Umewahi kupata mkasa gani barabarani?

Mwaka 2001 nilikuwa ndani ya Hice "public transport" ikiwa natokea Wilayani Kahama naelekea Kakola. Tulipo fika kijiji cha Lunguya, gari nilivyo panda ikiwa imesimama barabarani ikishusha abiria, nikishuhudia Mvua kubwa ikinyesha upande mmoja wa barabara na upande mwingine ikiwa hainyeshi na ardhi ni kavu kabisa.....
Hili jambo lilinishangaza sana hakika
Ukadhani ni uchawi au
 
Ukadhani ni uchawi au
Usinilishe maneno tafadhali.
Mimi nimesema kwamba nilishangaa na niliona ni kitendo cha ajabu sana katika maisha yangu, na hiyo ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kuona kitu ya aina hiyo
 
Nashangaa mtu anayegombana na askari, huwa wananikamata na wananiachia wenyewe sijawahi kuandikiwa fine.......kuna aina fulani ya utambulisho tu nikiwaambia wao wenyewe wanakuomba namba!! Yani wao ndio wana apologize na unapewa heshima kibao.

Siku moja natoka Bagamoyo, kuna ehemu kuna mteremko mzuri sana halafu ndio pale kuna mji sijui panaitwaje, kuna Satellite City pale, basi jamaa nimeshuka kwenye ile down niko na Primera Nissan, ghafla jamaa kanipoiga mkono, nikaweka kando, sikutaka kesi, nikaweka buku tano maana nilikua nawahi mjini. Kuja nikamuomba radhi nikamuonyesh abuku tano kimtindo ili achukue, akagoma akaniambia nishuke, nikashuka akanipeleka kwenye kundi la askari wenzie kama sita hivi.

Kufika pale nikawasalimia kwa uchangamfu sana sana lama nimepata kinywaji kidogo, jama wakasshangaa sana, basi nikajitambulisha kwa ule utambuloisho wangui aaaaghh kila mtu akaanza kufurahi, tukabadilishana namba na aakri wawili nikapanda zangu gari nikaondoka. Yule mjinga akawa amekosa buku tano hivi hivi kwa tamaa zake, alivyoona nimetoa buku tano akajua aknipeleka kwao nitatoa nyingi zaidi
 
Hebu nidokezee na mm na mm huo utambulisho mzee mwenzangu.
 
Salaam
Vyombo vya usafiri tunavitumia kutusaidia kutoka sehemu A kwenda B hivyo ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku, lakini pia vyombo hivi vinahitaji umakini wa hali ya juu sana uwapo barabarani kwani kosa moja linaweza kupelekea umauti, kilema, uharibifu au hata kupata kesi.

Pia muda mwengine unaweza kujitahidi kuwa makini sana katika uendeshaji wako lakini akatokea mtu tu akakosa umakini na kukusababishia matatizo, lakini pia yapo matatizo ya kiufundi yanaweza yakajitokeza na kusababisha ajali na dhahama.

Wapo wanaotukanwa au kutukanwa barabarani, wapo wanaopigana kisa uzembe wa barabarani, wapo waliopigwa risasi au kutishiwa kisa makosa ya ki uendeshaji na pia wapo wanaojikuta safari yao inakuwa chungu kutokana na jambo linalowakuta barabarani.

Uzi huu ni maalum kwa mikasa ya barabarani na kama limekukuta tueleze iwe kama somo kwa wengine, si lazima uwe na gari inaweza kuwa pikipiki, bajaji, na hata kama wewe ni abiria pia share yaliyo kukuta. View attachment 1262811
Dah nakumbuka mwaka Jana nlikua natoka kwenye show mmoja iv ya mziki ikiwa usiku kama saa8 iv nikiwa pembezon mwa barabara natembea sina hili wala lile gafra nikasikia pikipik ikitoka kwa nyuma kwa speed ikabidi nizid sogea kando ya barabara gafra nikapigwa bongeee la Kofi pasipo kujua nimepigwaje dah ilibid nikae chin kidogo sito sahau
 
Barabarani kuna visa vingi mno ambayo driver yoyote yule ama kwa kuwa makini au kutokuwa makini hukutana navyo. Itoshe kusema kwamba vingi humuimarisha driver with time.
Jana tu nilikutana na kisanga...nikaona fresh!
 
alikwambiaje mkuu?
16/09/2016 tukiwa miongoni mwa abiria Mimi na mchumba wangu kwny basi la newforce kutoka DSM kuelekea songea,majira ya saa mbili usiku maeneo ya kifanya njombe basi lilipinduka na kutamatisha maisha ya mchumba wangu, sitakuja kusahau maneno ya mwisho mchumba wangu aliyonitamkia muda mfupi kabla hajakata roho,inauma sana
 
2012, mbezi jogoo nimetoka kula bata saa 10 usiku hiyo nilisinzia bana bana asikuambie mtu siku yako kama haijafika haijafika, sijui kilichonitoa usingizini mbele kama mita 20 dala dala likawa linaingia barabarani lipo katikati afu gari iko speed nilishika breki gari inaserereka kama bahati daladala likawa limesogea nikaikwangua kidogo, mara nnaona lori la mchanga limeharibika kwa mbele hapo bado gari inaserereka na breki, ilibaki kama meter moja kuligonga lori gari ikasimama, aisee sitaisahai iyo siku, cha ajabu baada ya kutok hapo nikawa nnaendelea kusinzia...usinywe sana kisha ukaendesha gari hasa mida ya alfajiri ni bora upaki hapo bar ulipo lock milango ulale
 
Mimi niliwahi kusimamishwa na wana usalama nikakaidi mara ghafla nikaona mkonga inaingizwa road kunifukuzia, nilinyoosha goti na mtanange ulichukua takribani dakika 45 nikawaacha mbali sana ila walifanya mawasiliano nikafungiwa njia na gari kama nne hivi za jeshi la Polisi kutoka mji mwingine na hapo mambo yakafikia tamati.
Ulipoona umewaacha ulitakiwa utafuta kichochoro utulie mzee uondoke baaaade
 
16/09/2016 tukiwa miongoni mwa abiria Mimi na mchumba wangu kwny basi la newforce kutoka DSM kuelekea songea,majira ya saa mbili usiku maeneo ya kifanya njombe basi lilipinduka na kutamatisha maisha ya mchumba wangu, sitakuja kusahau maneno ya mwisho mchumba wangu aliyonitamkia muda mfupi kabla hajakata roho,inauma sana
Pole sana ndugu,barabara ya njombe to songea ni full milima na miteremko mikali,
 
Mi kuna siku niliendesha kinoma..sijui nilikulala nini tumbo lilikuwa linaunguruma balaa...ndo ilikuwa mara ya kwanza kupatwa na tumbo la kuendesha barabarani...
 
Ulipoona umewaacha ulitakiwa utafuta kichochoro utulie mzee uondoke baaaade
Njia ilikuwa ngeni kwangu lakini pia niliingia chochoro na nikapaki ndani ndani huko kwa kudhani wao hataniona, dakika kadhaa naona mkonga huu hapa nikaamsha tena nikaona nikiingia ndani sana kusipokuwa na watu wakinidaka itakuwa soo kabisa bora nirudi road kwenye watu.
 
2016 nilitoka kununua pikipiki kkoo nikiwa na dereva wangu tukasimamishwa kwa kuwa hatuna kibali cha kuingia mjini japo pikipiki Mpya ndio imetoka dukan
 
Back
Top Bottom