Miungu yetu ilishindwa, Mizimu yetu ikapigwa, Sasa tumekuwa Jamii iliyoanguka na hatuna Tumaini la kusimama

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
MIUNGU YETU ILISHINDWA, MIZIMU YETU IKAPIGWA, SASA TUMEKUWA JAMII ILIYOANGUKA NA HATUNA TUMAINI TENA LA KUSIMAMA.

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Mila zetu, Desturi zetu, tamaduni zetu, utambulisho wetu na kila kilichokuwa chetu kiliitwa Potofu baada ya kushindwa.
Upotofu upo kwa walioshindwa. Kama tungeshinda katika vita Ile wala istilahi "POTOFU” Isingesikika.
Ni potofu kwa sababu tulishindwa.

Miungu ya Mababu zetu ilishindwa vibaya katika vita ya miungu "god's War" sijajua nini kilipelekea kushindwa kwao. Bado najiuliza.
Je Haikuwa na nguvu ya kutosha kukabiliana na Miungu ya kigeni?
Je Haikuwa na akili na mbinu kabambe za kuwashinda maadui?
Nini kilitokea mpaka Anguko kuu la kutisha lilipotokea ambalo limedumu mpaka leo na hatujui litaendelea mpaka Lini.

Miungu ikishapigwa waumini hawana ujanja tena.
Wakati Ukristo na uislamu unaingia Afrika Wazee na Babu zetu walipambana vilivyo kuukataa kwa nguvu zote lakini ninawasiwasi Miungu yao haikuwapa sapoti ya kutosha kukabiliana na ugeni Ule mbaya.
Au miungu ile ilitoa sapoti lakini haikuwa na nguvu kushinda Maadui waliokuja.

Hatuwezi kusema Waafrika walisaliti miungu yao. Ila ninachokiona ni kuwa miungu ya kiafrika ilizidiwa na haikuwa na nguvu ya kutosha kukabiliana na miungu ya kigeni.

Nakumbuka mpaka nazaliwa zilikuwepo jitihada mbalimbali za wazee wetu wakijitahidi kufurukuta kujaribu kupambana na ujio wa wageni na miungu yao lakini walikuwa wanapambana wakiwa wameshashindwa kwani miungu yao ilikuwa aidha imekimbia au imetekwa au pengine hata kuuawa na miungu ya kigeni.

Miungu ndio imebeba mila, desturi, tamaduni na utambulisho wa jamii husika. Sasa kitendo cha miungu hiyo kupigwa Katiak vita na kufukuzwa au kuangamizwa kabisa kunaiathiri na kuua kabisa desturi , mila na tamaduni ya jamii zao.

Ni mila potofu kwa sababu miungu hiyo imeshindwa.
Ni mila potofu kwa sababu miungu hiyo haina nguvu na haina vigezo na uhalali wa kuitwa miungu.
Ni mila potofu kwa sababu miungu hiyo imeshindwa kutetea Watu wake.
Ni mila potofu kwa sababu miungu hiyo imeshindwa kulinda rasilimali za himaya zao mpaka zinaibiwa na wageni.

Ni mila potofu kwa sababu, miungu hiyo imeshindwa kuwapa Watu wake Akili na kutatua kero na changamoto za jamii yao ikiwemo Umaskini na ujinga.

Miungu na mizimu yako inaposhindwa hauna chochote utakachofanya zaidi ya kujisalimisha kwa miungu ya kigeni.
Ni pigo takatifu ambalo kunyanyuka haiwezekaniki.

Vita ya Miungu, waafrika walipoteza na hatujui miungu yetu ilikimbia, au ipo mateka au iliuawa.
Nyota ya matumaini ya Ukombozi haipo kwa sababu huwezi kukomboa jamii au taifa pasipo Miungu ya kwenu.

Acha Nipumzike sasa.
Nawatakia maandalizi mema ya Sabato.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
TUNAFANYAJE SASA?

Hili ndio swali la msingi.
Tufanyeje?
Hatujui miungu yetu ipo wapi? Imetekwa au iliuawa! Hakuna ajuaye. Kama ilitekwa ikakombolewe. 😀😀 Na itakuwa "vita ya kukomboa miungu yetu"

Kama iliuawa basi ndio hivyo tena tutakuwa watoto Yatima siku zote. Huwezi kuomba mungu wa kigeni akakupa kuliko atakavyompa mwanae. Huwezi kuomba Allah akakupa zaisi kuliko muarabu. Na wala huwezi kumwomba Yehova akakupa kuliko Myahudi.

Mungu Mkuu muumba wa miungu kumfikia nako sio lelemama. Ndio maana ikawepo miungu.
 
Matumizi ya imani hayana msaada wowote mbele ya matumizi ya akili .

Ili uamini hizi imani za kimungu inakupasa ujizime data kwanza yani uwe zuzu.

Asili ya Akili au wazo ni utata mkubwa.
Huwezi kuwa na akili bila nguvu isiyoonekana (miungu) mawazo huwezi kuyadhibiti au kuyazalisha.
Ni kama chembe ya uhai.

Miungu au Mungu ndio hukupa wazo(akili) na kuiweka katika ubongo wako. Kinachobaki ni juu yako.

Miungu na Mungu ndio hutoa mambo yasiyo onekana katika mwili. Kama uhai na Akili.
 
Yote uliyoyasema bado yapo kiimani tu kwa ambae hana hiyo imani yako mambo huwa tofauti.
 
Yote uliyoyasema bado yapo kiimani tu kwa ambae hana hiyo imani yako mambo huwa tofauti.

Hakuna mtu ambaye hana imani.
Bila imani huwezi kuishi.
Imani na akili vinapelekana.

Akili bila imani ni wendawazimu
Na imani bila akili ni wendawazimu.

Labda imani kuhusu nini ndio liwe swali la msingi? Kama ilivyo akili kuhusu nini?

Ndio maana mtu anaweza akapanda ndege ambayo hajaitengeneza yeye, hamjui dereva, lakini kwa imani anajua atafika salama. Sio kwaakili
 
Asante kwa tafakari nzuri.

Ninachokiona hapo ni utata tu kuhusu uelewa kuhusu Mungu. Kimsingi napendelea sana matumizi ya neno MUUMBA kwasababu halileti utata sana kiuelewa. Chukulia Mungu kama sehemu ndogo tu ya uelewa wa Kundi fulani dogo kwenye kundi kubwa la watu kuhusu nguvu ya asili iliyopelekea uwepo wa Kila kitu na MUUMBA kama ukamilifu unaotokana na kujumuisha 'uelewa' hizo ndogondogo kuhusu hiyo nguvu iliyopelekea uwepo wa Kila kitu.

Kwahiyo, kwa dhana ya Mungu utapata sehemu ndogo sana ya hiyo nguvu wakati kwa dhana ya MUUMBA utapata ukamilifu wake.

Aliwahi kusema Credo Mutwa kwamba watu walipojaribu kumuelewa MUUMBA waligundua ni nguvu ambayo haitoshi kwenye vichwa vyao na hivyo wakaamua kuivunjavunja maana yake ili tu waweze kuwa na uelewa fulani. Kutoka hapo ndipo unakuta kuna miungu mingi lakini MUUMBA daima ni mmoja. Lakini pia unakuta Kila Mungu anapewa sofa ya uumbaji. Mimi hupenda sana neno MUUMBA kwasababu hata kimantiki iko wazo kabisa kwamba MUUMBA anatenda kitendo cha KUUMBA na matokeo ya kitendo hicho ndipo tunapata VIUMBE. Unaona huo mtiririko ulivyokaa kimantiki?

Sasa inapotokea watu wamegawanyika katika makundi mengi na Kila kundi lina Mungu wake na watu hao wanaamini katika hiyo miungu yao kama ndiyo yenye nguvu kuliko Mungu wa wengine na wakafikia hatua ya kuhisi wako tofauti kabisa na wenzao ndipo shida ya kutoshirikiana inapotokea. Hapa unakuta Afrika kama eneo lenye makabila mengi na Kila kabila lina Mungu wake na linajiona tofauti na kabila jongine. Wakati huo unakuta Watu hao wageni wakiwa wachache na wameungana chini ya Mungu mmoja hivyo kihalisia wanakuwa na nguvu kubwa.

Sasa ujio wa miungu hiyo ya kigeni haikukabiliana na umoja wa kiafrika ila makundi ya makabila. Wageni walitambua mapema mgawanyiko huo niliofafanua hapo juu na hivyo wakauchochea na kusababisha machafuko na mgawanyiko zaidi baina ya waafrika wa kabila Moja na jengine. Matokeo yake waliweza kuushinda kirahisi kabila Moja baada ya jengine na hata sasa tupo kwenye hali hiyo.

Nini tufanye kama Waafrika?
Kwanza tuungane chini ya uelewa mmoja wa MUUMBA. Tujue kwa hakika ni jinsi gani MUUMBA wetu huyo aliumba ulimwengu huu na kusudi alilotupatia kama Waafrika maana Kila kiumbe kinaumbwa kwa kusudi maalum. Kisha tujue Sheria za asili na tuijue vema familia yetu ya kiafrika kuanzia mababu zetu na jinsi walivyokabiliana na mazingira na hatari za mazingira na hatimaye tujue mahusiano yetu na mazingira na mahusiano baina yetu kama watu.

Mpaka hapo tutaweza kupambana kama wamoja na sio kama makabila au makundi.

Na mimi niishie hapa kwa sasa.
 
Asante kwa tafakari nzuri.

Ninachokiona hapo ni utata tu kuhusu uelewa kuhusu Mungu. Kimsingi napendelea sana matumizi ya neno MUUMBA kwasababu halileti utata sana kiuelewa. Chukulia Mungu kama sehemu ndogo tu ya uelewa wa Kundi fulani dogo kwenye kundi kubwa la watu kuhusu nguvu ya asili iliyopelekea uwepo wa Kila kitu na MUUMBA kama ukamilifu unaotokana na kujumuisha 'uelewa' hizo ndogondogo kuhusu hiyo nguvu iliyopelekea uwepo wa Kila kitu.

Shukran sana mkuu kwa maelezo mazuri.

Swali linakuja, je MUUMBA Hawezi kuimba miungu ya kufanya kazi fulani fulani?
Kwa sababu Muumba sio Mhitaji lakini Mungu ukifuatilia anasifa ya uhitaji kama vile miungu mingi.
 
MIUNGU YETU ILISHINDWA, MIZIMU YETU IKAPIGWA, SASA TUMEKUWA JAMII ILIYOANGUKA NA HATUNA TUMAINI TENA LA KUSIMAMA.

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Nimependa huu uzi, lakini nina mtazamo na Imani tofauti nawewe

Ulipaswa kusema Imani katika miungu yetu ikishindwa, kwasababu hakuna miungu yeyote ya Kizungu wala kiafrika iliyowahi kuwepo kiuhalisia wala kufanya kazi...isipokuwa tu watu ndio walikuwa na Imani hizo ambazo hazipo

Waafrika tulizidiwa Kiakili, Kimbinu na Kiteknolojia

Kama kungekuwa na miungu ifanyayo kazi japo kidogo tu basi isingewezekana Mwafrika kuteswa kwa ku overwork, kutobolewa miguu na kuvalishwa minyororo, Kunyongwa na kuhasiwa

Aidha, isingewezekana Wanaume shababy wa kiafrika wanne au sita kumbeba mkoloni mmoja kutoka Arusha au Mzizima mpaka Tanga na Same kwenye mashamba ya mikonge kisa ana gobole moja tu kibindoni

MASWALI TAFAKURI:

- Kwanini Waafrika hatukujitahidi kwa kutumia akili na maarifa kugundua silaha kama gobole au risasi kuuwa wakoloni watesao ilihali tulikuwa na wafua chuma wengi wa kutosha huko Ugweno, Engaruka, Meroe, Axum na kwingineko? Jibu ni kuwa tulikuwa Wajinga

- Kwanini hatukuwa na UMOJA ilihali ndio Nguvu? Wao walikuwa wachache sana kuliko sisi tena walituma tu wawakilishi wao wakiwa Ulaya, kwanini walitushinda? Jibu ni kuwa tulikuwa wajinga

Huwa nasema kuwa Watu weusi ni jamii Dhaifu kiakili na kimaarifa kuliko jamii zozote katika dunia hii

So, napinga kuwa tulizidiwa kiimani ya kimiungu, Ukweli ni kuwa tulizidiwa kimbinu, kimaarifa na kiteknolojia kama ilivyo hata leo hii.
 
MIUNGU YETU ILISHINDWA, MIZIMU YETU IKAPIGWA, SASA TUMEKUWA JAMII ILIYOANGUKA NA HATUNA TUMAINI TENA LA KUSIMAMA.

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Mila zetu, Desturi zetu, tamaduni zetu, utambulisho wetu na kila kilichokuwa chetu kiliitwa Potofu baada ya kushindwa.
Upotofu upo kwa walioshindwa. Kama tungeshinda katika vita Ile wala istilahi "POTOFU” Isingesikika.
Ni potofu kwa sababu tulishindwa.
Robert please write something kuhusu kuhusu hizi combination za kipumbavu mpya 49 za A level hasa kuhusisha dini kwenye Uga wa secular state
 
Hakuna mtu ambaye hana imani.
Bila imani huwezi kuishi.
Imani na akili vinapelekana.

Akili bila imani ni wendawazimu
Na imani bila akili ni wendawazimu.

Labda imani kuhusu nini ndio liwe swali la msingi? Kama ilivyo akili kuhusu nini?

Ndio maana mtu anaweza akapanda ndege ambayo hajaitengeneza yeye, hamjui dereva, lakini kwa imani anajua

atafika salama. Sio kwaakili

Hakuna mtu ambaye hana imani.
Bila imani huwezi kuishi.
Imani na akili vinapelekana.

Akili bila imani ni wendawazimu
Na imani bila akili ni wendawazimu.

Labda imani kuhusu nini ndio liwe swali la msingi? Kama ilivyo akili kuhusu nini?

Ndio maana mtu anaweza akapanda ndege ambayo hajaitengeneza yeye, hamjui dereva, lakini kwa imani anajua atafika salama. Sio kwaakili
Imani bila akili ni uwandawazimu , imani za kidini na kimiungu hazihitaji akili ,rejea vita ya majimaji . Ndio sababu ya sisi kushindwa kwa sababu wenzetu walitutangulia kuzitumia akili zao vizuri ili kujithibitishia iman zao katika matumizi ya akili.
 
Hilo anguko limetokea wapi? Anguko hili ni la kudhania-hii ndio potosha yenyewe.

Hili bandiko kati ya mengi, limejaa sumu.

Wazungu sio Miungu.

I am proud to be an African and there is absolutely nothing you can do about that.
 
Imani bila akili ni uwandawazimu , imani za kidini na kimiungu hazihitaji akili ,rejea vita ya majimaji . Ndio sababu ya sisi kushindwa kwa sababu wenzetu walitutangulia kuzitumia akili zao vizuri ili kujithibitishia iman zao katika matumizi ya akili.

Ni Kweli.
Imani bila akili huitwa imani potofu.
Akili bila imani huitwa mmomonyoko wa maadili.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom