Umewahi kusikia nini kuhusu madereva wa malori?

Mchochezi

JF-Expert Member
Feb 29, 2012
10,416
6,578
Mimi niliwahi kusikia madereva wa malori wanaoenda nchi jirani kuna muda wanasahau kama wapo safarini, kutokana na changamoto mbalimbali za njiani kama mipakani nk

Naskia wamatembea na majiko yao kabisa pia wakiwa na unga, vitunguu, mboga, nyanya yaani wakifika mahali wanashuka wanakaa wanapika ili wale waendelee na safari, hakuna kwenda hotelini.

Wewe uliwahi kusikia nini kuhusu hawa jamaa?
IMG_9667.jpeg
 
Sasa ajabu nini?Kifupi Lori ni geto ndomaana likawekewa kitanda na kabati..Kwenye Scania kuna kabati la vyombo,Nguo,Chakula,Friji ndogo..Vitanda viwili..Benzi Axior ndo wanazingua wanaweka kitanda kimoya kama una Tingo utakubali mzik..

Kupika ni mara moja au mbili mchana na Usiku kuepusha garama za matumizi ya pesa..Mfano wanaoenda Burundi/DRC ukifika Kabanga mnasubirishwa Siku 2-3 hata nne hasa magari yanayobeba mizigo..Magari ya Mafuta ni chap tu

Tabia pekee wanayofanana madereva ni Umalaya..Inakua Tabu kwasababu kila sehemu watakayopark Malaya wanajaa utafikiri kuna mnada wa Nguo..Nilienda na Jamaa Congo,Burundi kabla hata hatujavuka boda huko Kibanga ukifika kabla ujashuka unakuta Malaya wanagombania kukufungulia mlango sio Tingo wala Dereva na Bei elekezi ni ya kizalendo kabisaa..Kwahiyo madereva huwaingiza ndani ya gari na kucheza michezo michafu kisha anahamia gari lingine..kwahiyo hii nayo ni changamoto ukifikiria madereva wengi sana wameoa na ni kuanzia 35+ ila bado wanaendekeza umalaya

Changamoto nyingine ni Uvamizi hasa Sudan ya chini ambapo kuna kipindi wanakamata dereva unachapwa fimbo za kutosha na mda mwingine kuuwawa ukiwa mbishi..

TZ hii wanao ongoza kwa gari ni MO DEWJI anagari zaidi ya 600+ na madereva 1000+ mwenye Lake oil gari kama uchafu,GSM utajiri kaupatia huko..na yule mchaga
 
1. Pindi dereva anavyoludi kuchukua mzigo mwingine kiwandani au store huwa anaweza kuchukua mzigo wowote ule njiani na kuusogeza kituo ambacho abiria anataka lkn bei huwa ni makubaliano pia huwa chini kuliko kutumia bus lakini usiwe na haraka tuu maana wanamsemo wao "No hurry in Africa we have a lot of time"

2 huwa ni wepesi sana kuongelea maisha yao ivyo kwa muda mfupi anaweza kukuambia kuhusu vitu vyote alavyo Fanya kwenye maisha yake aijalishi mnajuana au amjuanai

3. Wanapata pesa nyingi njiani lkn robo ya pesa huishia kwa traffic pia robo tatu kwenye familia au mchepuko

4. Wanathamini kununua viwanja na kujenga kuliko kufanya biashara maana muda mwingi wanatumia barabarani ivyo ni vigumu kuwekeza kwenye biashara maana ufwatiliaji unakuwa mgumu

5 asilimia kubwa ya wake zao huwa ni Mama wa nyumbani au wanauza maduka karibia na nyumbani

6. Huwa wanatabia ya kumwambia utingo wake alale kwenye gari yeye anaenda kulala lodge

7. Kama amenunua Kuku, Mbuzi, Mchele na Mkaa basi jua Mkaa ndio utakao enda nyumbani ivyo vingine vitaishia kwa mchepuko
 
Back
Top Bottom