Kuhani
Watu huchukua misimamo mbalimbali, kuna wasio na misimamo, wenye misimamo na kuna wale ambao hawajijui kuwa wana msimamo ama hawana. Kuna wenye uthubutu wa kuchukua hatua mbele zaidi na kuzuia madhara wanayohisi yaweza kutokea kutokana na aina ya msimamo walionao, na kuna wale ambao wanasubiri madhara yatokee halafu waseme 'nilijua tu pataharibika' na kuna wale ambao hata madhara yakitokea hawajali. Hawa ni wenzetu na ni lazima kuwa nao, hatuwezi kuwatenga.
wale mafundi vibatari wataupgrade na kuuza zaidi. Wataanza kutengeneza majeri ken ya kumwagilia badala ya kutengeneza vibatari; hii itawaongezea kipato kwani jeri keni moja bei yake ni juu kuliko ya kibatari. Kumbuka unaweza kukaa na kibatari miaka mitano bila kununua kingine (kinawekwa pale kumulika tu-hakipati mikiki). Hata hivyo umeme utawasaidia kufanya kazi kwa urahisi na kutoa products zenye ubora utakaokidhi masoko nje ya nchi.
...sasa Rev. Kishoka yupo ktk kundi gani?? mie nahisi yupo ktk hilo kundi la "nilijua tu pataharibika"
...usitolee sana macho haya mambo, ningekuwa mwandishi ningekupa lecture, lakini kwa bahati mbaya mie ni mtu wa domo zaidi kuliko kalamu....eazy now.
...umefikiria sana!! hahahaha kama ni vipodozi basi umejidodeka..
Kwani wewe uko kwenye kundi gani?
kwa sasa mie nipo kwenye kundi la, "wale ambao hata madhara yakitokea hawajali." Vipi unataka nikupe sababu au umeridhika kulijua kundi langu?
hivi kukiwa na umeme sasa wale mafundi wa sido wa vibatari (wakina joe the plumber wa kibongo) wakale wapi? acheni nyinyi maneno yenu.........kukosekana kwa umeme ni industry flani na kupatikana kwake kunapunguza ajira!!
hizo ni two cents zangu, in a nutshell.....
Kuhani,
On a serious note though, hivi umeona kuwa natumia mgongo wa Nyani kutukana Watanzania na kuona sina kende kutukana kwa mdomo wangu mwenyewe?
Si wewe uliyeshangilia nilipomsiliba FMES kwenye hoja moja mpaka ukatoa tuzo ya Mtu mwenye Makende ya Chuma?
Umepitia Screw Muungwana? Je CCM adui wa Maendeleo nako huko nimekosa mfupa?
Sasa kwenye hili la Nishati na kutumia maneno ya Nyani "Ndivyo Tulivyo" nimekosea nini kueleza ukweli kuwa Serikali yetu na watendaji wake ni wavivu wa kufikiri, kupanga mambo na kuingia gharama?
Wewe ni mchumi, tupe basi zako nasaha kuwa tufanyeje zaidi ya kupembua utata wa tungo zangu au wasifu wangu.
tatizo la miradi mingi tanzania ni kuweka maslahi binafsi mbele kuliko National interest au tuseme kitu ambacho kitakuwa na faida kiuchumi. Ndio maana utaona leo hii Viongozi wetu wanafurahia umeme wa Vibaba, badala ya kuwa na Grand Project kama atleast kama Kidatu, to cut the story short, mradi wanaotakiwa kuwekeza ni huo wa Stigler, mingine ni hiyo ya upepo, na jua, sasa labda hamna kamisheni ya kutosha ndio maana wanakimbilia miradi ya dharura
tatizo la miradi mingi tanzania ni kuweka maslahi binafsi mbele kuliko National interest au tuseme kitu ambacho kitakuwa na faida kiuchumi. Ndio maana utaona leo hii Viongozi wetu wanafurahia umeme wa Vibaba, badala ya kuwa na Grand Project kama atleast kama Kidatu, to cut the story short, mradi wanaotakiwa kuwekeza ni huo wa Stigler, mingine ni hiyo ya upepo, na jua, sasa labda hamna kamisheni ya kutosha ndio maana wanakimbilia miradi ya dharura
Kusema sisi Miafrika ni Ndivyo Tulivyo sio tusi. Ni ukweli na watu wanajua kuwa ndio ukweli..and just like the old adage goes...truth hurts.............
Lakini Nyani, hawa hawa watanzania wanaonekana kwenye nchi yao hawawezi kufanya kazi au kuengeneza anything productive wakienda kwenye nchi za watu wanasifika kwa ufanyaji kazi na wenyeji wao wanawatumia kuleta maendeleo. Ukichukulia Botswana, Namibia, Rwanda watanzania wengi tu wamezisaidia hizi nchi kusonga mbele.
Mifano mingine ni waliopo/waliokuwepo kwenye mashirika ya kimataifa, kama kina merehemu Balali, wakati wakiwa huko walikuwa ni wafanyakazi wazuri na wenye sifa kibao mpaka kuombwa kuja nyumbani. Mimi nadhani tatizo kubwa la tanzania ni 'system' yetu ya utawala inayojumuisha mambo mengi kama utungaji wa sera na malengo, utekelezaji wake, evaluation & monitoring, uwajibikali wa serikali na kiongozi mmoja mmoja etc...Kwa ujumla sijui nchi kama nchi tunajua tunataka nini na tufikaje huko tunakotaka kwenda.
Huko kwenye nchi za watu kila kitu kiko tayari na kilitengenezwa ama kuundwa na wenye nchi yao. Sisi tukienda huko tunavikuta tu. Sasa kama unasema "system" yetu ni mbovu na tunajua kuwa ni mbovu kwa nini sasa tusitengeneze inayofaa kama tunaweza?
Hao kina Balali wanafanya kazi huko majuu kwa kusimamiwa na wazungu na wanafanyia kazi makampuni na mashirika yaliyoanzishwa na wazungu. Kwa hiyo hoja yako iko nullified...
Ndio maana nimetolea mfano nchi kama Rwanda(recent example), Botswana, Namibia .....ambazo ni za waafrika wenzetu lakini walikaa chini wakaamua wapi wanataka kwenda na watafikaje. Mkishajiuliza maswali hayo mtajua kuwa kama ni kuwa na viwanda & uwekezaji wa nguvu tunahitaji umeme wa uhakika na wa bei rahisi kama moja ya goal, issue itakuwa tutaupataje? then utaweka strategy. Baadya ya hapo utaangalia sehemu zote muhimu na mwisho kutokana na uwezo utaamua kuanza lipi na lipi lifuate.
Kwa hiyo wakifanya hivyo tatizo la umeme kwisha habari yake...?
Hao nao hawana tofauti kubwa na sisi. Wote ni ulimwengu wa tatu tu