Umeme umekuwa janga la Taifa, Rais jitokeze uiambie Taifa ukweli

saigilomagema

JF-Expert Member
Jun 5, 2015
4,173
6,157
Watanzania wenzangu sijaona hali mbaya ya umeme km wakati huu. Tuliambiwa ilikuwa tatizo la upungufu wa maji kutokana na ukame.

Mvua imenyesha tangia mwezi wa 11 na mpaka sahivi inanyesha mpaka imekuwa kero. Lakini hakuna umeme na hali ndiyo imekuwa mbaya sana, hata km watanzania mmezoea ni wavumilivu hii hali haivumiliki.

Umeme unakatwa tangia asubuhi unaweza kurudi usiku mmeshalala, mnaamka mara ghafla kabla ya saa 2 umekatwa tena. Rais km mkuu wa nchi tuambie tatizo ni nini, tumechoka na ngonjera za wasaidizi wako.

Kama wanakuhujumu chukua hatua. Huku nilipo hali ni mbaya sijawahi ona ktk awamu yoyote ile iliyopita ya uongozi. Inakera, inaudhi tuko gizani. Maisha gani haya tunaishi dunia ya leo wakati karibu kila shughuli inahitaji umeme?
 
Nenda Chunya ukaone makali ya umeme.
Kuna hata nyaya za umeme wezi wameamua kuzichukua na kuuza kwenye wanunuzi wa vyuma chakavu.
 
Niko Arusha yaani kama upo Insungangwada kule Ubilimbi Kahama ndani ndani.....

Wakenya Wanatucheka kweli kweli na sisi tumeona UMEME NI ANASA.. ......hiii bhagosha Gete Gete???,
 
Usikute kuna biashara ya majenereta!! Anaefanya hivyo ni muuwaji, kuna anaetegemea umeme ili mkono uende kinywani, huyo hana uwezo wa kununua jenereta.
 
Kuna ng'ombe inasmama Mahali inapga kelele kua kuna raisi
 
sio janga la kitaifa,

umeme upo wa kutosha hivi sasa, ila ipo kasoro kwenye miundombinu ambayo imebainika ni mikuu kuu mno, jambo ambalo linashughulikiwa kwa bidii sana na karibuni litakamilika na adha kidogo ya umeme kukatika inayowakumba baadhi ya waTanzania katika baadhi ya maeneo itakwisha 🐒

Bado ni suala lililo chini ya uwezo wa wizara na linaloweza kutatuliwa kisekta bila kauli au mgono wa Rais,

subira yavuta kheri...
Kwa Neema na Baraka za Mungu, hili nalo litapita Salama Salimini ...
 
Maajabu ya Dunia Iringa lilipo bwawa la mtera na mvua inanyesha kila siku, hapa mjini hatuna umeme!
Hii nchi inahitaji mabadiliko, tuamke aisee!
 
sio janga la kitaifa,

umeme upo wa kutosha hivi sasa, ila ipo kasoro kwenye miundombinu ambayo imebainika ni mikuu kuu mno, jambo ambalo linashughulikiwa kwa bidii sana na karibuni litakamilika na adha kidogo ya umeme kukatika inayowakumba baadhi ya waTanzania katika baadhi ya maeneo itakwisha ...
Acha siasa wewe watu wanateseka, wanafilisika unaongea upupu hapa
 
Unataka aseme ukweli iki chama kianguke kwenye uchaguzi mkuu ujao?

Watu wanakusanya maokoto ya kununulia khanga na Tshirts za uchaguzi
 
Back
Top Bottom