Tanzania kuanza uzalishaji wa Dawa za Kufubaza Makali ya VVU (ARV)

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Ziara ya kimkakati iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan nchini India, imezaa matunda katika sekta ya afya baada ya nchi hizo mbili kuingia makubaliano ya kuanzisha kiwanda cha dawa, huku dawa za kufubaza makali ya virusi vya Ukimwi ARV ni miongoni mwa zitakazozalishwa.

Makubaliano hayo ya ushirikiano wa kuboresha huduma za afya na uzalishaji wa bidhaa za afya nchini Tanzania, utahusisha pia uzalishaji wa dawa za wanyama.

Akizungumza na Mwananchi jana, Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daudi Msasi alisema kilichosainiwa ni makubaliano ya kumwezesha mwekezaji kuanzisha kiwanda kitakachozalisha dawa za binadamu na wanyama.

“Kampuni hii ya Hester Bioscience itawekeza Sh24 bilioni katika kuanzisha kiwanda husika, dawa zinazotarajiwa kuzalishwa zitahusisha antibiotiki, ARV, vichocheo yaani dawa za homoni na zile za maumivu.

“Mwekezaji huyu tayari ana kiwanda kingine nchini kinachozisha chanjo za wanyama kilichogharimu jumla ya Sh48 bilioni,” amesema Msasi.

Mfamasia huyo amesema mkataba uliosainiwa utasaidia uwekezaji wa haraka kwa kumrahisishia mwekezaji kumsaidia katika upatikanaji wa vibali mbalimbali vinavyohitajika kutoka mamlaka na taasisi za Serikali.

Kwa upande wa kupata vyeti vya ubora wa bidhaa husika na kuweza kuuza kwa Bohari ya Dawa (MSD), Msasi alisema kutazingatia sheria zilizopo za nchi.

Shughuli ya kusaini hati za makubaliano hayo ilishuhudiwa na Rais Samia Oktoba 10 mwaka huu ambapo kwa Wizara ya Afya Katibu Mkuu, Dk John Jingu alisaini hati za makubaliano na taasisi za afya nchini India.

Rais Samia alizitaka pande zote zilizoingia makubaliano kuheshimu na kutekeleza masharti ya makubaliano hayo kwa manufaa ya nchi zetu mbili.

Makubaliano hayo yataiwezesha Wizara ya Afya Tanzania kushirikiana na Hospitali ya huduma za kibingwa bobezi za magonjwa ya watoto ya Rainbow kwa ajili ya kuwezesha wataalamu wa magonjwa ya watoto Tanzania kupata mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi.

Pia itashirikiana na Hospitali ya huduma za kibingwa bobezi ya Max Healthcare Group kwa ajili ya kutoa mafunzo ya ubingwa bobezi katika upandikizaji wa ini na upandikizaji wa marudio wa figo.

Pamoja na hayo pia Rais Samia amefanya mazungumzo na Serikali ya India kupitia Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Narendra Modi kuhusu kuanzisha kituo cha dawa asilia.

MWANANCHI
 
Uzuri watu wa nje walishagundua Watawala wa bongo ni mazuzu.

1697205558443.png
 
kichwa cha uzi tu kinafukuza walowekaji kuchangia uzi na kubaki kuwa viewers
 
Nawaasa Vijana wa JF, Ngwengwe isikie kwa mtu.

Hizo kauli, "sikuhizi Ukimwi hauui" ni ukiwa mzima.

Ingia kwenye 18 za mdudu uone.

Zinaa sio Sifa, Epuka Ukimwi kwa Njia zinazoepukika.
Hakuna cha ngwengwe wala ngwenye.

Kwa lifestyle ya Watanzania huo ugonjwa ungekuwa kweli upo hii nchi ingeshaisha.
 
TPI Arusha walikuwa wanazalisha HIV, wakapigwa zengwe na kupatikana wanazalisha dawa feki. Kama hatutakuwa na akili tutaendelea hivi hivi maisha yetu yote.
 
Back
Top Bottom