SoC02 Umuhimu wa Afya ya Akili

Stories of Change - 2022 Competition

jackline karata

New Member
Sep 14, 2022
2
1
Taifa na wananchi kwa ujumla tunatakiwa kujua na kuelewa umuhimu wa afya ya akili kwa kila mmoja wetu ....hii itasaidia kupunguza mangonjwa mengi yasioambukizwa na kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na kujiua .

---
“Jamani, nini hiki tena kila siku kujiua na mauaji yamezidi sana!” ilisikika sauti ya mwanamama aitwae Selena mnamo usiku wa saa mbili kamili akiwa anaangalia taarifa ya Habari. “Vipi Selena?” aliuliza Daniel mume wa selena, “nipo naangalia taarifa hapa, kila siku ni mauaji, watu wanajiua, wengine wanauana “alieleza selena akiwa ameshika tamaa. “Hee tena si juzi tuu nilisikia taarifa ya yule kijana aliyejiua, jana tena tukasikia ya mwengine aliyeuawa na mwenzie, leo tena!” Daniel alisema kwa mshangao, “Mungu tuu aturehemu “akajibu Selena kwa masikitiko makubwa.

Selena na Daniel waliishi katika Kijiji cha Runda na walifanikiwa kupata mtoto mmoja aitwae Helena. Helena alikuwa kidato cha pili katika shule ya wasichana ya sekondari Runda. Helena alikuwa na Rafiki yake aitwae Rian.

Rian ni mwanafunzi bora kwenye darasa lake, alikuwa anasoma kwa bidii sana pia alikuwa anafaulu kwa kiwango cha juu ghafla Rian akaanza kufeli kutoka wa kwanza hadi wa hamsini na tano, walimu wake walishindwa kujua sababu ni nini na badala yake walikuwa wanampa adhabu kali sana.

Siku moja Rian alijaribu kujiua kwa kunywa vidonge vingi sana kwa wakati mmoja, wakati wenzake wapo darasani kwa bahati nzuri Dada mkuu wa shule alikuwa anapita maeneo aliyokuwepo Rian, alipata kumuona na kupiga kelele kuita msaada wakafanikiwa kumuokoa.

Hospitalini Daktari akamuuliza baba yake Rian, “Baba kuna tatizo lolote unalohisi linaweza kupelekea Rian akawa katika hali hii?”. “Hapana kwa kweli, sijajua anashida gani” alisema Baba Rian akiwa na majonzi mazito. Baada ya muda mfupi daktari akaenda kuongea na Rian kiurafiki Zaidi, “Rian unajisikiaje kwa sasa?” daktari alimuuliza Rian. “sijui” Rian akajibu. “Rian unaweza ongea na mimi, nini shida kwanini unataka kujiua?” daktari aliuliza tena kwa msisitizo Zaidi.

“Kila kitu kilikuwa sawa mpaka nilipogundua kuwa baba ana kansa, hali ya nyumbani ikaanza kuwa ngumu, baba akaanza kunywa pombe kila siku.

Nina hofu sana juu ya Maisha yake ,sitaki kumpoteza , sina mtu mwengine hapa duniani ninaye mpenda na kumuamini kama yeye , mama alishafariki miaka minne iliyopita “ Rian aliendelea kuelezea huku machozi yakimtoka “ pia sehemu niliyokuwa nategemea kujificha na uhalisia ni masomo yangu , nilikuwa napambana sana kitaaluma ila mwalimu aliponitongoza nikakataa akaanza kunifelisha na kuniwekea vikwazo mbalimbali masomoni , kwanini niendelee kuishi wakati kila nilichokuwa nacho na kinachonipa Faraja kinabomoka siku baada ya siku , maumivu haya ni mazito sana , mazito mno”. Kwa kweli swala la Rian lilimuhuzunisha sana daktari, kiasi cha kwamba akaamua kumpigia simu mwanasaikolojia atakayeweza kumsaidia Rian.

Wiki mbili baada ya kisa cha Rian, Kijijini palitokea mauaji ya wanandoa ambapo mwanaume aitwae Samson alisadikiwa kumuua mkewe aitwae cassie kisha baadae kujiua na yeye. Polisi walifika eneo la tukio na kuwaoji majirani na ndugu za karibu nao walisema sababu kuu ni malumbano kati yao wawili yaliotokea kwa siku kadhaa na nyumbani kwao palikuwa hapana mawasiliano mazuri. kwa upande wa kiafya, hospitalini madaktari wanasema yawezekana vifo hivyo vimesababishwa na matatizo ya akili.

Siku tano baada ya kifo cha wanandoa hao palitokea kifo cha mtoto Gabriel aliyekuwa na umri wa miaka kumi na mbili, mtoto huyo alijinyonga baada tuu ya kugombezwa na mama yake. Polisi walifika eneo la tukio wakashindwa kuelewa nini shida ukiachana na kugombezwa lakini tatizo lilipofika hospitalini wanasaikolojia wakasema yawezekana mtoto huyo alikuwa na matatizo ya akili ambayo hayakugundulika mapema.

Mganga mkuu wa Hospitali ya Kijiji cha Runda akaamua kuitisha kikao kilichowakutanisha madaktari na wanasaikolojia wa sehemu mbalimbali kujadili swala la kujiua na mauaji kuwa mengi , kikao kilichukuwa muda wa masaa mawili na baadae wakatoka na mapendekezo kadhaa ya kwenda kutatua tatizo hili .

Pendekezo la kwanza ni kuelimisha jamii juu ya swala la afya ya akili, aina za afya ya akilli sio uchizi tuu ambao watu wengi wakijua mtu ana matatizo ya akili wanafikiria anao. Matatizo mengine ya afya ya akili ni kama Ugonjwa wa wasiwasi, Ugonjwa wa bipolar, shida ya akili ya kupoteza fahamu, skizofrenia, Usonji, kukosa usingizi na ugonjwa wa mkazo baada ya kiwewe.

Pia elimu itolewe juu ya familia kuwa na mshikamano na mawasiliano ya mara kwa mara, msaada wa kirika haswa kwa vijana, kuwepo kwa Imani za kitamaduni na kidini zinazopinga kujiua na kuhimiza kuishi kwa afya Zaidi. pia jamii inatakiwa kujifunza mbinu mbalimbali za kutatua tatizo na utatuzi wa migogoro. Elimu hii itatolewa kwa njia mbalimbali kama mitandao ya kijamii, redio, televisheni zilizopo majumbani, hospitalini na nyengine kuwekwa masokoni ambapo watu wengi wanapatika na kila baada ya nusu saa matangazo yanayoelimisha jamii juu ya afya ya akili uwekwa kisha kuendelea na vipindi vyengine, pia jamii inaweza kuelimishwa kwa kupitia ubao wa matangazo uliopo barabarani.

Pendekezo la pili ni juu ya walimu na wafanyakazi wa mashuleni ambao wanatakiwa watengeneze mazingira mazuri ambayo yatawafanya wanafunzi kuwa na uhuru wa kueleza taarifa kama hizo au kuwa rahisi kubaini atakapoanza kuonyesha dalili za kujiua ambazo ni kama kubadilisha tabia kwa muda mfupi na kuwa na usemi wa kutaka kujiua mara kwa mara. Walimu pia wanahimizwa kupata mafunzo ya saikolojia hata kwa hatua ndogo itakayowawezesha kutambua na kuelewa tabia za wanafunzi ili kuweza kuwasaidia wanapoitaji msaada badala ya kuwapa adhadu kali, wanajukumu la kuwajenga Watoto kisakolojia Zaidi.

Pendekezo la tatu ni juu ya kutumia ubunifu kama vile michoro, maigizo, michezo, muziki na uandaaji wa matamasha mbalimbali ya kuelimisha jamii juu ya afya ya akili.

Pendekezo la mwisho ni ombi kwa viongozi kwenye ngazi mbalimbali kusaidia uhamasishaji wa wanajamii juu ya afya ya akili, umuhimu wake na pia kutunga sheria ambazo zitailinda afya ya akili ya kila mwananchi kwa kiwango cha juu kwa namna moja au nyengine.

Mapendekezo hayo yalifanyiwa kazi na matokeo yalianza kuonekana ambapo vifo vilianza kupungua idadi na wananchi walianza kuielewa Zaidi juu ya afya ya akili hii ikapelekea furaha, amani, kuelewana na mafanikio Zaidi katika jamii hiyo.


STORI HII IMEANDALIWA NA JACKLINE KARATA
 

Attachments

  • UMUHIMU WA AFYA YA AKILI.docx
    18.4 KB · Views: 2
Back
Top Bottom