Umeme wa REA kiukweli umeleta changamoto sana kwa baadhi ya waombaji wapya wa Umeme

luangalila

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
6,325
6,871
Pamoja na serikal ilifanya vizuri kuja na mradi wa kuleta umeme katika maeneo ya mbali na mijin

Kwa maoni yangu naona bado katika baadhi ya utekelezaj wa mradi hii watekelezaji walivurunda sanaa hasa katika swala la kuzingatia uwekaji nguzo katika mipaka baina ya kiwanja kimoja na kingine

Yapo maeneo nguzo zimeingia ndani katika kiwanja cha mtu, na hapa sasa ndipo hoja yangu ilipo, kwa sababu kwa case kama hii mmiliki wa kiwanja huzuia hata nyumba za jirani kuvuta umeme kutoka katika nguzo iyo kwa kigezo tu ana taka kulalamika nguzo ihamishwe na zoezi la uhamishaji nguzo ni mchakato sanaaa

Ukizingatia umeme wa REA wakati una wekwa wao walikuwa wana fuata makazi yaan watu walipo ndio maana una kuta nguzo za rea zimekaa shaghala baghala zig zag ovyo ovyo tu
 
Back
Top Bottom