trudie
JF-Expert Member
- Jan 15, 2014
- 4,454
- 10,821
Niliwaza kumbe tuna mhenga wa miaka 100 humu ila nilivyosoma unaongea na simu nikajua basi ni 2020.Typographical error ni 2019 na siyo 1920 mkuu
Niliwaza kumbe tuna mhenga wa miaka 100 humu ila nilivyosoma unaongea na simu nikajua basi ni 2020.Typographical error ni 2019 na siyo 1920 mkuu
Tangu nione hiyo video mtu aling'atwa na nyoka kwenye tako basi kila kuingia chooni naogopa vibaya, tena ilikuwa Uingereza kama sikoseiBasi hii mada ya nyoka leo naogopa hadi kukaa kwenye sinki la choo, maana nilishawahi kuona video nyoka anatokezea chooni. Leo kazi ipo
Mende siogopivipi mende
Mimi kuna kipindi nilisahau ila leo woga umezidi upya...yaani nikitaka kukaa nainuka mwenyewe, ndoo zisipotumika leo sijuiTangu nione hiyo video mtu aling'atwa na nyoka kwenye tako basi kila kuingia chooni naogopa vibaya, tena ilikuwa Uingereza kama sikosei




Wengi sana! Ingia kibaha pori la tumbi hapo,nenda milima ya udzungwa, ruvuma, wapo wengi sana!Bongo tuna Cobra?? Eneo gani?. Ungenambia koboko sawa.
Mi uoga upo kila siku, na mbaya zaidi kuna chamber ilikanyagwa na gari yani kila nikienda toi mawazo km yote, itabidi nimwagie oil huwa namwagia hot water sometimes,, ni kwikwi huyu mdudu sijui kwanini aliumbwaMimi kuna kipindi nilisahau ila leo woga umezidi upya...yaani nikitaka kukaa nainuka mwenyewe, ndoo zisipotumika leo sijui
Kuna nyingine nyoka anatokezea kwenye sinki la choo halafu anarudi ndani.
Naogopa sana na sijawahi ona kwa macho. Mwaka huu mtoto wangu ilikuwaa usiku tupo nje yeye alisimama kwenye majani ghafla akaja analia amegongwa na nyoka mimi sikumwona ila yeye anasema kamuona wa black ( mweusi). Nilikuwa na jirani yangu akamwangalia akasema huyo sio nyoka atakuwa mdudu tuu wa kawaida mimi sijui kitu.We muoga sana
Yaani nachukia sana niki mwona jinsi alivyo mbayaYanga na chura ni kitu kimoja


tunamchokonoahuduma ya kwanza ni nyoka wangu kichwa wazi 😀Sijui hata unapewaje huduma ya kwanza![]()
Ulivyosema ulikuwa unatumia fimbo kupiga nyoka umenikumbusha tukio moja la miaka ya nyuma.
Wakati niko shambani nalima kuna nyoka akakatiza mbele yangu, nikasema huyu simuachi.
Nikachukua fimbo ndefu nikawa namchapa nayo ila alikuwa yuko fasta kukwepa. Ghafla nilikuta nilivyorusha kumchapa akairukia ile fimbo akawa anatembea juu yake kuja kwangu.
Aisee nilipagawa niliachia ile fimbo nikafanya mara 3 ya kile anachokifanyaga Usain Bolt



Wako tele haswa Tabora.Kwahiyo bongo Tuna cobra na koboko
Yaani mnaogopa aina zote za nyoka kweki?🤣Aaah wapi tena wanawake tunaogopa nyoka sana, mie nyoka dudu washa na kinyonga sitaki kuviona kabisaa
Chatu alitaka kunimeza.Lakini kwa vile hii hadithi nimeisimulia mara kadhaa Facebook na wapi,sitaki kuwaboa watu.Kuna mtu ukimtania "hapo chini Kuna nyoka" ni Kama unatafuta kumuua kwa presha, hawapendi kabisa kuleteana utani wa nyoka. Wengine wakijua ndani, nyumba wanazoishi Kuna nyoka ataikimbia nyumba na kuitelekeza kabisa hadi asikie nyoka ameshauawa.
Sasa, Kuna akina sisi ambao huwa hatuogopi nyoka. Kuna baadhi ya matukio nayakumbuka na mengine najiona mjinga Sana kwa kucheza na mdudu huyu hatari Sana.
====
Enzi hizo nipo kijana mdogo wa darasa la tano, siku moja ilikuwa msimu wa baridi Kali (kipupwe). Kwetu kipindi Cha baridi Hali inakuwa tete kwa sisi tusiopenda maji, inafikia wakati baridi linakuwa Kali Hadi mchanga ukikanyaga bila viatu unahisi umekanyaga barafu. Kipindi hiki swala la kuoga linageuka kuwa Jambo la ufahari.
Sasa siku moja nikiwa nimejiandaa mapema Sana ili niwahi shule kuchukua namba maana mwalimu wa zamu alikuwa mnoko. Kwa sababu ya baridi kuwa kali, nikagahilisha swala la kuoga, nikapiga mswaki Kisha nikanawa uso na kutinga uniform tayari kwenda shule. Sasa njiani Kuna zile nyasi zilizopata umande. Nikijiangalia miguuni naona miguu Kama imepakwa chokaa, habari ya kupaka mafuta usiku kabla ya kulala upo kijijini unaanzia wapi? Nikasema hii miguu hapana kwa kweli, imezido kuchakaa, nikawa nimehama njia na kuanza kupita kwenye nyasi zenye maji (umande) ili kusafisha miguu. Hapo miguuni nimevaa kandambili alafu kitendo Cha kupita kwenye nyasi zenye maji zikawa Safi hadi nikiwa nainua mguu kandambili inaitika waah!! .Watoto wa siku hizi wa gari za njano na wakiamka wanasalimia good morning Dad and mamy hawaelewi hizi mambo za kunawa maji ya umande.
Sasa wakati nimehama njia natembea kwenye nyasi ili kuosha miguu, huku kidumu na fagio vipo mikononi, Ghafla..!! Cobra akiwa amevimbisha shingo huku amejaza mate yenye sumu alikuwa ameshajihami yupo mbele yangu tayari yupo katika mkao wa kushambulia. Wakati nimetaharuki nawaza nini Cha kufanya yeye ndiyo kwanza akasogea barabarani kweupe kabisa. Ni Kama alisogea mbele kuniblock nisiende shule. Nikaangalia nyuma Kama Kuna mtu anakuja nikawa naona ukungu tu, nilikuwa mzee wa kuwahi Sana. Wale wanafunzi wanaowahi sana shule. Nidhamu nyingi. Hata hivyo kwa sababu sikuwa mwoga wa nyoka nikasema leo mbona tutanyooshana tu. Pembeni yangu kulikuwa na mti mrefu kidogo nikauchukua nikatoa vitawi ikabaki fimbo. Nikaanza kumrushia.
Sasa Cobra kwa kukwepa ndiyo mwaliku wao. Kila nikirusha anakwepa alafu ananifokea balaa huku amejaza lundo la mate yenye sumu shingoni. Lakini Cha ajabu Wala harudishi mashambulizi wala kunitemea mate yake yaliyojaa shingoni yenye sumu Kali.
Kumbe nyoka ana akili Sana.
Wakati najiona Kama napambana nae nimuue kumbe mwenzangu ananiona Kama mtoto tu nisiye na hatia akawa ananikwepa pasi na kunidhuru. Ilikuwa Kama anacheza na Mimi maana hata nguvu ya kurusha ule mti ilikuwa dhaifu Sana kwa sababu ya umri wangu.
Alipoona nimetaharuki huku macho yamenitoka Kama tochi nakaribia kulia alafu sina msaada akaamua kuinama chini na kusepa mdogo mdogo na kuishia zake porini. Alipotokomea ndiyo nikakumbuka Kumbe nilibeba kidumu cha maji na fagio, sijui nimevitupa wapi. Nikavitafuta nikakuta nilivitupa kwenye majani, maji yameshamwagika maana kidumu hakikuwa na mfuniko. Nikasepa zangu shule miguu ikiwa haina nguvu kabisa.
Ila sikukoma, niliendelea na tabia yangu ya hovyo na kukutana na balaa la nyoka? Ilikuwaje?
Ulifanya uzembe mkubwa sana yaani kupuuzia, huyo ni Kobra moja kwa mojaNaogopa sana na sijawahi ona kwa macho. Mwaka huu mtoto wangu ilikuwaa usiku tupo nje yeye alisimama kwenye majani ghafla akaja analia amegongwa na nyoka mimi sikumwona ila yeye anasema kamuona wa black ( mweusi). Nilikuwa na jirani yangu akamwangalia akasema huyo sio nyoka atakuwa mdudu tuu wa kawaida mimi sijui kitu.
Tumekaa ndani kama dk 5 hivi mguu ukaanza kuvimba, bahati kuna bodaboda niliagiza msosi akawa analeta akashangaa leo mbona anko mpole sio kawaida yake nikamwambia kuna mdudu kamng'ata anavimba mguu kuja kumwangalia nusu aninase vibao aisee.
Akamfunga mguu kumbeba mbio mpaka kwa huyo mzee anamjua ndio kumpa dawa ya kunywa na nyingine akampaka na kusugulia mguu wote. Akaendelea na dawa hizo siku hadi ilipoisha Yule boda boda alinambia kama nisingekuja kwa dk 10 mbele ulikuwa unamkosa mtoto huyu. Yaani sikulala karibia wiki kwa woga.
Zoote hata kiwe kidogo km mnyoo, kwanza mnyoo nauogopa naoYaani mnaogopa aina zote za nyoka kweki?🤣