Umri wa mtu kuteuliwa kushika nafasi yoyote Serikalini uwe ni walau kuanzia miaka 35

Kwa mantiki hiyo unataka utuaminishe kuwa wanaohombea wasiwekewe sharti ya elimu wala umri. Alafu hapohapo wanaopiga kura wawe kuanzia miaka 18+..!? Hhahahhhaa sasa hizo zitakua hesabu za wapi bwa shee??

Tumebarikiwa akili na utashi kiasi ili maisha yetu yaende vizuri tuweze kupangilia mambo. Na ndio tukawekewa utaratibu kuwa kila jambo lina Wenye. Sasa hii wenye hii ndio hizo qualifications and qualities
 
Kuhusu sabaya na bashite ishu sio umri bali ushamba na kubebwa na magu
 
Shida ambayo nimegundua ni kwamba vyama vya siasa especially the goddamn CCM, wanachagua disciples wao kwa kutazama vijana viherehere na wajuaji na kuacha wenye hekima na utulivu wa akili.

Katika akili ya kawaida, huwezi kukuta mtu kama mimi nina hangaika na siasa kushindana na wengine kugombea nafasi ambazo kuzipata kuna kujuana kwingi na ili upate cheo basi ni ulambe miguu ya waliokutangulia au ukubali kudhalilika ndipo upite, mimi bado sijafikia kiwango hicho cha kujishusha.

But upande mwingine, wale wenye vipaji vya kweli vya uongozi, tusifunjike mioyo. Platforms zipo nyingi sana ukitoa majukwaa ya vyama vya siasa. Politics ni game pana sana na kama una madini ya kusaidia jamii yetu then nafasi ipo nje ya vyama vya siasa.
 
Hao kina Baahite na Sabaya ni zao tu la kupewa madaraka yanayowazidi umri.
Bashite tokea hata hajawa mkuu wa wilaya wala hata hajawa pale CCM kwenye UVCCM. Akiwa chuo cha ushirika kama waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi nilijua tu hapa hakuna kiongozi bali kuna mtu anae tafuta kuwa superstar kupitia vyeo vya kisiasa.
 
Kwa mantiki hiyo unataka utuaminishe kuwa wanao[g]ombea wasiwekewe sharti ya elimu wala umri. Alafu hapohapo wanaopiga kura wawe kuanzia miaka 18+
Ndio. Ni kwa vile hudhaniwa kwamba mtu yeyote asiyefikia umri wa miaka 18 ni mtoto asiye mtu mzima, na wala akili zake hazijatimia bado.

Sekunde anayotimiza umri wa miaka 18 shurti aweze kupata stahiki zote za haki na wajibu wa mtu mzima. Iweje tena tuanze kumuwekea mizengwe kwamba hiki au kile asigombee?
 
Miaka 35 bado ni kijana sana kichwani. Kina Malcom X, Martin Luther, Nyerere ni watu wenye vipaji maalum na hutokea mara chache wakaishi.

35 bado ana akili za kujirusha, anajiona mwepesi kimwili na kiakili, mfano ndio hawa kina Sabaya na Makonda.
 
Hapa unamuogelea Makonda, Sabaya au Ally Hapi au wote

Vija a wametuangusha sana yaani wamefeli mbaya
 
Duuuh nyerere aliula at 38 ni presidaa


Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…