Ummy Mwalimu awatumbua Mkurugenzi wa Temeke (Mwakabibi) na Mkurugenzi wa Sumbawanga (Msemakweli)

Bwana Lusubilo Mwakabibi DED - TEMEKE, Amesimamishwa rasmi kupisha uchunguzi.

Ni aibu kwa maafisa wa TISS mnaoteuliwa kwenda kuongoza ofisi za Umma, mkageuka waharibifu. Kumbukeni viapo vyenu na miiko ya kazi yenu.

Kumbe jamaa ni TISS? Ndio maana alikuwa mbabe sana...Kufukuza na kufunga waandishi wa habari.
 
Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu amewasimamisha kazi Wakurugenzi wawili.

Wa kwanza ni Nyangi Msemakweli wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Huyu katumbuliwa kwa ubadhirifu wake na usimamizi mbovu wa miradi ya Maendeleo pia alikuwa hana maelewano na Madiwani.

Wa pili ni Lusubilo Mwakabibi, Mkurugenzi wa Manispaa ya temeke. Huyu yeye katumbuliwa kutokana na kuwa na mwenendo usiofaa na matumizi mabaya ya Madaraka.

Mwakabibi ametumbuliwa kutokana na watu kumlalamikia kwa mwenendo usiofaa na matumizi Mabaya ya Madaraka, Ubadhirifu, usimamizi mbovu wa miradi ya Maendeleo Katika Manispaa ya Temeke.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu amewataka Wakurugenzi wote Nchini kuzingatia Mipaka yao ya kazi.

Pia soma hizi:
1) Mkurugenzi wa Temeke, Mwakabibi awasweka ndani waandishi wa habari ili wasihudhurie kikao chake na wafanyabiashara

2) Wizara ya habari kuchunguza tukio la DED wa Temeke kuwaweka chini ya ulinzi waandishi kwa kufika kwenye kikao chake bila mwaliko

3) Wito: ITV isusie kutangaza taarifa zote za Manispaa ya Temeke mpaka pale DED Mwakabibi atakapotimuliwa

4) Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke aache kutisha na kufedhehesha Waandishi wa Habari

5) Mkurugenzi TEMEKE naye akamatwe na ahojiwe



Huyu pimbi lazima aonane na Pilato kabla ya August 30. Nimesikia maagizo ya PM Majaliwa
 
Back
Top Bottom