Kama umefuatilia mkutano wa Membe na waandishi wa habari leo utagundua kuwa mheshimiwa Membe hayuko tayari kumuunga mkono mheshimiwa Lissu kwenye kiti cha urais.
Ikumbukwe kwamba kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo mhe. Zitto Kabwe na mwenyekiti wake mhe. Maalim Seif S. Hamad wameshatangaza waziwazi kwamba wanamuunga mkono na watampigia kura mgombea wa CHADEMA mhe. Lissu kwa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na inavyoonekana mheshimwa Membe atakuwa keshafanya vikao na viongozi wake wakuu wa chama na kuwakatalia kwamba hatamuunga mkono mhe. Lissu
Ninachokiona ni kwamba mheshimiwa Membe ana uchu sana na madaraka au anataka kugawa kura za upinzani hata baada ya kukosa mvuto kwa wananchi lakini bado anang'ang'ania kwamba ataiangusha CCM katika uchaguzi huu kitu ambacho ni ndoto za mchana.
Sasa ni dhahiri kuwa ACT hawakupiga hesabu zao vizuri walipompokea mheshimiwa Membe, walidhani angekuwa Asset lakini sasa amekuwa Liability!