Umewahi kupata mkasa gani barabarani?

Aisee kidogo niwemo kwenye safari hiyo ghafla usiku nikahairisha safari kwenda Songea baada ya ajali walinipigia watu wa karibu walihisi nimesafiri pole sana mwamba
 
Kawaida sana, hizi mvuaza juzitu hapa airport ilinyesha mvua kubwa sana terminal 2 mbaka nusu ya covered walkway, na terminal 3 palikuwa pakavu kabisa.
 
Nilitoka boda horohoro sa 11 jioni na gari haina namba kuja bongo ila full dokomaa, nilipofika segera nikachukua cartoon ya castle ili nizugie na pakt ya embassy nikafungua moja nikainywa nikaitupa ili nivuke kabuku rd block. Askari pale akanikagua mwisho akaona laga siti ya nyuma akauliza za nani nikamwambia za kwangu ili nitakapochoka nizinywe nilale akasema nazikabidhi ktuoni Sikh nikipita siendeshi nizipitie akabeba na embassy 10. Iliniuma sana
 
Mimi mkasa wangu ni watofauti kidogo. Huwa napenda sana kusafiri usiku nikiwa naendesha gari mwenyewe. Nakumbuka mwaka jana around April nilikuwa natoka kigoma naenda Geita. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kuendesha hiyo njia kwa hiyo nikatumia msaada wa Google Map.

Safari ilianza saa mbili usiku, saa tatu na nusu nilikuwa kasulu, saa sita kasoro nilikuwa Kibondo. Hapo nikashuka nikanunua Redbull, nikanywa saa saba kamili nikaamsha. Sasa ukiwa unatoka kibondo unaitafuta Kakonko, kuna sharp corner moja ambayo kama sio mzoefu au unapita usiku ni vigumu kuiona. Na bahati mbaya hapo network ipo chini.

Sikuiona hiyo corner, nikanyoosha. Network inakamata nilikuwa kama km 60 hivi niingie Burundi. Nikaona isiwe kesi nikageuza gari nikarudi nikaipata ile corner safari ikaendelea.

Ubaya wa Google map kwa wakati ule walikuwa hawaja update barabara hii mpya inayounga Kakonko na Kibondo, so walikuwa na ile ya zamani ambayo ilikuwa haitumiki. Bwana wee nikapita hiyo njia, Mungu saidia nikatoboa nikaipata njia mpya mwendo.. nikapita Kakonko vema mpaka Nyakanazi.

Sasa ukiwa Nyakanazi, Google Map inaonesha njia ya kufika Geita ni kupitia Biharumo, wakati kiuhalisia kuna hii ya Runzewe (Hii nilipita wakati narudi).

Hiyo safari ilikuwa ndefu sana , ilinifurahisha maana nilijifunza na maeneo mengi. Gari niliyokuwa natumia ilikuwa Land cruiser Prado, na mimi sio mkimbiaji sana. So safari hiyo ya Biharamuro, nikazunguka nikaingia Geita Saa nne Asubuhi.

Tired but excited
 
Daaahh pole sana yaani MTU uko Nyakanazi halafu unaenda Biharamulo kwanza then unarudi Bwanga then Katoro haaaaa Daaaa pole sana.
 
Nakumbuka mwaka 2009 niliiba pikipiki ya mzee ,ilikuwa Yamaha DT ndo kwanza Mpya kabisa,nikaenda kupiga nayo misele ,mida ya kurudi nikakanyanga gunzi la mahindi kwenye tail la nyuma,daa nilijikuta nipo mtaroni hafu pikipiki imenigandamiza miguun huku ikiunguruma,sikuumia sana wala pikipiki haukuharibika hata kidogo ila tangia siku ile mpaka Leo sjawahi kuendesha tena pikipiki ,naiogopa balaa
 
Leo hii nilikuwa nakimbilia mahala..
Sijui ilikuwaje nashitukia nipo chini ..mwenye boda boda naye kashangaa ilikuwaje..maana ...hakukuwa na cha kufanya tuanguke!
 
Leo hii nilikuwa nakimbilia mahala..
Sijui ilikuwaje nashitukia nipo chini ..mwenye boda boda naye kashangaa ilikuwaje..maana ...hakukuwa na cha kufanya tuanguke!
Dah! Pole sana ndiyo mambo ya barabarani hayo.
 
Mpaka leo chombo unaiona nuksi!
 
Mimi nilikoswa na semi nilikuwa naendesha bajaji Natoka stendi kuingia barabara kuu ya lami nikasimama kucheki kushoto na kulia kuangalia usalama niingie lami mzee kushoto kwangu nikaona gari kwa mbali sana inawaka mataa nikajiaminisha ni basi liko mbali kwa hiyo nikaingia lami,ile nakanyaga lami tu kama sekundi tu semi likafunga breki kali sana nyuma ya bajaji hadi tela likapinda likaziba barabara.

Ili kukwepa kunigonga basi mapigo yangu ya moyo yalienda kwa kasi sana kwa kukosa kugongwa na lori nilichanganyikiwa nikawa sijielewi kabisa kama ni mimi, sasa dreva wa semi akaanza kunitukana sana mimi nikawa namuomba msamaha tu maana nilikuwa na kiwewe cha kufa mtu,huku tena abiria nilikuwa nimembeba akawa ananitupia lawama eti nataka kumuua familia yake itabaki na nani.dreva wa semi alikuwa kafungulia mafuta mpak mwisho ilikuwa mida ya saa mbili usiku muda ambao malori yanakuwa mengi barabara ya dar-mwanza hili tukio limeacha kumbukumbu miongoni mwa masaibu niliopitia ilikuwa natoka stendi mpya naelekea mjini Nzega Tabora.
 
Kuna sehem moja inaitwa Mto Koga kama unatoka Tabora kwa gari unakwenda MPANDA....

Hio sehem ina Mbu sijawahi ona maishani mwangu, tulifika hapo saa nne usiku hivi, tukalala ndani ya Gari,
Asubuhi tunaamka Tyre Zote zina Pancha hazina Upepo.

Mbu wamenga'atanga'ta Tyre zote zimetoboka.
 
😂😂😂😂😂😂walikukomaa
 
Pole sana,
 
Kwenye mguu nina kovu la pkpk xl, nilikunywa pombe nikawa narud zangu home, mvua ilikua imetoka kunyesha dah sijui ilikuaje nkajikuta mguu mmoja joto limezid kuinua pkpk siwezi wee,
Lakini sahiz mm ni mshindi aliye fanikiwa kuacha pombe kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…