Umeshawahi kukutana na balaa la nyoka?

Umeshawahi kukutana na balaa la nyoka?

Urambo,tabora!!koboko msikie tu,ni kiburi,mbabe na mshenzi haswa! Kuna jamaa alimpga na jiwe ikawa kosa kupita ile njia!alikua anagonga kila kinachopita hadi raia tukabadili njia,ilibid wamwue kwa gobole la magololi maana alikua tishio! pia niliwa kutana na koboko huko huko urambo ghafula aloo nilisali sala zote maana alisimama na kutoa kunitazama my next act ili ajibu,uzur nilitulia mwisho akasepa zake!almost Tabora yote koboko wapo na hawana noma na mtu ila ukimchokoza umekwenda na maji!

Tabora nyoka ni wengi kulko raia sababu ya mapori
 
Muongo sana eti nyoka wote, wakati hata usiku huu kuna nyoka utamchezea😂😂
😂😂😂😂 Laiti ungejua sina namna ya kumpata huyo nyoka, tatizo baridi la kwenu ni kali mwee nawaza July itakuwaje itabidi nikimbie aisee
 
Naogopa sana na sijawahi ona kwa macho. Mwaka huu mtoto wangu ilikuwaa usiku tupo nje yeye alisimama kwenye majani ghafla akaja analia amegongwa na nyoka mimi sikumwona ila yeye anasema kamuona wa black ( mweusi). Nilikuwa na jirani yangu akamwangalia akasema huyo sio nyoka atakuwa mdudu tuu wa kawaida mimi sijui kitu.

Tumekaa ndani kama dk 5 hivi mguu ukaanza kuvimba, bahati kuna bodaboda niliagiza msosi akawa analeta akashangaa leo mbona anko mpole sio kawaida yake nikamwambia kuna mdudu kamng'ata anavimba mguu kuja kumwangalia nusu aninase vibao aisee.

Akamfunga mguu kumbeba mbio mpaka kwa huyo mzee anamjua ndio kumpa dawa ya kunywa na nyingine akampaka na kusugulia mguu wote. Akaendelea na dawa hizo siku hadi ilipoisha Yule boda boda alinambia kama nisingekuja kwa dk 10 mbele ulikuwa unamkosa mtoto huyu. Yaani sikulala karibia wiki kwa woga.

Kama unaogopa kaa kimya unachafua uzi kwa udangaji wako
 
Cobra sio koboko, ni aina mbili za nyoka tofauti. Cobra nimeshuhudia Mwaka huu mwezi January tulimuua baada ya kuingia kwenye zone yake pasipo kujiua akatuletea utata tukapambana naye.

Cobra anajitanua shingo yake hasa anapokuwa ameudhika.

Koboko (Black/Green mamba) sijawahi kumuona kwa macho yangu ila nimehadithiwa na nimemsikia hasa nyakati za usiku akiwa anawika
umechanganya kidogo ndugu... yule anayewika ni mwingine kabisa (kiswahili halisi sijui ila kikwetu tunamuita ntuanyika). koboko yeye ni mrefu, mgongoni kama amesukwa na jina lake ni black mamba hata awe wa kijani au rangi nyingine yoyote
 
taja vingine vyote ila kiumbe nyoka! hapana kwakweli yaani namuogopa, namuona kinyaa na simpendi kiujumla
 
Kama unaogopa kaa kimya unachafua uzi kwa udangaji wako
Umekurupuka kama jina lako mkuu. Sijadanganya ni kweli ilitokea january hii. Tena ni Dar mbezi mwisho huko kuna nyoka wengi sana nina bahati tuu sikuwahi kuona kwa macho ila wenyeji wanakutana nao kila siku na wamezoea.
Sasa nidanganye ili nifaidike nini??
20230121_112252.jpg
 
Stress zipo tuchukue hatua,, nyuzi za leo ni ukimwi na nyoka ujikute vyote vimekujeruhi kila anaecheka anakuwa mbaya
Hahahaa yaani leo nyuzi trending ni hizi, Ukimwi na nyoka hata mimi nazunguka humo humo toka mchana.
 
Chatu alitaka kunimeza.Lakini kwa vile hii hadithi nimeisimulia mara kadhaa Facebook na wapi,sitaki kuwaboa watu.
Lakini huyu chatu nilikuwa sijui kama ni chatu. Nilidhani ni oversized cobra.
We unasema cobra alikuhurumia. Hayo ndiyo mawazo yangu pia. Nilifanikiwa kumtoroka yule chatu,au alinihurumia?
Siku hiyo chatu alipomitokea ni siku ambayo Kagame alikuja Dar kumuona Kikwete,siku hiyo hiyo.
Pole Sana mkuu.
 
Mbezi beach moja hii. Hata ukiambiwa Bongo kuna vinyonga utabisha.
Watoto wa kishua hao,nyoka wanawaona kwenye channel ya Nat Geo wild.

Hao hata jongoo akiingia ndani wanakimbia nyumba wanaenda kulala kwa jirani.
 
Nilikuwa naishi maeneo ya changanyikeni, karibu na kikosi Cha jeshi, Sasa jirani na kwangu kulikuwa na mti.
Yaaani kila siku mchana Kuna joka lefuuu la kijivu ni refu sana linaotea jua kwenye huo mti na likichoka linashuka linaingia shimoni kwenye mshimo!
Cha ajabu miaka 5 nimekaa pale halijawahi kunidhuru, japo mara kadhaaa nahisi likukuwa linakula kuku wangu
 
Back
Top Bottom