Umeshawahi kukutana na balaa la nyoka?

Umeshawahi kukutana na balaa la nyoka?

Kiboko yake diesel, ikugusa mwili wake anachanika na kukatika vipande.
Kumbe!! Eneo la hapa napoishi niliona gamba la nyoka,, na kuna msingi wa nyumba una vishimo basi nitamimina hiyo diesel maana nyoka sitako hata kuwasikia
 
Kumbe!! Eneo la hapa napoishi niliona gamba la nyoka,, na kuna msingi wa nyumba una vishimo basi nitamimina hiyo diesel maana nyoka sitako hata kuwasikia
Kwenye hivyo vishimo ukipata oil chafu itasaidia sana. Diesel inawahi kukauka.
 
Naomba picha ya cobra boss
Huyu hapa ni Mozambique splitting Cobra ambao hata hapa TZ wapo. Wewe unachanganya na King Cobra ambaye ni mkubwa kama Chatu na ndiye nyoka mwenye sumu mkubwa kuliko wote duniani. Nitakuletea picha yake
Screenshot_20230519-212610.jpg
 
Nyoka wasikie tu, nina shamba lipo katikati ya pori ni balaa. Hela naitaka na uhai nautaka na sehemu inayonipatia kipato ni shamba na siwezi kuliacha ila lina nyoka balaa. Tukio la la kwanza ilikuwa 1920 nikiwa shambani kuna sehemu moja ndio inapatikana network siku hiyo nipo hapo porini nikiwa eneo hilo naongea na simu nikiwa nimesimama zaidi ya dakika 10 kuchungulia nyuma yangu nakuta kuna bonge la kiwiliwili cha mkia wa nyoka kimejilaza kuonyesha niliposimama nyoka amelala katikati ya miguu yangu miwili , kuangaza upande wa pili naona bonge la kichwa bapa cha nyoka aina ya kifutu niliruka kama umeme sikuwa na hamu ya kulima siku hiyo nikarudi nyumbani. Nilipofika nyumbani ndiyo nakumbuka kwa nini sikumuua maana hatari bado inabakia kwangu pale shambani.

Mwaka 2021 nikiwa nimekaa barabarani kando ya shamba hilo hilo majira ya mchana nasubiria usafiri ilipita pikipiki nikaona kitu kwa speed kali kinakatiza kwa kasi mbele ya pikipiki kuvuka barabara kuingia shambani kwangu kukwepa ile pikipiki. Sikuamini kama yule alikuwa nyoka akiwa na speed kama ile kukatiza barabara ya vumbi ikabidi nisogee eneo husika kuona kama kuna mchirizi wa nyoka au macho yangu yaliingia wenge. Bwana we nakaribia kwenye mchirizi nikiangaza pembeni nikakuta bonge la Black mamba kasimama kwenye kwenye ukingo wa tuta la barabara amenizidi urefu tayari kunishambuliwa. Nilishikwa na kiwewe nikakosa nguvu ya kukimbia nikaanza kusali maana hata sikuwa na fimbo mkononi. Nilisimama kama dakika moja bila kupiga hatua sikuamini macho yangu baada ya hiyo dakika moja tukiwa tumetazamana alirudi chini nikaona anatambaa kwenye nyasi anaenda zake nami ndipo nguvu ikaniijia nikaondoka kwa haraka kwa kukimbia kama hussein bolt.

Tukio la tatu mwaka jana hapo hapo shambani nakatiza ndani ya shamba kwenye nyasi majira ya saa mbili asubuhi nikaona bonge la nyoka mbele yangu anang'aa sikujua ni aina gani kabla hajaniona nikageuza kurudi napotokea nikarudi nyumbani kwa woga . Kesho yake nikapita lile eneo kwa umakini kuona kama nitamwona tena nikakuta ngozi yake kumbe lile tukio la jana kuona anang'aa yake alikuwa anajibandua hiyo ngozi yake.

Tukio la mwisho ni mwaka huu mwezi uliyopita kuna sehemu ya msitu nilikuwa nimefyeka hapo hapo shambani nikapachoma moto. Sasa siku ya 2 mida ya asubuhi nikapita eneo hilo kwa mbali nikaona kichwa kama cha nyoka kinazama kwenye shimo sikuwa na hakika kama ni nyoka au mjusi nikaamua kusomba nyasi na magogo ya kutosha nikayasambaza juu ya lile shimo kisha nikawasha moto. Nikakaa kama dakika 30 kipindi yanaungua sikuona kitu kinatoka nikaondoka kuendelea na shughuli zangu hapo shambani. Baada ya masaa 2 nikarudia eneo lile kucheki kama kuna lolote bwana wee kama 40 yako haijafika haija fika tuu . Bila kuchukua tahadhari za kutosha jirani na lile shimo moto ulikuwa unawaka kulikuwa na vichaka vya nyasi kumbe baada ya ule moto kuzidi eneo lile la shimo kulikuwa na bonge la Black mamba ndani akashindwa kuvumilia na joto mule ndani akaamua kufyatuka na kutoka ndani kwa kuungua kaja kutega kandokando ya nyasi. Ile nakaribia tu kaachama mdomo wake anataka kuning'ata nikaruka . Kwa kuwa alikuwa kaungua kaishiwa nguvu hakuwa na nguvu kunifukuza nikatafuta gongo nikampiga hadi nikamuua.

Nyoka WASIKIE TU
Kabla sijaendelea kusoma mkuu hapo ni mwaka 1920 au kuna makosa ya uandishi?
 
Back
Top Bottom