Umeshawahi kukutana na balaa la nyoka?

Umeshawahi kukutana na balaa la nyoka?

Nilikuwa naishi maeneo ya changanyikeni, karibu na kikosi Cha jeshi, Sasa jirani na kwangu kulikuwa na mti.
Yaaani kila siku mchana Kuna joka lefuuu la kijivu ni refu sana linaotea jua kwenye huo mti na likichoka linashuka linaingia shimoni kwenye mshimo!
Cha ajabu miaka 5 nimekaa pale halijawahi kunidhuru, japo mara kadhaaa nahisi likukuwa linakula kuku wangu
Hao nyoka wa kijani hawana shida na mtu kabisa, labda ukiwachokoza ndiyo utanunua kesi
 
Nilikuwa naishi maeneo ya changanyikeni, karibu na kikosi Cha jeshi, Sasa jirani na kwangu kulikuwa na mti.
Yaaani kila siku mchana Kuna joka lefuuu la kijivu ni refu sana linaotea jua kwenye huo mti na likichoka linashuka linaingia shimoni kwenye mshimo!
Cha ajabu miaka 5 nimekaa pale halijawahi kunidhuru, japo mara kadhaaa nahisi likukuwa linakula kuku wangu
Sasa kama ulilijua shimo mbona uliliacha?
 
Kun siku wakati nipo mdogo almost Darasa la 5 hiviii, tulienda Porini kukata kuni. Wakat tupo porini kila mmoja aliingia sehem iliyomfaa ili akate kuni,
Mimi nilienda sehemu kukata kuni lakini nikiwa kule nikaona kama kichwa kinaniuma iviii hivyo nikatafuta kivuli cha mtu ili nipumzike baadaye nikapitiwa na Usingizi. Nikiwa usingizini nikasikia kama naitwa hiviiii kumbe wenzangu wamekata kuni wamefunga wanataka kuondoka hawanioni, wakajaribu kuniita siitiki wakaamua waondoke kurudi nyumbani
Nimelala pale baadaye nikawa kama naota iviiii kua kuna kitu cha baridiiiii kinanipitia mgongoni, (nikiwa ndotoni sijui au hali halisi) nikatulia kimya hadi ule ubaridi ulipoishaaa baada ya dakika kama 10 hivi ndo nikaamka kwa kukurupuka pale nlipolala.
Nikaamka kwa Wenge sana na kuanza kuwaita wale wenzangu huku nikikimbia kutafuta njia ya kurudi nyumban

Nafikiri ni Nyoka mkubwa alipita wakati nmelala pale chini. Ni Mungu tu alininusuru na Nyoka uyo. Baada ya kama Wiki Nyoka mkubwa sana aliuawa maeneo yale
 
Kuna mtu ukimtania "hapo chini Kuna nyoka" ni Kama unatafuta kumuua kwa presha, hawapendi kabisa kuleteana utani wa nyoka. Wengine wakijua ndani, nyumba wanazoishi Kuna nyoka ataikimbia nyumba na kuitelekeza kabisa hadi asikie nyoka ameshauawa.

Sasa, Kuna akina sisi ambao huwa hatuogopi nyoka. Kuna baadhi ya matukio nayakumbuka na mengine najiona mjinga Sana kwa kucheza na mdudu huyu hatari Sana.


====


Enzi hizo nipo kijana mdogo wa darasa la tano, siku moja ilikuwa msimu wa baridi Kali (kipupwe). Kwetu kipindi Cha baridi Hali inakuwa tete kwa sisi tusiopenda maji, inafikia wakati baridi linakuwa Kali Hadi mchanga ukikanyaga bila viatu unahisi umekanyaga barafu. Kipindi hiki swala la kuoga linageuka kuwa Jambo la ufahari.

Sasa siku moja nikiwa nimejiandaa mapema Sana ili niwahi shule kuchukua namba maana mwalimu wa zamu alikuwa mnoko. Kwa sababu ya baridi kuwa kali, nikagahilisha swala la kuoga, nikapiga mswaki Kisha nikanawa uso na kutinga uniform tayari kwenda shule. Sasa njiani Kuna zile nyasi zilizopata umande. Nikijiangalia miguuni naona miguu Kama imepakwa chokaa, habari ya kupaka mafuta usiku kabla ya kulala upo kijijini unaanzia wapi? Nikasema hii miguu hapana kwa kweli, imezido kuchakaa, nikawa nimehama njia na kuanza kupita kwenye nyasi zenye maji (umande) ili kusafisha miguu. Hapo miguuni nimevaa kandambili alafu kitendo Cha kupita kwenye nyasi zenye maji zikawa Safi hadi nikiwa nainua mguu kandambili inaitika waah!! .Watoto wa siku hizi wa gari za njano na wakiamka wanasalimia good morning Dad and mamy hawaelewi hizi mambo za kunawa maji ya umande.

Sasa wakati nimehama njia natembea kwenye nyasi ili kuosha miguu, huku kidumu na fagio vipo mikononi, Ghafla..!! Cobra akiwa amevimbisha shingo huku amejaza mate yenye sumu alikuwa ameshajihami yupo mbele yangu tayari yupo katika mkao wa kushambulia. Wakati nimetaharuki nawaza nini Cha kufanya yeye ndiyo kwanza akasogea barabarani kweupe kabisa. Ni Kama alisogea mbele kuniblock nisiende shule. Nikaangalia nyuma Kama Kuna mtu anakuja nikawa naona ukungu tu, nilikuwa mzee wa kuwahi Sana. Wale wanafunzi wanaowahi sana shule. Nidhamu nyingi. Hata hivyo kwa sababu sikuwa mwoga wa nyoka nikasema leo mbona tutanyooshana tu. Pembeni yangu kulikuwa na mti mrefu kidogo nikauchukua nikatoa vitawi ikabaki fimbo. Nikaanza kumrushia.

Sasa Cobra kwa kukwepa ndiyo mwaliku wao. Kila nikirusha anakwepa alafu ananifokea balaa huku amejaza lundo la mate yenye sumu shingoni. Lakini Cha ajabu Wala harudishi mashambulizi wala kunitemea mate yake yaliyojaa shingoni yenye sumu Kali.

Kumbe nyoka ana akili Sana.

Wakati najiona Kama napambana nae nimuue kumbe mwenzangu ananiona Kama mtoto tu nisiye na hatia akawa ananikwepa pasi na kunidhuru. Ilikuwa Kama anacheza na Mimi maana hata nguvu ya kurusha ule mti ilikuwa dhaifu Sana kwa sababu ya umri wangu.

Alipoona nimetaharuki huku macho yamenitoka Kama tochi nakaribia kulia alafu sina msaada akaamua kuinama chini na kusepa mdogo mdogo na kuishia zake porini. Alipotokomea ndiyo nikakumbuka Kumbe nilibeba kidumu cha maji na fagio, sijui nimevitupa wapi. Nikavitafuta nikakuta nilivitupa kwenye majani, maji yameshamwagika maana kidumu hakikuwa na mfuniko. Nikasepa zangu shule miguu ikiwa haina nguvu kabisa.

Ila sikukoma, niliendelea na tabia yangu ya hovyo na kukutana na balaa la nyoka? Ilikuwaje?
Nyokaa n kifo mkuu Eva alivyompa adamu liletunda tukaachiwa dhahama ya kifo
 
Hapana mkuu,

Cobra ni nyoka mwingine na koboko ni mwingine pia. Na Kati ya hao wawili hatari zaidi ni koboko,ni nyoka mwenye kisirani na anapenda sifa za kijinga.

Unaweza kwenda kuchunga ng'ombe yet akaamua kukutia hasara akawagonga ng'ombe wote ili wafe tu akutie umasikini. Cobra anavimba Sana kwenye mashavu akiwa na hasira na anatema mate yenye sumu,nakumbuka cobra ameshawahi kumtia upofu ng'ombe wa shule kwa kumtemea mate yenye sumu Kali.
Maelezo mazuri sana hapa umemtofautishia Mamba na Cobra
 
Hapana mkuu,

Cobra ni nyoka mwingine na koboko ni mwingine pia. Na Kati ya hao wawili hatari zaidi ni koboko,ni nyoka mwenye kisirani na anapenda sifa za kijinga.

Unaweza kwenda kuchunga ng'ombe yet akaamua kukutia hasara akawagonga ng'ombe wote ili wafe tu akutie umasikini. Cobra anavimba Sana kwenye mashavu akiwa na hasira na anatema mate yenye sumu,nakumbuka cobra ameshawahi kumtia upofu ng'ombe wa shule kwa kumtemea mate yenye sumu Kali.
Hivi cobra ndio swila, au ni nyoka wawili tofauti?
 
Back
Top Bottom