Umeya Dar: CCM waenda tena kortini

Umeya Dar: CCM waenda tena kortini

Ukawa watashinda umeya, mkishapata umeya....onesheni mfano wa kiungozi ili mumrahisishie EL ashinde kirahisi asubuh na mapema 2020
Wataonyeshea wapi wakati mnatumia nguvu kubwa hata kama mmechokwa na wananchi
 
Tunaoijua CCM hatushangai,kwa wale wasioamini kwamba matatizo ya nchi hii huletwa na CCM,sasa ndo muda wa kujiridhisha.
 
1. UDA itawekwa wazi
2. Mabasi yaendayo kasi itakuwa ishu
3. Mabango watu watafungwa
4. Miradi ya jiji itakula gichwa vya watu
5. Treni ya Mwakyembe itawekwa wazi
6. Viwanja vya wazi jipu kuu
7. Etc

UKAWA ikichukuwa madaraka CCM itapata shida sana na hasa waliojipa viwanja vya wazi
Magu angekuwa mzalendo wa kweli angetaka UKAWA ichukue Umeya wa Dar ili iwe kazi rahisi kwake kupata pa kuanzia katika kuchukua hatua.
 
Bora hata wanyama wasio na demokrasia wanaheshimu utawala waliojiwekea kuliko hii ngozi nyeusi laana tupu!

Haki ya mungu ni bora hata nimuombee shetani kuliko hawa watu!!

Waliosema kwenye "human evolution" kuwa tumetokana na "chimpanzee" nakubaliana nao kabisa ila naona bado hatuja-develop(mentally) kiasi cha kutosha na ndio maana tuko hivi.

!
!
Imeongea kwa machungu mno. Nadahani utakuwa mwenzangu katka kumtakia Bwana Donald Trump kila la kheri ashinde urais wa Marekani. Maana hawa wapuuzi wangefanywa vibaya.
 
Kuna tatizo gani umeya wa Dar es salaam ukienda Ukawa? Namba hazidanganyi ndugu zangu ukawa wako 87 ccm wako 76 sasa ccm mlisahau nini ofisi za umeya wa Dar es salaam?
Walisahau mafaili yenye data za kifisadi. Walikuwa na uhakika wa kurudi ofisini. Sasa wanataka wapige foul play moja tu hata kama ya wazi, wakae ofisini japo siku moja 'wasafishe ofisi' then wa-rest in pieces!

Labda ndiyo hivyo. Otherwise, kwa nini wanang'ang'ania? na hii ndiyo sura halisi ya CCM. Wako tayari kufanya lolote al-mradi wapate wanachotaka...kama walivyofanya kule kwenye manukato uakipelagoni!
 
Serikali itende haki kwa wananchi, nchi hii ni yetu sote, CCM na UKAWA wote ni Watanzania, kama wananchi wa mkoa wa Dar es salaam wmechagua UKAWA basi sauti zao ziheshimiwe!
 
Magu angekuwa mzalendo wa kweli angetaka UKAWA ichukue Umeya wa Dar ili iwe kazi rahisi kwake kupata pa kuanzia katika kuchukua hatua.
Uzalendo wa kuigiza tu..ukisikia 'Baba' anasema atahakikisha mwanae ameshiba kabisa ndio ampe chakula mtoto wa kambo ambaye anaishi naye kama mwanae, basi hapo ujue hakuna baba. Ndiyo issue ya Magu ilivyo. Sasa hivi bado ni frenzy and 'ecstasy' ya majipu na pool...yakipoa hayo na pressure na challenges za maisha zikaanza kushika hatamu, rangi halisi za ngozi tutaziona, siyo hizi za pseudo-skin!
 
Viwanja vya wazi 90% ccm wamechukua,Vilivyobaki makadaa wetu wamechukua ,hofu ya kupokwa ni kuu,bora ade punda mZigo ufike
 
Sijui itaishaje hii maana mahakama yaweza kubaliana na hilo ombi lao ati
 
nashangaa mtakatifu mtumbua majipu hakumuona aliefoji hati za mahakama..
au na hilo hahusiki nalo ?
NASHINDWA KUIELEWA MAANA YA DEMOKRASIA kwa mujibu wa CCM..
kule Zanzibar risasi ndio zinachagua viongozi.
 
Bora hata wanyama wasio na demokrasia wanaheshimu utawala waliojiwekea kuliko hii ngozi nyeusi laana tupu!

Haki ya mungu ni bora hata nimuombee shetani kuliko hawa watu!!

Waliosema kwenye "human evolution" kuwa tumetokana na "chimpanzee" nakubaliana nao kabisa ila naona bado hatuja-develop(mentally) kiasi cha kutosha na ndio maana tuko hivi.
Basi weye ni Mzungu mwenye asili ya Gorrila. Kwa sababu za hasira zako za ushabiki wa siasa unatutukana watu.
Kisa?
 
Haya yote anae yaratibu ni makonda, huyu jamaa kumsifia wameharibu kabisa utawala wa kisheria, alimpiga warioba akapewa UDC, amesababisha wapinzani kufunguliwa kesi za kipuuzi nyingine zikisababishwa na hili suala la umeya, amepewa ukuu wa mkoa, sasa anampango ahakikishe meya anatoka ccm hata kama watakufa watu akitegemea kupata uwaziri mkuu, hapa ndipo heshima ya Magufuli inapo chafuka, aache demokrasia ifanye kazi.
 
CCM inatia kinyaa.

Anayetakiwa kulaumiwa ni Rais Magufuli maana suala hili lipo chini ya ofisi yake. Ni wakati wa Watanzania kujua rangi halisi ya Rais wetu katika ujenzi wa misingi ya demokrasia. Rais asome historia na kuelewa saikolojia ya binadamu. Binadamu anaweza kukushangilia na kukupongeza kwa mema 100 uliyotenda na akakulaani kwa ovu moja ulilolitenda.

Tusishabikie uvunjaji wa misingi ya demokrasia bila ya kujali ni nani anayevunja. Rais hata afanye mema 100 lakini akaruhusu Watanzania waongozwe kidikteta, hakuna mtanzania mwenye nia njema na Taifa hili atakayemuunga mkono. Faida ya utumbuaji majipu ni ndogo sana ukilinganisha na hasara ya kukanyaga demokrasia.
 
Basi weye ni Mzungu mwenye asili ya Gorrila. Kwa sababu za hasira zako za ushabiki wa siasa unatutukana watu.
Kisa?
Ina maana waliotufundisha human evolution huko mashuleni walitufundisha matusi?
 
Nashangaa sana magufuli kukaa kimya wakati akijinadi kwamba ni mtoa haki na tuzidi kumuombea.sasavtutamuombeaje mtu ambaye hataki kuwajibika?UKAWA tunaposema hakuna mabadiliko ya kweli ndani ya ccm manyumbu ya lumumba yanakuja juu.
unamanisha,magufuli kesi yake,afanye upelelezi mwenyewe,ajikamate mwenyewe,ajihukumu na kujifunga mwenyewe?
 
Magufuli ashasema hawezi kumpa chakula mtoto wa jirani,wakati wake ana njaa,Dar es salaam ni mtoto wa jirani kwa CCM hawatakiwi kuendelea
 
CCM haitoki kwa vikaratasi ambae hajaelewa sijui ataelewa lini hivi vyama ni kupumbaza watu
 
Namuamini sana mh.Rais ukiachana na chama chake, lakini akishindwa kutenda haki kwenye umeya wa Dar es salaam imani yangu kwake itapungua sana!

Ameshindwa suala la Zanzibar ambalo ni muhimu ataweza hili!? Kama ataliweza basi atatoa maamuzi ya tukose wote.Unafikiri hajui au hasikii sarakasi zinavyopigwa na chama chake ili kukwamisha hili!? Kama ameweza kupiga simu katika Tv na kuwasalimia watangazaji, unadhani hana muda kweli wa kulimaliza hili?. Hivi unafikiri ingekuwa CCM wana wingi wa kura katika huu uchaguzi wange uchelewesha mpaka wakati huu hasa kwa jiji kama hili!?


Tusiwe wanafiki na tuache kuvaa miwani ya mbao...
 
Back
Top Bottom