Boss la DP World
JF-Expert Member
- Dec 12, 2021
- 1,997
- 7,551
Serikali imesema hivi karibuni itaruhusu mabasi kusafiri kwa saa 24, ni jambo jema sana endapo jambo hili muhimu litafanyiwa kazi.
Jambo lenyewe ni kufunga taa kwenye barabara kuu zote, fungeni taa zinazotumia solar panels ili kuongeza mwanga barabarani, kwa wanao endesha usiku watakubaliana namimi kuwa mwanga wa taa za gari pekee hautoshi kuonesha kila kitu barabarani hasa kipindi cha kupishana.
Nadhani wapo watakaohofia wizi wa taa, well zipo taa ambazo zina camera zenye uwezo wa kudetect mpaka alama za macho, napendekeza zifungwe hizo pia wakuu wa wilaya waambiwe kuwa ikitokea taa hata 1 imeibiwa kwenye eneo lako basi kibarua chako kimeota nyasi na utakatwa mafao yako kufidia.
Nadhani vyombo vya ulinzi vitaongeza umakini kulinda miundombinu hiyo badala ya kukimbizana na wanasiasa huko Ngorongoro. Hii nchi ni tajiri, msiue raia wenu kisa taa za barabarani. Anzeni na barabara ya Dar-Dodoma kisha barabara nyingine za kuunga mikoa yote.