ya msingi kama hii ya watu wengi kuwa na uhitajio wa huduma moja kwa wakati mmoja ambayo hupatikana pahala pamoja kila siku na hii ndiyo changamoto ya msingi.

Usafiri wa barabara ndiyo njia kuu ya usafiri inayotumika katika nchi zinazoendelea khaswa katika majiji na miji na hivyo hupelekea sekta ya usafirishaji kulemewa na kutokidhi mahitaji na hivyo kuamua kutafuta usafiri binafsi kitu ambacho huzaa foleni ya barabarani.

Usafirishaji ni nyenzo kuu ya kuchochewa ukuaji wa nyanja zingine, zaidi ya 90% ya wasafiri hutumia barabara na 75% ya mizigo hutumia barabara kuwafikia wateja kwa Tanzania nzima.

B: UWASILISHAJI NA UCHAMBUZI.
Dar es Salaam ni jiji kubwa kuliko yote Tanzania kwani ndio jiji tegemezi kama lango kuu la biashara na uchumi wa kimkakati hii ni sababu ya uwepo wa bandari yenye uwezo kuliko zingine zilizopo. Jiji hili linapatikana kijiografia nyuzi 6°.48' Kusini na 39°.7' mashariki , lina hali ya hewa ya kitropiki yaani unyevunyevu na joto kwa kipindi kirefu cha mwaka. Lina wilaya tano yaani Kigamboni , Temeke, Kinondoni, Ubungo na Ilala.

Sababu za Dar es Salaamu kuwa mfano kazi licha ya uwepo wa majiji mengine.

a). Idadi ya watu zaidi ya milioni 6 (ripoti ya sensa 2022)
b). Msongamano mkubwa wa barabarani.
c). Ina njia zote za usafiri
d). Alfa na omega ya magari ya abiria na mizigo ya nchi nzima.
e). Kitovu cha biashara na uchumi wa kimkakati.

Sababu za watu kusafiri.
1. Kufuata huduma za kijamii
2. Kufanya biashara
3. Utalii
4. Burudani
5. Kuongeza maarifa na ujuzi
6. Kwenda kazini na kurudi majumbani.

CHANGAMOTO ZA USAFIRI KATIKA MIJI/MAJIJI.

  1. Foleni :- Hii husababishwa na misafara rasmi ya viongozi, ongezeko la watu na vyombo vya usafiri, kukua kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na uhaba wa mipango miji inayoendana na wakati.
  2. Ulinzi na usalama :- Tatizo la wizi hasa wakati wa shinikizo la hitajio la usafiri, udharura wa hali mfano magonjwa na majanga kama moto.
  3. Miundombinu usiokidhi hitajio :- Katika majiji tuna miundombinu ambayo haina vitu muhimu kama taa za barabarani, maeneo machache ya maegesho ya magari haswa katika vituo vya kibiashara kama vile kariakoo na pia njia za watumia kwa miguu kutumika isivyo dhamiriwa.
  4. Usafiri mbovu wa umma :- Magari yanayotoa huduma katika majiji (daladaa) yameonekana kutokidhi hitajio la umma kwani mengi ni chakavu kupita kiasi, hayana ratiba maalum, muda mrefu wa kusubiri huduma na pia kukiuka njia elekezi haswa wakati washinikizo la uhitajio wa usafiri.​
  5. Usimamizi mbovu :- Usimamizi wa idara zote zinazohusiana kama vile LATRA, TANROAD, TARURA na jeshi la usalama barabarani zote hizi hazina mfumo unasomana na kila moja ina sheria zake za usimamizi wa barabaran hivyo huleta ukinzani kwa watumiaji.​
  6. Ajali :- Haya ni matukio yasoyakukusudia yenye athari mbaya kwa watumiaji wa barabara husababishwa na uzembe, ulevi na miundombinu isiyo rafiki kwa nyakati zote za matumizi.​

SABABU ZA CHANGAMOTO ZA USAFIRI KATIKA MAJIJI /MAJIJI.

  1. Muundo ya miundombinu kutokidhi hitajio la watumiaji wa usafiri.
  2. Matumizi yasosahihi ya maeneo Tengefu ya barabara. Sera za usafirishaji na usafiri ambazo siyo rafiki.
  3.  Wimbi la uhamiaji kutoa kijijini kwenda katika majiji kwa kujitakia maisha bora.
  4. Kutegemea njia moja ya usafiri haswa barabara na kusahau njia kama reli ambayo hutumika katika majiji mengi kwani yanauwezo wa kubeba abiria wengi kwa wakati mmoja.
  5. Usimamizi ambao unakinzana kutokana na utofauuti wa sheria na kanuni.
  6. Uimara wa vyombo vya usafiri.

VITU VYA KUZINGATIA WAKATI WA UPANGAJI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA KATIKA MAJIJI/MIJI.

  1. Lazima muundo wa makazi ya watu uendane na mipangilio ya jiji na miundombinu yake.
  2. Huduma za kijamii na uchumi ziwe zenye kugawanywa kwa usahihi.
  3. Kipato cha jamii husika
  4. Miundombinu sahihi inayoendana na hali za majiji na idadi ya watumiaji.
  5. Mgawanyo wa njia mbalimbali za usafiri.
  6. Lazima muundo wa ukuwaji wa majiji na miji uzingatiwe kama ni muundo wima au muundo mlalo wa ukuwaji wa miji na majiji.

NJIA ZA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA BARABARA KATIKA MAJIJI AMBAYO HAYAJAPANGIOLIWA.

1. Matengenezo ya barabara na vyombo vya usafiri yawe ya mara kwa mara.

2. Uhusiano wa kisekta yaani kuwe na vituo ambavyo vinaweza kutoa huduma mbalimbali kwa pamoja lengo kupunguza mizunguko ya watu katika jiji.

3. Matengenezo ya mifumo ya maji taka na safi ambayo ni himilivu kwa vipindi vyote vya mwaka.

4. Zuio la utumizi wa magari binafsi kuingia katikati ya jiji na kushawishi matumizi ya magari ya umma na pia mashirika na kampuni yenye wafanyakazi wengi kuwa na magari ya watumishi wao hii itapunguza idadi ya magari pia kuwango cha uchafuzi wa hali ya hewa utapungua.

5. Kupendekeza nishati mbadala kama gesi na umeme kutumika katika taasisi zenye magari zaidi 40 haswa taasisi za umma kama Manispaa na halmashauri.

6. Kuwepo na usimamizi mzuri wa matumizi ya maeneo tengefu yaani maegesho ya magari na njia za waenda kwa miguu.

7. Kukithiri kutoa elimu na kuzidisha uelewa kwa wananchi.

TANBIHI. Tahadhari juu ya njia ya kuongeza barabara kama suluhisho isitumike na isipendelewe kwani hii huzidisha kuvuta na kushawishi watu kununua vipando zaidi na baada muda tuna rudi kwenye tatizo lile lile.

C: HITIMISHO.
Tanzania ni katika nchi zinazoendelea na hivyo zinakabiliwa na ukuwaji mkubwa wa miji na majiji. Hivyo changamoto za usafiri na usafirishaji huweza kusababisha tusifikie lengo la sera ya maendeleo ya mwaka 2050 kama inavyotarajiwa. Hivyo lazima sekta ya usafirishaji ikuzwe kwa kasi kwani ndio nyenzo kuu ya kukuwa kwa sekta zingine zote.

Pia kuhakikisha ukuwaji wa sekta ya usafirishaji hauathiriki mazingira na ili kutekeleza haya kwa haraka lazima serikali ishirikiane na sekta binafsi katika hili yaani (public private partnership).

Pia mabadiliko katika sekta hii yasisahau kushirikisha wadau wa usafirishaji na usafiri na kuunda chombo kimoja kinachojishughulisha na upangaji wa miji na majiji kwa kushirikiana na taasisi zilizopo kama vile TANROAD na TARURA na mwisho uwepo wa sera madhubuti zinazoendana na wakati.
 
Hakuna watu wenye maono hayo zaidi ya kuwaza kuiba, huko UK 1890 walikuwa tayari wana underground railway kukabiliana na foleni, njoo kwetu sasa.

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom