Sharbel
JF-Expert Member
- Feb 20, 2020
- 1,693
- 3,277
1.Diploma ni mwaka wa mwisho tu hivyo GPA ni average ya semester mbili tu.1. A-level inaruhusu kufanya makosa kwasababu unaweza feli mwanzoni, mwishoni ukakaza ukafaulu NECTA. GPA ya kila semester inaamua hatma yako kwenye Diploma.
2. Vyuo vingi vya nje havitambui diploma, ni ngumu kwenda bila ACSEE.
3. Diploma ni mwaka 1 zaidi wa kukaa shule. Kumaliza shule mapema kuna faida zake.
4. Mara nyingi A-level ni nafuu kuliko Diploma.
5. Kwa masomo ya sayansi na uhandisi, A-level inajenga msingi mzuri sana wa hisabati na fizikia. Haya masomo yanafundishwa Diploma ila wanafunzi hawashurutishwi(fimbo😁) mwishowe wanashika machache.
Hayo ni maoni yangu kama mtu wa Diploma.
2. Uongo vyuo vingi tu huko nje vinatambua Diploma, tena huko nje, wale waliopita diploma wanasoma miaka michache degree.
3. Sio diploma zote ni miaka 3
4. Ni sawa Diploma ni gharama
5.Ujue kwenye kazi hizo za science hazitaki maneno, ni mwendo wa kazi tu, hapo wengine wenye theory kichwani hawajui kufanya application.