Ummy Mwalimu awatumbua Mkurugenzi wa Temeke (Mwakabibi) na Mkurugenzi wa Sumbawanga (Msemakweli)

Huyu DED machachali mwenye kelele nyingi za kujifisia hatimae amesimamishwa kazi kwa kushindwa majukumu na ufisadi .

Mwakibinga ambaye alikuwa shabiki mkubwa wa jpm kiasi yeye na mkewe wote kupewa u-DED alijaa tuhumu za ufisadi na ulevi was madaraka huku akionekana kupambana zaidi na DC Gondwe muda wote
View attachment 1763510
Naona ummy sahv hacheki na mtu
Ukizingua anakuzingua
Safi sana ummy

Ova
 
Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu amewasimamisha kazi Wakurugenzi wawili.

Wa kwanza ni Nyangi Msemakweli wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Huyu katumbuliwa kwa ubadhirifu wake na usimamizi mbovu wa miradi ya Maendeleo pia alikuwa hana maelewano na Madiwani.

Wa pili ni Lusubilo Mwakabibi, Mkurugenzi wa Manispaa ya temeke. Huyu yeye katumbuliwa kutokana na kuwa na mwenendo usiofaa na matumizi mabaya ya Madaraka.

Mwakabibi ametumbuliwa kutokana na watu kumlalamikia kwa mwenendo usiofaa na matumizi Mabaya ya Madaraka, Ubadhirifu, usimamizi mbovu wa miradi ya Maendeleo Katika Manispaa ya Temeke.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu amewataka Wakurugenzi wote Nchini kuzingatia Mipaka yao ya kazi.

Soma hizi:
1) Mkurugenzi wa Temeke, Mwakabibi awasweka ndani waandishi wa habari ili wasihudhurie kikao chake na wafanyabiashara

2) Wizara ya habari kuchunguza tukio la DED wa Temeke kuwaweka chini ya ulinzi waandishi kwa kufika kwenye kikao chake bila mwaliko

3) Wito: ITV isusie kutangaza taarifa zote za Manispaa ya Temeke mpaka pale DED Mwakabibi atakapotimuliwa

4) Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke aache kutisha na kufedhehesha Waandishi wa Habari

View attachment 1763482
View attachment 1763546
Magu alikua anawaokotea wapi hawa watu?
 
Mbona jaffo alikua anawaogopa sana wakurugenz halafu ummy mwalimu anawatumbua vizuri tu?..
Madhara ya kuwekeza ktk nafasi za juu za uongozi mbele ya safari km sio kuwa alikua ananufaika na matokeo ya utendaji mbovu na udhukumati....staili hii yabuongozi ni mbaya kabisa. Tenda na ongoza kwa mujibu wa kanuni taratibu hata ukiwa na Malengo makubwa zaidi ya kiongozi, utendaji thabiti utakujenga na kulipa zaidi
 
Tunamtumia barua ya pili ya kumfukuza kwenye idara
Mkuu ikifanikiwa hiyo itakuwa safi sana. Nina imani takukuru watakuwa fair katika kumpekua hilo jinga kubwa. Kumbe Kakonko huko alisababisha mwalimu Mkuu wa Sekondari kujiua. Alikula pesa ya ugenzi wa shule mwalimu alipoenda kuuliza pesa akamruka kimanga. Mwalimu wa watu akajiua.
 
Mkuu ikifanikiwa hiyo itakuwa safi sana. Nina imani takukuru watakuwa fair katika kumpekua hilo jinga kubwa. Kumbe Kakonko huko alisababisha mwalimu Mkuu wa Sekondari kujiua. Alikula pesa ya ugenzi wa shule mwalimu alipoenda kuuliza pesa akamruka kimanga. Mwalimu wa watu akajiua.
Hao kufukuzwa haisaidi
Si ajabu akaunti zao zimenona

Ova
 
Back
Top Bottom