Umeshawahi kukutana na balaa la nyoka?

Umeshawahi kukutana na balaa la nyoka?

Kuna mtu ukimtania "hapo chini Kuna nyoka" ni Kama unatafuta kumuua kwa presha,hawapendi kabisa kuleteana utani wa nyoka. Wengine wakijua ndani, nyumba wanazoishi Kuna nyoka ataikimbia nyumba na kuitelekeza kabisa hadi asikie nyoka ameshauawa.

Sasa,Kuna akina sisi ambao huwa hatuogopi nyoka. Kuna baadhi ya matukio nayakumbuka na mengine najiona mjinga Sana kwa kucheza na mdudu huyu hatari Sana.


==============================================
Enzi hizo nipo kijana mdogo wa darasa la tano,siku moja,ilikuwa msimu wa baridi Kali (kipupwe). Kwetu kipindi Cha baridi Hali inakuwa tete kwa sisi tusiopenda maji,inafikia wakati baridi linakuwa Kali Hadi mchaanga ukikanyaga bila viatu unahisi umekanyaga barafu. Kipindi hiki swala la kuoga linageuka kuwa Jambo la ufahari.

Sasa siku moja nikiwa nimejiandaa mapema Sana ili niwahi shule kuchukua namba maana mwalimu wa zamu alikuwa mnoko,Kwa sababu ya baridi kuwa kali,nikagahilisha swala la kuoga,nikapiga mswaki Kisha nikanawa uso na kutinga uniform tayari kwenda shule. Sasa njiani Kuna zile nyasi zilizopata umande. Nikijiangalia miguuni naona miguu Kama imepakwa chokaa,habari ya kupaka maguta usiku kabla ya kulala upo kijijini unaanzia wapi? Nikasema hii miguu hapana kwa kweli,imezido kuchakaa, nikawa nimehama njia na kuanza kupita kwenye nyasi zenye maji (umande) ili kusafisha miguu. Hapo miguuni nimevaa kandambili alafu kitendo Cha kupita kwenye nyasi zenye maji zikawa Safi hadi nikiwa nainua mguu kandambili inaitika waah!! .Watoto wa siku hizi wa gari za njano na wakiamka wanasalimia good morning Dad and mamy hawaelewi hizi mambo za kunawa maji ya umande.

Sasa wakati nimehama njia natembea kwenye nyasi ili kuosha miguu,huku kidumu na fagio vipo mikononi..Ghafla..!! Cobra akiwa amevimbisha shingo huku amejaza mate yenye sumu alikuwa ameshajihami yupo mbele yangu tayari yupo katika mkao wa kushambulia. Wakati nimetaharuki nawaza nini Cha kufanya yeye ndiyo kwanza akasogea barabarani kweupe kabisa. Ni Kama alisogea mbele kuniblock nisiende shule. Nikaangalia nyuma Kama Kuna mtu anakuja nikawa naona ukungu tu,nilikuwa mzee wa kuwahi Sana,Wale wanafunzi wanaowahi sana shule..Nidhamu nyingi!!! Hata hivyo kwa sababu sikuwa mwoga wa nyoka nikasema leo mbona tutanyooshana tu!! Pembeni yangu kulikuwa na mti mrefu kidogo nikauchukua nikatoa vitawi ikabaki fimbo. Nikaanza kumrushia.

Sasa Cobra kwa kukwepa ndiyo mwaliku wao,Kila nikirusha anakwepa alafu ananifokea balaa huku amejaza lundo la mate yenye sumu shingoni. Lakini Cha ajabu Wala harudishi mashambulizi wala kunitemea mate yake yaliyojaa shingoni yenye sumu Kali.

Kumbe nyoka ana akili Sana.

Wakati najiona Kama napambana nae nimuue,Kumbe mwenzangu ananiona Kama mtoto tu nisiye na hatia akawa ananikwepa pasi na kunidhuru. Ilikuwa Kama anacheza na Mimi maana hata nguvu ya kurusha ule mti ilikuwa dhaifu Sana kwa sababu ya umri wangu.

Alipoona nimetaharuki huku macho yamenitoka Kama tochi nakaribia kulia alafu sina msaada akaamua kuinama chini na kusepa mdogo mdogo na kuishia zake porini. Alipotokomea ndiyo nikakumbuka Kumbe nilibeba kidumu cha maji na fagio,sijui nimevitupa wapi. Nikavitafuta nikakuta nilivitupa kwenye majani,maji yameshamwagika maana kidumu hakikuwa na mfuniko. Nikasepa zangu shule miguu ikiwa haina nguvu kabisa.

Ila sikukoma,niliendelea na tabia yangu ya hovyo ya n kukutana na balaa la nyoka? Ilikuwaje?
Nitarudi ngoja Nile Kisha nisome hii isidingo
 
Nyoka hatari sana,hasa unapomchokoza,Kama huna uelewa na kuwafahamu nyoka basi ni vyema ukaachana nae.

Maana inaweza ukajidanganya umeshika panga na fimbo lakini ukachokoza balaa ambalo halitakuwa na msaada wowote kwa ulivyokuwa navyo

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
Hivi chatu anaweza kukimbiza mtu zaidi ya kukuvizia?
 
Nyoka hatari sana,hasa unapomchokoza,Kama huna uelewa na kuwafahamu nyoka basi ni vyema ukaachana nae.

Maana inaweza ukajidanganya umeshika panga na fimbo lakini ukachokoza balaa ambalo halitakuwa na msaada wowote kwa ulivyokuwa navyo

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
Usipende kuua nyoka kama hayupo nyumbani kwako
 
Koboko ni yule ambaye huwa anagonga Utosi Satoh?
Huyo huyo.

Moja Kati ya viumbe katili duniani,na ana hasira Kali balaa,ugomvi wake hauishi Hadi mmoja Kati yenu awe amekubali yaishe(kifo).

Ukimkuta amelala barabarani ukasema umgonge na kigari chako ana tabia ya kujificha chini ya uvungu,mwisho wa safari yako ukishuka nae anatoka uvunguni mmalizane kiroho mbaya.
 
Aisee, mimi naogopa nyoka. Nyoka nawaogopa kiasi kwamba nikimuona tu, naanza kuhisi kuishiwa nguvu kwenye joint zate za miguu. ophidiophobia yangu ni ya kiwango cha juu sana. Hataa huu uzi tuu kuusoma kunanamna umenichukua.

Juzi kati tuu hapa nimesoma habari mtandaoni huko kenye mtoto aling'atwa na kitu usiku wamelala, alivozidiwa wakampeleka hospitali akaenda kufa. Ila wakaambiwa ameng'atwa na nyoka. Walivorudi nyumbani wakamkuta cobra kajizungusha kwenye blanketi walilokuwa wamejifunika. Hiyo habari inanipa wakati mgumu usiku nikilala. Hadi leo.

1. Miaka ya nyuma, kulikuwa na kichaka cha wastani kwenye shamba letu la mihogo. Palikuwa na uvumi kwamba kile kichaka ni makazi ya chatu. Na kuna watu waliwahi kikiri kabisa kumwona chatu akiingia na kutoka kwenye kile kichaka sio mara moja.

Mzee wangu alitafuta watu wa kukifyeka kile kichaka lakini hakupata. Watu waliogopa kujigeuza kitoweo cha chatu kwaajili ya vijisenti.

Mimi wakati huo ndo nmemaliza form four nasubiri matokeo nipo tu home najishughulisha na kazi za shamba. Jioni moja mzee akanichukua tukakifyeke kile kichaka. Niseme tuu kwamba kazi tuliifanya hadi ikaisha na hatukukuta chatu wa dalili ya chatu ila hakuna wakati nmewahi kuuona mgumu maishani mwangu kama wakati tunafyeka kile kichaka.

2. Mwaka 2015 nilikuwa najitolea kufundisha shule moja ya kata. Nilikuwa hosted pale pale shuleni. Kwenye ile nyumba tulikuwa tunaishi watatu, kila mmoja chumba chake tunashea sebule.

Ile shule ilikuwa na hostel. Baadhi ya wanafunzi hasa wa mbali walikuwa wanakaa hostel. Kwahyo walikuwa wajisomea madarasani usiku (Prepo)

Siku hiyo nimeenda kuzurura jioni. Mida ya saa mbili usiku nikarudi. Nikamkuta ticha mwenzangu kakaa sabuleni. Ile nataka kwenda chumbani kwangu akaniambia 'kuna nyoka huko'. Nilikuwa kama nimepigwa shoti ya umeme. Yaani nyoka, chumbani kwangu?!!. Nikamuuliza nimkubwa, akasema ni wa wastani tuu. Yule jamaa ni wale watu wasioogopa nyoka. Lakini kwangu, nyoka ni nyoka.

Nikamuuliza ameingiaje humu. Akaanza kunisimulia. Kwamba alikuwa amekaa pale pale alipokuwa, akasikia kama kitu kinakwaruza kwenye floor. Kutupa jicho akamuona nyoka mweusi anamfukuzia chura. Wametokea nje, wamepita sebuleni wakaenda chumba cha ticha mmoja hakuwepo.

Yeye akaanza kuwafuata kwa nyuma. Baade yule nyoka akahisi anafuatwa, akakurupuka arudi atoke nje. Akakutana uso kwa uso na ticha. Nyoka akabadili uelekeo ndo akaingia chumbani kwangu. Muda huo nasikiliza hiyo story nahisi kuishiwa nguvu kabisa.

Nikamuuliza sasa mbona hujamuua. Akanambia ameita madogo (wanafunzi) waje wamuue. Tunazungumzia nyoka lakini jamaa amekaa kwa kurelax utafikiri tunazungumzia panzi.

Dakika sifuri nikaona vijana wamefika. Kamawatano hivi na silaha za jadi. Wakazama rum wakaanza kumtafuta nyoka. Mi ndo kwanza nikaondoka kabisa. Asije akakurupushwa huko anikimbilie mimi.

Baada ya kama nusu saa nikarudi. Bado wanamsaka. Ile nauliza tu 'hawajampata?' Nikasikia chumbani huyo huyo huyoo.... paa...paa...kii..kii... tayari.

Kwa mashambulizi yale ilikuwa ni mda mfupi tu nyoka akakata kauli. Wakamto sasa. Aisee. Cobra jeusi tii...lirefu unene wa kufikia tairi ya baiskeli. Nilitetemeka balaa. Wakaliweka hapo nje tukaanza kulipiga picha.

Niliingia chumbani kwa hofu kubwa. Chumba kimeparaganyika. Walipoliulia limeacha damu nyingi sana. Damu inatoa haru. Inanuka yani. Nikaifuta nikapanga panga kwa tahadhari kubwa. Siku hiyo nililala kwa shida sana. Usingizi wa mang'amung'amu.

Kama mimi ningekuwa jasiri wa nyoka, ningekuwa nawafuga. Sumu ya nyoka inalipa sana.
 
Huyo huyo.

Moja Kati ya viumbe katili duniani,na ana hasira Kali balaa,ugomvi wake hauishi Hadi mmoja Kati yenu awe amekubali yaishe(kifo).

Ukimkuta amelala barabarani ukasema umgonge na kigari chako ana tabia ya kujificha chini ya uvungu,mwisho wa safari yako ukishuka nae anatoka uvunguni mmalizane kiroho mbaya.
Hii ni hadithi za abunuasi.
Unaujua uvungu wa gari wewe?
Joto lote?
 
Back
Top Bottom