Umesoma shule ya bweni wewe?

Umesoma shule ya bweni wewe?

Nakumbula Moringe Sokoine enzi hizo dah, kila wikendi ni wali au beche, na kuna shule ya endalofta karatu nakunbuka tulikuwa tunatembea na vijiko mifukoni kama kalamu,
 
Daaah! Menikumbusha mbali sana, enzi hizo nipo Galanos boys! Kuna sehem moja hiv tulikuwa tunapenda sana kulia, tukapa name "THE GROUND OF CHALLENGE" coz baada ya kupiga hiyo kitu tulikuwa tuna-challengiana sana!
Mbaya zaid kwenye hilo harage kitu "kerosine" ilikuwa haikosekani, ikifika siku ya kande utafkir hizo kande zimepikiwa Mount Meru Petrol Station zinavyonukia hilo futa!
 
Kibiti boys high school lilikua linaitwa. Dongo

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
dha!!nakimiss kweli.....dona haragwe.....maisha ya bodingii bana...mara oooh utasikia carolina ana mimba
 
sengerema sec iliitwa bondo pia, kama una 100 unanunua kijiko kimoja cha dagaa au mchicha kwa bibi ( yule ndugu yake na nesi wa shule) basi unamaliza share 2 za bondo......
 
Duuu.....nyali(wali)....bondo(ugali)pola(uji) shybush chini ya mkuu Mbanga..siku ya mechi unatorokea mgodini ku refresh...daaaa.....mkuu ume rewind memory yangu mbali saaaana aisee
 
Weekend munatorokea beach, wenyewe tukiita cost pale Shangani
Mtwara
 
ukiirudia hiyo kitu milambo tabora tulikuwa tunasema second selection au paper two
 
Mara secondary kulikuwa na watoto tunawaita busima dar umenikumbusha mbali sana na badae mazengo dodoma kulikuwa na raha yake sana.

Busima wengi walitokea sehemu za nyamatare, kibini na ile mitaa karibu na kambi ya jwtz ya zamani maeneo ya sda church, ama kweli tumetoka mbali sana.
 
mkuu nimekumbuka mbal sana iringa dabaga pomerini high school,tulikua tunapkiwa maharage mix kabich,al maarufu sotojo ilikua raha sana miaka hyo.
 
nilijiapiza sitakula makande tena, remembering junio seminari, mrgr
 
very tru

Kuna rafiki yangu Mbelgiji aliwahi kuniambia kitu nikacheka nusura nife kwa kupaliwa mate 'ukisoma shule ya bweni Tanzania basi una uwezo wa kukaa jela yeyote ulaya' na kisa cha kusema hivyo ni yale aliyoyaona tulipoenda kumtembelea mdogo wangu Forest Hill Sec
 
Hii ni nguna bhana, kwa wale tuliosoma ndanda sec, ongeza hapo na mbaadhi kitu kama mazega ya nyuki. Kwetu siku ya nguna na harage, basi ilikuwa ni furaha tupu:doh:
 
Dah wapi jamaa zangu tuliosoma wote pale masaselo sec school? Hiyo ukipenda unaiita' nsima'.
 
Musoma Tech/Alliance enzi hizo! Dishi la maharage na ugali yakitolewa mwenye kubeba la harage anakimbilia South mwenye la ugali anakimbilia North sasa either upate ugali au harage. Harage zenyewe sasa! Ktk harage 1 kuna wadudu kama 6 hivi! Ugali unga kama umeoza hivi,
siku ya wali masomo mwisho saa sita, mapema watu wanatoka kwenda kuuvutia pumzi. Kichekesho ni pale utakapo pata huo wali, kwanza ni kama ngumi ya mtoto, ration master, kiranja wa bwalo na wapishi wanaiba zaidi ya nusu ya ration then wanaongeza mchanga. Nusu wali nusu mchanga. Siku ya wali inageuka kua kwaresma.
Ukipata kijitamvua cha samaki unaficha plate 2.
'Maisha ya boarding noma, utafikiri kambi ya mafunzo' Jmo
 
nyie watoto mumesoma shule kwa taabu sana. Mimi nimesoma shule moja sitaki kuitaja kwani mtanifahamu bure, tulikuwa tunaoshewa vyombo vya vyakula na kila jumamosi tunapata karanga na kuita atoms. usiku kila siku nyama na wali halafu kila jumamosi sabuni ya kufulia na kuogea inaitwa carbolic basi hiyo carbolic ukienda bafuni inachubua kweli.
 
Back
Top Bottom