Umoja wa vyama 10 vya upinzani nchini Tanzania vimefungua kesi Mahakamani Kuu kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa

#ZittoKABWE: Mwaka 2017-2018 alisema "Serikali haileti miswaada ili ijadiliwe bungeni"...!!

#Huyo huyo Zitto Kabwe mwaka huu 2019 amesema kwamba, wanakwenda mahakamani kuizuia serikali isilepeleke "mswaada wa marekebisho ya vyama vya siasa nchini" ili ukajadiliwe bungeni...!!

#Ukiambiwa jambo na mwanasiasa wa upinzani hapa Tanzania,,, changanya na za kwako...!!View attachment 985484
Calvin ungependeza sana kuwa baa unachoma mishikaki na kuuza makongoro, huku siyo kwako wala haufanani nako, mbona Rombo, Mwika na Marangu zipo baa nzuri tu zinahitaji wachoma nyama nadhifu kama wewe!
 
Katika moja ya vitu ambavyo vyama vya upinzani vimekuwa vikipigia kelele mara kwa mara ni kuwa mihimili iheshimiane na kutekeleza majukumu yake. Lakini kufuatia kufunguliwa kwa hati ya dharura mahakamani kudai kuondolewa kwa mswada wa vyama vya siasa ambao bado haujapitishwa, ni kutoheshimu na kuyaamini maamuzi ya Bunge. Wabunge ndio wenye haki ya kuukubali au kuukataa mswada unaopelekwa Bungeni kwa kura.
Sasa je! ni sheria ipi inayoruhushu mtu asiye mbunge (Umoja wa vyama vya siasa unaoundwa na baadhi ya wajumbe wasio wabunge) kupinga au kukubali mswada Bungeni. Hashim Rungwe, Fatma Karume, Lowasa, Maalim Seif hao wote si wabunge wapange mswada ukubaliwe au ukataliwe! Kwanini wasingoje Bungeni waupinge kama wanavyotaka kufanya?
MIHIMILI IHESHIMIWE!
Kama kikatokea chama fulani cha wahuni, kikawa na wabunge wengi, halafu serikali ya chama hicho ikapeleka bungeni mswada kuwa serikali inapendekeza kusiwepo uchaguzi; kwa fikra zako wewe, wananchi wote wanatakiwa kukaa kimya kwa sababu kuna wabunge wataenda kuujadili wakati unajua kabisa kuwa wabunge wale wapo kwenye genge lile lile la wahuni?

Zinatakiwa kutumika njia zote ili kuondoa mambo ya kihuni ambayo serikali inaweza kukusudia kuyafanya kuwa sheria dhidi ya watu wake.

Bunge litumike kupinga uhuni. Likishindwa Bunge, mahakama itumike. Mahakama ikishindwa, nguvu ya wananchi itumike. Ni lazima kuukataa utumwa, kuukataa udikteta, kuukataa uonevu, kuukataa ubaguzi wa namna yoyote ile, kukataa watu kutekwa, kupotezwa, kuuawa kama kuku, kukataa vyombo vya usalama kutumika katika njama za kisiasa.

Hakuna aliye juu ya umma. Bunge ni taasisi ndogo sana ikilinganishwa na umma wa wananchi. Bunge linapogeuka kuwa kama kikundi cha propaganda cha chama, wananchi wakiamua wanaweza kufutilia mbali hata Bunge.

Juu ya wote, hata juu ya Rais, kuna umma, ndio wenye uamuzi wa mwisho.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viongozi waandamizi wa vyama mbalimbali vya upinzani leo watazungumza na waandishi wa habari. Watazungumzia maazimio ya #Azimio la Zanzibar.

Muda: Saa tano kamili asubuhi

Eneo: Makao Makuu ya CHAUMMA, Makumbusho, Dar es salaam.

======

UPDATES;

Viongozi Waandamizi wa Vyama mbalimbali vya Upinzani ACT, CUF na CHAUMMA wamefungua kesi Mahakama Kuu ya TZ Kanda ya DSM kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa kujadiliwa na Bunge kwa minajili ya kupitishwa kuwa sheria, kesi hiyo itatajwa kesho kwa mara ya kwanza.

Wanataka muswada wa vyama vya siasa ujadiliwe kabla ya kupitishwa kuwa sheria itakayozuia vyama hivyo visifanye mikutano ya hadhara.

Vyama mbadala tumefanya juhudi kupinga mswada huu, tumetoka matamko, tumeshirikisha nchi wahisahi, mashirika ya kimataifa, AZAKI hapa nchini na viongozi wa dini, hizi ndizo hatua tumechukua kupinga.

Serikali imepeleka bungeni muswada wa sheria ya vyama vya siasa unaohalalisha agizo la Rais Magufuli mkoani Singinga mwaka 2016 kuzuia mikutano ya vyama vya siasa na kufanya shughuli za kisiasa kuwa suala la jinai. - Zitto Kabwe.

Ni mswada unao kwenda kufifisha nguvu ya vyama vya siasa baada ya vyama vya siasa kuimalika na kuwa na uwezo wa kushindana kwa hoja.

Muswada huo unalenga kumfanya Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa na Mamlaka ya Usimamizi (Regulatory Authority), na kuwa na mamlaka ya kuingilia shughuli za kiutawala na maamuzi ya ndani ya vyama vya siasa ikiwemo kusimamisha / kumfukuza mtu uanachama.


"Hatujajadili suala hili bungeni kama mnavyofahamu bunge limejaa wabunge wa CCM, na wabunge wa CCM wengi ni makasuku"- Kiongozi wa Chama ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.

"Walalamikaji (Applicants) kwa niaba ya vyama ni Waheshimiwa Joran Lwehabura Bashange, Salim Abdalla Rashid Bimani na Zitto Zuberi Kabwe. Mlalamikiwa (Respondent) ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali."


Umoja wa vyama 10 vya upinzani nchini Tanzania vimefungua kesi Mahakamani Kuu ya Tanzania kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa kujadiliwa na Bunge kwa ajili ya kuupitishwa kuwa sheria.

Kesi hiyo imefunguliwa Desemba 20,2018 ikitarajiwa kuanza kusikilizwa kesho Ijumaa Januari 4,2019 huku mlalamikiwa akiwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akisoma tamko la umoja huo leo Alhamisi Januari 03, 2019, Kiongozi wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesema muswada huo unakinzana na Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 hivyo ni muhimu kwao kuupinga.

Amesema muswada huo unalenga kuvikandamiza vyama vya siasa na kufanya shughuli zote za kisiasa kuwa jinai.

“Tunawaomba wanachama wetu wote kesho tufike kwa wingi mahakamani kusikiliza kesi hii, wanademokrasia waone kwamba hatujakaa tunachukua hatua,” amesema Zitto.
=========​
Imefunguliwa Mahakama Kuu ya Tanzania, case no. 31/2018 ipo mbele ya jopo la majaji 3, Sehel, J., Maghimbi, J., na Masoud, J.

hamna kituhapo
 
Wataungana kila uchwao ila muungano wa kinafiki. Muda ndio muamuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa,unawashauri,unawapinga au unawashambulia. Mara nyingi mmewasema watu wanaokosoa uongozi wa Rais,na kuwaona siyo wazalendo,mkawataka wamshauri. Waliopeleka kesi ya kupinga huo muswada ni viongozi,wana watu zaidi ya 6m nyuma yao. mbona mnawapinga na kufurahia kitachowapata? Je nanyi siyo wazalendo,au asiye mzalendo ni yule anayempinga Rais tu? Alafu oooooh watanzania tuungane kupambana na wazungu! Wakati ninyi ndiyo mnaoligawa taifa. Uvccm kule kigoma wanataka kuandamana kutaka uhamiaji kuangalia uraia wa zito Kabwe. Je hii ni akili timamu? Zito amekuwa kiongozi miaka mingapi,hao uhamiaji walikuwa wapi? Basi kama Zito siyo mtanzania,nchi haiko Salama. Yaelekea kila taasisi INA mamluki toka nje ya nchi wanafanyakazi bila taasisi za ulinzi na usalama kujua. Je wategemea wanaomuamini zito na kuamini kuwa ni mtanzania wataungana nanyi kupigana na wazungu vita mnayoiita ya kiuchumi? Mfalme suleman,aliomba hekima na akapewa,ALIJUA KUWA AKILI ANAZO. NINYI OMBENI AKILI MTAPEWA TENA BUREEEE,MUNGU NI MUAMINIFU NAYE ATAFANYA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom