Umeme na Nishati: Tatizo sugu Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umeme na Nishati: Tatizo sugu Tanzania

Discussion in 'Great Thinkers' started by Rev. Kishoka, Nov 13, 2008.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Jana nimejiuliza sana kwa nini Tanzania tunahangaika na ukosefu wa umeme kila mwaka na hata kuzorotesha uchumi n kukua kwa maendeleo? nikajiuliza ni mvua, mabwawa au mitambo? Nikapata tamati kuwa ni watu au kwa maneno sahihi ni Uongozi pofu na mbovu.

  Leo hii nadamka asubuhi nasoma gazeti, nakutana na hii kauli ya Waziri Mkuu Pinda anayesema tukaribishe wawekezaji!

  Je Tanzania si kuna IPTL, Songas, Agreko, Kiwira,Richmond, Dowans, Tanesco na Ewura na wengine wengi ukiongezea majenereta? Sasa kama tuna makampuni na taasisi zote hizi, kwa nini tuendelee kusema tunahitaji wazalishaji wapya wa umeme?

  Kwani mahitaji yetu ni kiasi gani kwa mwaka? je mabwawa ya maji ya Kidatu, Handeni, Wami, Nyumba ya Mungu, Mtera, Kihansi na hata hili jipya la Ruhiji yana uwezo wa kuzalisha umeme wa kiasi gani?

  Je gesi, mafuta, makaa ya mawe, jua na upepo zinatuzalishia megawati ngapi kila siku au kila mwaka kukidhi mahitaji ya Taifa?

  Hivi kweli Tanzania tuna sera kamambe ya kujijenga katika miundombinu kama Umeme, Barabara, Maji, Simu, Bandari, Reli na mengineyo ambayo ni muhimu kwa kujenga Taifa lenye uchumi imara au kama suala la Umeme na Nishati tunakimbilia kusema "njooni wawekezaji"?


   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Nov 13, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,406
  Trophy Points: 280
  Unajua ninachotaka kusema lakini sitakisema.....
   
 3. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Nyani,

  Wala usione aibu, sema wazi tukusikie, "ndivyo tulivyo", wavivu w kufikiria, wavivu wa kufanya kazi, waoga wa kuingia gharama, tuliokosa ubunifu na zaidi mwamko wa uzalendo=Kutegemea misaada!
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Nov 13, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,406
  Trophy Points: 280
  You said it!!!!
   
 5. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #5
  Nov 14, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Fundi Mchundo, Mwalimu Kichuguu,

  Hivi Tanzania inahitaji umeme kiasi gani kwa mwaka na tuna uwezo wa kuzalisha umeme wa kiasi gani kupitia mabwawa ya maji tuliyonayo?
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Nov 14, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Kwani tatizo la umeme Tanzania limetokana na nini? tumezungukwa na maziwa makubwa matatu, tuna mito bwelele, mabonde kibao n.k kwanini bado tunahangaika na nishati?
   
 7. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #7
  Nov 14, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Chagua upande. Simama uhesabiwe.

  _____________
   
 8. K

  Koba JF-Expert Member

  #8
  Nov 14, 2008
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  .....tatizo ni politiki za umeme Tanzania na Pinda naye anaongea kama mtu asiyejua kitu au ni kweli haelewi kitu ambacho ni hatari sana,na humu ndani ya JF wengi wenu ni makelele tuu na hamna idea na wala hamchukui muda kufanya research kidogo na ninakumbuka wengi humu mlikuwa staunch supporter wa wabunge waliokataa muswada mpya wa umeme halafu leo mnajiuliza kwa nini hatuna umeme? TZ kuna gas kibao ambayo ingeweza kuzalisha umeme na kubaki ziada,wananchi dont deserve this na hii ni kwa sababu moja tuu ya ukilaza na siasa chafu za watu wasiojua kitu....tatizo la kukosa umeme,migawo,rushwa na kutapeliwa kwenye sekta ya umeme ni moja tuu na mchawi ni sheria zilizopo na bila kuzibadili tusitegemee chochote,lakini at least JK alijaribu lakini wabunge kwa kutaka misifa au kutokuelewa basi wakaipiga chini bill yote,inasikitisha sana!
   
 9. M

  Mama JF-Expert Member

  #9
  Nov 14, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Kuna Stieglers Gorge mto Rufiji yenye uwezo wa kutoa hadi 1000 MW; kiwango hiki cha umeme kingekidhi mahitaji ya Tanzania na ziada. Nilikuwa na habari kuwa World bank walikuwa tayari kuu-fund mradi huu kwa masharti with prerequisite ya kujenga miundombinu ya kutosha kuiwezesha serikali kuuza umeme wa ziada huu nje ya nchi. Pamoja na vikwazo toka kwa wanamazingira, sijui hii plan iliishia wapi. Umeme wa maji ni rahisi kuufua, gharama yake kubwa ni kwenye ujenzi wa hizo turbines na mazagazaga yake. Afterwards n maintanance tu. Tanzania ingesahau tatizo la umeme.
   
 10. YournameisMINE

  YournameisMINE JF-Expert Member

  #10
  Nov 14, 2008
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 2,451
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 145
  hivi kukiwa na umeme sasa wale mafundi wa sido wa vibatari (wakina joe the plumber wa kibongo) wakale wapi? acheni nyinyi maneno yenu.........kukosekana kwa umeme ni industry flani na kupatikana kwake kunapunguza ajira!!

  hizo ni two cents zangu, in a nutshell.....
   
 11. YournameisMINE

  YournameisMINE JF-Expert Member

  #11
  Nov 14, 2008
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 2,451
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 145
  ubovu wenyewe hujui Rev. Kishoka anasimamia nini!! ungekuwa unajua, usinge thubutu kumfagilia kwa kuweka hiyo quotation ya Malcom X wa Dudley.......
   
 12. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #12
  Nov 14, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Duuuh, yani we umeona ile quote ya Malcom pale inamfagilia ? Hebu pitia tena posti nzima.

  Trust me, mwenyewe kaelewa!
   
 13. YournameisMINE

  YournameisMINE JF-Expert Member

  #13
  Nov 14, 2008
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 2,451
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 145
  unajisahau sana! nimeangalia post nzima na hiyo ni take yangu..upo hapo? suala si mwenyewe kuelewa, suala ni sisi adhila tunaonaje..........ukifuatilia thread za Rev. Kishoka ua zianaishia hewani, si mfuatiliaji na kwa maana hiyo ni mzushi flani tu anayependa kuja na mada mpya kila apatapo nafasi baada ya kunywa mvinyo wa dezo wa kanisa.

  maneno mingi tu...
   
 14. M

  Mama JF-Expert Member

  #14
  Nov 14, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  wale mafundi vibatari wataupgrade na kuuza zaidi. Wataanza kutengeneza majeri ken ya kumwagilia badala ya kutengeneza vibatari; hii itawaongezea kipato kwani jeri keni moja bei yake ni juu kuliko ya kibatari. Kumbuka unaweza kukaa na kibatari miaka mitano bila kununua kingine (kinawekwa pale kumulika tu-hakipati mikiki). Hata hivyo umeme utawasaidia kufanya kazi kwa urahisi na kutoa products zenye ubora utakaokidhi masoko nje ya nchi.
   
 15. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #15
  Nov 14, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Tatizo lenu ni kuogopa kufikiria na kushupalia udaku usio na nguvu! Mtu kutoa maoni yake kwa upeo wake wa kufikiria na kupima mambo mnaona mzushi!

  Lakini mkiambiwa Manji ana kaswende, hamchelewi kujaza kurasa mia kuuliza alipataje kaswende, mara ana wanawake 10, mara laana ya kutumia Quran kwenye tiketi za Yanga, sijui kaiba EPA, mdogo wake ni mchumba wa Ridhiwani, ananyumba Makambako jirani na Sumaye na utitiri mwingi.

  Vitu relevant ambavyo ndivyo mnapaswa kuvipima na kuvipigia kelele si kukosoa tuu hata kutoa tathmini au alternative hamna.

  Yes Mchungaji ni Mzushi, huanzisha mada mpya ambazo hazina muelekeo lakini kama kawaida yenu mtarudi kuzikumbuka miaka ya baadaye.

  Umesahau aliyeanzisha Kagoda, Meremeta, Richmond na nyinginewe ambazo mlizipuuzia unyasi ulipotikisika mkazubaa mpaka mkang'atwa ndipo mkaamka kwa ghadhabu?

  Mimi si Malaika kama Kuhani anavyonipiga dongo, kuna tunayokubaliana na tusiyokubaliana. Kuhani kaona kauli zangu zina utata si mara ya kwanza, yeye ni mtaalamu, mkutubi wa kukumbusha kauli zilizotoka awali.

  Weye shangilia ushindi wa Obama na naomba nisaidie kumwambia Nyani Ngabu anitumie Kavwasiye yangu, siku ya kuingia utumwani na kuuza uhuru (Thanksgiving) inakuja, baada ya shibe shurti uteremshie na maji yaliyochachuka!
   
 16. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #16
  Nov 14, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mama,

  You are talking the right talk, progressive thinking and not a defeated and cowardly soul.
   
 17. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #17
  Nov 14, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Nimejisahau vipi sasa?

  Kishoka hana spine ya kuchukua msimamo katika kutukana watu weusi. Siku ya ushindi wa Obama alipiga tarumbeta la hadhi ya watu weusi. Akakandya misemo ya ndivyo walivyo. Lakini akikaa kidogo ana flip, anaanza kukejeli race nyeusi kama walivyofanya ma "devil" wa miaka ya Civil Rights era. Ndio Malcom anasema ni bora Ku Klux Klan maana msimamo wao unajulikana, kuliko hawa wanaokuja kama Malaika.

  Na kilicho repugnant zaidi ni kwamba, sio tu hawezi kuchukua msimamo, ila pia akianza kutukana watu weusi huwa hawezi kuongea mwenyewe mpaka atumie mgongo wa mtu mwingine. Hana backbone yake mwenyewe, ama balls, ama vyote. Ooooh fulani anasema ndivyo tulivyo, ooooh anavyosema inawezekana ni kweli. Siku nyingine anaiweka kama ni swali hivi, "je ni kweli," lakini wakati mwingine akipandwa na mukari wa ajabu anatukana bila simile za "inawezekana ni kweli."

  Ndio maana ni bora yule anaekwambia yuko upande gani, hata kama yuko wrong.
   
 18. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #18
  Nov 14, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  YNIM,

  Do not mess with Zohan my friend! nenda katengeneze vibatari kwa Mjomba bichwa kubwa, is he still kicking?:p
   
 19. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #19
  Nov 14, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Amini uaminilo Kaka, kama sina uti wa mgongo, basi nateleza kama nyoka, mithili ya Kuhani alivyo! Chukua kioo ujiangalie! kwi kwi kwi!
   
 20. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #20
  Nov 14, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Kuhani,

  On a serious note though, hivi umeona kuwa natumia mgongo wa Nyani kutukana Watanzania na kuona sina kende kutukana kwa mdomo wangu mwenyewe?

  Si wewe uliyeshangilia nilipomsiliba FMES kwenye hoja moja mpaka ukatoa tuzo ya Mtu mwenye Makende ya Chuma?

  Umepitia Screw Muungwana? Je CCM adui wa Maendeleo nako huko nimekosa mfupa?

  Sasa kwenye hili la Nishati na kutumia maneno ya Nyani "Ndivyo Tulivyo" nimekosea nini kueleza ukweli kuwa Serikali yetu na watendaji wake ni wavivu wa kufikiri, kupanga mambo na kuingia gharama?

  Wewe ni mchumi, tupe basi zako nasaha kuwa tufanyeje zaidi ya kupembua utata wa tungo zangu au wasifu wangu.
   
Loading...