Umeshawahi kutekwa? Ladies be very careful

Umeshawahi kutekwa? Ladies be very careful

Umenusurika this lesson ni tahadhari kubwa kwa jamii kuwa maadili na haki ya URAIANI unatoweka polepole na Ukatili, uhuni ndiyo unachukuwa nafasi na kuingia mitaani na maishani mwetu...Naomba tuwe HADHARI na tuwe ALERT all time.!! Nakusikitikia na kuhuzunika kwa yalotokea kwako nakwa wengine hata wasiyosema au kuyaleta jamvini wapo wngi wameonewa! Poleni sana Mungu atakuwa nayinyi na watu wema. amin
 
aaaah wapi, siwezii kuwa na swali lingine, nimekosa cha kufanya? we kula zako hamsini katafute ugali wako na familia yako tu, kila mtu anajua maisha yake anaishije, punguza hasira wala sina muda wa kufuatilia maisha yako mimi. i was just expressing my opinions!
Ndugu yangu usingeuliza swali wala mimi pia nisingekuwa na muda wa kukujibu. Nilitaka nirekebishe mtazamo wako na wengine kama wewe kuhusu kwenda na wakati uliopo.

Kuna wengine walikuwa na fikra kama zako wakati simu zinaanza kuingia nchini, unakuta mtu anasema niache kununua kiwanja nikanunue simu? Leo hii nafasi za kazi, nafasi za chuo, taarifa za habari( local and international), miamala ya kifedha yote unapata kupitia simu.

Ukimcheka mchimba mfereji wa maji kwa gharama kubwa ili maji yatiririkie shambani kwake wakati wewe unatumia gharama kama hizo kujengea nyumba, kumbuka mwenzio akishaseti mfereji hela ikaanza kuingia bila kikomo, nyumba zitajengwa na mashamba mengine yatafunguliwa wakati wewe bado una nyumba yako moja.

Uko sahihi kusema kila mtu na maisha yake lakini kama una mtazamo hasi ukirekebishwa na wenzako waliopitia huko huko na kufanikiwa japo kidogo ni vyema ukawasikiliza. Kama kuna mtu ananunua gari halafu muda mwingi gari linapaki baa halafu hana hata kibanda basi gari hilo ni la starehe.

Tumia hela upate hela zaidi . Tchao
 
aisee. pole sana kwa mkasa huo na asante kwa maonyo hayo ..
mwenye ufahamu na abebe
 
Ha ha ha ha me nilikuwa mpenzi sana wa lift lkn tangu lile vuguvugu la kuuliwa sana wanawake
ndo ilikuwa fundisho kwangu na mwisho wa kupanda lift heri nitembee kwa mguu kuliko

Pole mwaya,hizi lift hizi zitakuja kutuua mie siku hizi

nasimamaga kituoni hadi nahis miguu kuingia ndani,ila its better that way
 
Habari wana MMU.

Ningependa kushare na nyinyi what I experienced ili kwa namna moja au nyingine niwasaidie wanajamvi wenzangu ili siku moja wasijepatwa na such majanga au zaidi ya haya.

Ilikuwa tarehe 4/6/2013, nikiwa nimetoka zangu kazini nikisubiri a friend of mine ambae huwa nakuja nae town (by that time alikuwa maeneo ya Moroko) nikaamua kwenda pale church (St. Joseph for prayers). Kabla sijaingia getini, upande wa pili nikasikia mtu akiniita jina langu, akiwa kasimama pembeni ya gari. Bila kufikiria mara tatu tatu nikajua ni mtu anayenifahamu. Nikavuka upande wa pili na kumkuta uyo mtu ila kiukweli sio mtu niliyemzoea hadi kunijua jina ila yes nilishakuja nae several times to town with other people.

Akanisalimia na kuniambia kuwa several times amekuwa akija na mimi town (ni kweli mara nyingi huwa napanda taxi au private cars mida ya asubuhi kuja town) na kwa wakazi wengi wa mjini Daslam thats very common maeneo ya tabata, mbagala, mtongani, mivinje e.t.c. Akaniambia wanamsubiri rafiki yao then wanaenda where I was going (Kijichi) so tuondoke wote and I would pay TSh 2000. Nikampigia uyo rafiki yangu akaniambia kuna foleni kubwa na atachelewa. Kwa kuona kwamba its late nikaona niondoke nao as long as wanaelekea where I was going.

Niliwasikia wakimpigia uyo rafiki yao ila wakasema hapokei so tuondoke. Basi mi nilikaa back seat na gari yao ni vitz ya mlango1. Mbele walikuwa 2 na mimi nyuma. Basi safari ikaanza ila moyoni sikuhisi amani kabisa!!Nikawa natafta nione plate number za gari kwenye kioo nikagundua kuwa haikuwepo na vioo vilikuwa tinted!Kiukweli hofu iliniingia sana. Mara moja nikachukua my bible and prayer books nikapiga sala pale (im sure they saw me praying). Wakati tunaondoka walipromise kuchukua abiria wengine kituo cha stesheni so nikajua tutakuwa wengi.

The guys were very quiet, yaani kama hawana midomo! Wakati tukiwa kwenye foleni mdogo wangu akanipigia simu, tukawa tunaongea about school fees za shule fulani hivi. Ile namaliza kuongea tumeshafika lapa Dawasco. Nikawauliza mbona hamjapakia abiria wengine? Wakadi usiku umeingia afu wanaogopa foleni. Hofu ikazidi sana ila nikajipa moyo kuwa Mungu atanilinda.

Tulipofika njiapanda ya Kilwa road, wakaingia barabara ya shimo la udongo kule Bandari na nilipowauliza wakadai wanakwepa foleni. Hapo sasa hofu ndo ilizidi sana. Nikapata wazo la kupiga simu home ila before that jamaa alokuwa uoande wa pili akanipokonya simu kisha wakafunga vioo na jamaa akanirukia uku nyuma nilipokuwa nimekaa. Alinikaba sana shingo mana nilikuwa nashindana nae, lengo ilikuwa ni kujaribu kumkamata sehemu fulani ili akose nguvu aniachie! Waapi!Kwani hata sehemu hizo nilifanikiwa kuzigus? Nahisi jamaa labda hana! Alinipa ngumi moja huku kanikaba na akapromise kuitoa roho yangu iwapo sitofanya fujo. Sikuwa na ujanja zaidi ya kutulia na ku surrender! Jamaa akaniambia wao wanataka hela na vitu vyote vya thamani nilivyokuwa navyo.

I had earrings and the chain (hazikuwa original) basi jamaa walivyo wajinga wakaona deal! Wakauliza thamani yake nikawaambia zote thamani yake ni laki 5!Wakajua bonge la deal! Alokuwa ana drive akaanza kumpigia mtu anamwambia anamletea mzigo (nikajua kabisaa mzigo ni mie, yaani natolewa kafara au ndo nabakwa kiroho mbaya). Sio siri nililia sana, nikawasihi waniachie nitawapa hata pesa kama wanataka mana account yangu benk ilikuwa inapumua kiasi chake! Wakachukuakila nilichokuwa nacho, cash, handbag, bank cards zangu zote yaani waliniacha sina ata kumi. Wakati huo jamaa kanishika shingo mikono yote miwili ili nisifurukute.

Akaniambia dada tumeshachukua chetu sa ivi tuntafta sehemu ya kukuacha na tukikushusha usigeuke nyuma mana tutakumaliza. Hapo mimi nikawa naomba Mungu waniache tu salama na kweli kufika sehemu wakasimamisha gari, mkabaji wangu akaniachia wakafungua mlango wakaanisukuma ila sikuambua chini. kweli sikugeuka nyuma nikaanza kukimbia kutafta msaada. Kichwani mwangu nilijua wamenipeleka mbali sana, ajabu nauliza watu pale wapi wananimbia maeneo ya Kanisa Katoliki Kurasini!!

Nilipiga magoti na kumshukuru Mungu, wasamaria wakanisaidia kutafta bodaboda, nikafika home na kwa vile I had money home basi nikamlipa bodaboda. Thats what happened to me, ni story ndefu ila napenda especially wadada wajifunze haya.
  • Ni heri ukabanane kwenye daladala hata kama una pesa ya kupanda taxi kuliko ku risk maisha yako kuchukua taxi au private cars.
  • Kama mtu humfahamu, hata kama atajifanya kumjua hadi baba yako, please do not trust them
  • Ikitokea unalazimika kupanda a private car au taxi make sure uko na watu mnaofahamiana not strangers especially men, uwiiii!!
  • Jenga utamaduni wa kunote plate numbers za gari lolote unalopanda iwe taxi au gari binafsi na ikibidi mtaarifu mtu/watu wa karibu ili in case of anything unaweza kupata msaada.
  • Epuka sana kutoka job night hours kwa kisingizio cha kukwepa foleni na usumbufu wa magari. Ni heri usafiri mchana its safe than usiku.
  • Dont entertain your employer aisee, mimi hili lilinitokea kwa sababu ya mwajiri wangu mana kulikuwa na kazi zilizonilazimu kuzifanya on that day! Fanya kazi kwa muda mliokubaliana kwenye contract tu na hata kama unalipwa overtime my dear usiendekeze sana pesa kwani hizo zintaftika ila uhai ukipotea hautaftiki.
  • Tembea na silaha zetu za imani ama bible au msaafu mana kwa njia ya ajabu zaweza kukusaidia pale usipodhania wala kutegemea.
  • Tumkumbuke sana Muumba wetu na tumtegemee in our daily life. Unapotoka asubuhi kuja kazini pray to him and ask for his protection. Huu uwe utamaduni wako daily
  • Mhh, siku hizi kumuliki gari sio anasa, unaepusha kwa asilimia kubwa kupatwa na majanga kama haya. Baada ya kuumwa na nyoka sasa sioni kama kumiliki gari ni anasa, nimechukua hatua na wewe mwenzangu usiogope kuchukua hatua.
NOTE: Kuna watu walionilaumu na pia mtanilaumu kwamba I was stupid kwa kuchukua uamuzi wa kupanda hilo gari but kwangu mimi nafahamu kuwa everthing happens with reasons! Kwa namna moja au nyingine Mungu alitaka kunifundisha kitu mimi pamoja na wengine/wewe unaesoma huu uzi. Binadamu wengi siku hizi wamekuwa sio wema kabisa! Kuna tetesi kuwa wengine wanawateka watu na sio kwamba wanawapora ila wanawaua na kuwatoa kafara! Please be careful especially wadada mana sie ndo tupo kwenye risk coz we cant fight back.

pole sasa dada,mshukuru Mungu kwa kukuepusha na hilo.kulingana na story yako sioni hata kama kuna sehemu mtu anaweza kukulaumu ukizingatia kwa hapa dar kumiliki usafir sio anasa kwani kero yake hakuna mtu asiyeijua...no,wapo wasioijua manake nisijesema wote tunaijua coz wengine wakitaka kupita madaladala yetu yanawekwa kando kwa madakika kadhaa kama sio masaa kadhaa.nachoweza kusema ni jitahidi kuwa makini nxt tym.makosa yapo na lazima utayafanya tu but jitahidi yasiwe kama hili au yanayoshabihiana na hili.pole sana bidada,ningesikitika sana hadi kulia kama wangeuosha huo wali mweusi ili uwe mweupe
 
Kama uliniona enzi hizo 1999 sijapata usafiri nilifanikiwa kupata shamba eka mbili kwa bei rahisi sana kibamba mwisho sehemu moja inaitwa mpiji. Nauli ya taksi kwenda huko baada ya kushuka daladala kibamba mwisho mpaka huko ilikuwa shilingi elfu kumi kwenda tu elfu kumi kurudi nyingine na bado unaachwa ng'ambo ya mto unatakiwa uvuke utembee kwa mguu kama kilomita moja hivi.

Kuna wakati hela ilinipiga chenga kidogo hivyo sikufika huko kwa kama mwaka na nusu hivi. Kilichoniokoa ni simu ya jirani niliyoiandika kwenye mkataba wa mauzo ndiyo iliyotumika na mjumbe kunitaarifu kuwa kuna mtu anakimendea kiwanja chako njooo haraka.

Na wakati huo simu ilikuwa ni anasa kuwa nayo, je kama simu ilikuwa anasa lile shamba ningekuwa nalo leo, je kama ningekuwana usafiri hayo yote yangetokea?

Jibu ni hapana mkuu, tena ungekuwa mbali zaidi ya hapa kwani ungewaza hata kupanda nafaka au matunda na ungekuwa umepafaidi zaidi. Tuwaelemishe hawa ndugu zetu wanaofikiri gari ni anasa ili wajue gari ni tool kama jembe na shoka.
 
Jibu ni hapana mkuu, tena ungekuwa mbali zaidi ya hapa kwani ungewaza hata kupanda nafaka au matunda na ungekuwa umepafaidi zaidi. Tuwaelemishe hawa ndugu zetu wanaofikiri gari ni anasa ili wajue gari ni tool kama jembe na shoka.
Kabisa mkuu.
 
Habari za asubuhi? Umeamkaje? Ungenifuatilia toka mwanzo ungenielewa, lakini kwa kukusaidia tu uliyeingia sasa hivi ni kwamba nilianza na gari nikiwa na malengo yangu na hiyo gari ikanifanya nifike kweye dili zangu kwa wakati na likazaa nyumba ya maana Mbezi Beach na gari jingine la type yangu kwa wakati husika.

Kama huna malengo na gari utaishia kuwa na mawazo kama hayo, utapigwa vimemo kila siku na wakuu wako sababu ya uchelewaji mwisho na kazi ukose kisa unadunduliza umalizie kibanda kwanza.

Upo hapo? vinginevyo unakaribishwa kama una swali lingine.
Mkuu wengine wana mitazamo hasi juu ya ununuaji wa gari wanashindwa kuangalia gharama ya gari ni ndogo ukilinganisha na gharama ya kujenga hivyo kwa mahitaji ya haraka na umuhimu wa gari ni vema mtu akaanza kununua gari kwanza hasa kwa kuepuka haya yaliyojiri kwenye mada hii., haijalsihi utalipaki wapi hata kwa jirani au garage. Nakupa hongera mno kwa uamuzi uliochukua kipindi hicho.
 
Mkuu wengine wana mitazamo hasi juu ya ununuaji wa gari wanashindwa kuangalia gharama ya gari ni ndogo ukilinganisha na gharama ya kujenga hivyo kwa mahitaji ya haraka na umuhimu wa gari ni vema mtu akaanza kununua gari kwanza hasa kwa kuepuka haya yaliyojiri kwenye mada hii., haijalsihi utalipaki wapi hata kwa jirani au garage. Nakupa hongera mno kwa uamuzi uliochukua kipindi hicho.
Ahsante sana.
 
WALIMWEUSI,
Mshukuru SanaMungu kwa kukuponya na kukuokoa kutoka kwenye janga hilo

Maana wangeweza hata kuitoa Roho yako hao

Pole Sana
 
Last edited by a moderator:
Kwa maelezo haya ngoja nimpe pole tu

Lakini kwa kweli kanichanganya sana, siku hizi jinsia imepotea kabisa:smile-big:

Kongosho mbona we hadi leo mimi sijui jinsia yako? Walimweusi ni username yangu tu huku JF kama vile wewe unavyojiita Kongosho. Wapo ambao wametumia majina yanayoweza kuonesha jinsia zao ila wengine ndo kama mimi na wewe, hatueeweki jinai zetu. Sasa from today umeshanijua, I am a woman.
 
Sadaka ni muhimu. Vipi kwani mbona unasema mhh? wengi hawaamini wanadhani labda nilibakwa!Anyway hata msipoamini it isnt my business, my business ni kutoa sifa kwa Mungu wangu
Achana nao acha wafikirie watakavyo ili mradi wewe nia yako ilikua kutu-alert asante sana.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
pole sana hili swala la kutekwa maeneo ya posta limekuwa sugu kwa kweli....jamani noah zile za 2,000Posta-Mwenge muwe makini pia sio zote zina nia njema

Daah mie nshazipanda sana zile mwenge posta japo nami huwa naangalia sura zilizomo tena kuna siku nilishangaa prado inapiga mwenge [posta 2000 mmmh saa ingine mungu tu anatulinda.
 
vits ya mlango 1? Kuangalia plate namba ukiwa ndani ya gari, how? Walimweusi ni binti?

Anyway, sijui nisemeje kwa sasa.

mbona wewe ulivyojifungia ndani ya gari lako baada ya kusahau ufunguo kwenye kitasa cha nje ulitupigia simu tuje tukufungulie? I m just joking.
Ana bahati watekaji hawakutamani kula wali mweusi.

Pole kwa kutekwa walimweusi
 
Sadaka ni muhimu. Vipi kwani mbona unasema mhh? wengi hawaamini wanadhani labda nilibakwa!Anyway hata msipoamini it isnt my business, my business ni kutoa sifa kwa Mungu wangu
mi sjasema skuamini WALIMWEUSI.. Mtukuze Muumba wako
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom