Umoja wa mechanical engineers Tanzania (TME), tunaomba mashine zote za uzalishaji zisamehewe kodi

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Uzalishaji ndiyo nguzo kuu ya uchumi katika nchi yoyote na nguzo kuu za uzalishaji katika nchi ni mbili. Uzalishaji wa kilimo na uzalishaji wa bidhaa za viwandani.

Mechanical engineers ndiyo nguzo ya uzalishaji wa viwandani na sisi tunaiomba serikali yetu iweke msamaha wa kodi katika mashine zote za kuzalisha bidhaa za viwandani.

hatua hii itasaidia kuchochea uzalishaji wa bidhaa hapa hapa kwetu badala ya kuagiza bidhaa nje.

zipo faida kuu mbili za kuzalisha bidhaa hapa hapa kwetu kwani
1. kupunguza imports na hivyo kujenga uchumi wetu na
2. kutengeneza ajira kwa watu wetu.

bidhaa nyingi zilizojaa kwenye masoko yetu ni imports za finished goods na sisi tunaona kabisa ni fursa nzuri sana kulisukuma soko hili kwa watanzania wenyewe kuzalisha bidhaa hizi. pa kuanzia ni kuweka mazingira rafiki katika kuagiza mashine na kuanzisha uzalishaji.
 
Back
Top Bottom