Waziri wa Nishati toka hadharani utueleze kulikoni matatizo ya umeme

koryo1952

JF-Expert Member
Mar 7, 2023
382
764
Mhe. Waziri wa Nishati ulituaminisha kuwa katika muda wa wiki mbili kutakuwa na afadhali kidogo kuhusu upatikanaji wa umeme.

Pili ulitueleza kuwa kutokana na ukame ndiyo maana upatikanaji wa umeme umekuwa ni shida LAKINI mvua zimeanza kunyesha kwa wingi sana na mito na mabwawa yamejaa maji mbona Mhe. Waziri bado kuna matatizo makubwa ya upatikanaji wa umeme?

Mfano hai leo tarehe 16 Novemba, 2023 maeneo mengi hapa Jiji la Mwanza hapakuwa na umeme tangu asubuhi na umeme umerudi saa 11.30 jioni.

Tunakuomba utoke hadharani kupitia luninga na uwaeleze wananchi kulikoni matatizo ya umeme wakati mvua zinanyesha na mito na mabwawa yamejaa maji.
 
Back
Top Bottom