Umbea Umemtoka Dk.slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umbea Umemtoka Dk.slaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Antsadism, Jul 1, 2008.

 1. A

  Antsadism Member

  #1
  Jul 1, 2008
  Joined: Mar 22, 2008
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MBEA UMEMTOKA DK.SLAA
  Pamoja na kutaka kuwapotosha Watanzania kuwa fedha zilizochotwa isivyo halali na makampuni 22 kutoka mfuko wa madeni ya nje (EPA) katika benki kuu ya Tanzania (BoT) ni za serikali, mbunge wa karatu mkoani manyara (CHADEMA) Dr. Wilbroad Peter Slaa wiki hii ameumbuka katika mkutano wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania unaoendelea mjini Dodoma.

  Dr. Slaa mwanasiasa alieukimbia upadri wa kanisa katoliki aliumbuliwa bungeni na waziri wa fedha, MUSTAFA HAID MKULO aliyesisitiza kuwa kauli yake kuhusu fedha hizo kwamba sio za serikali iko palepale na ndio inayosema ukweli.

  Mbunge huyo wa karatu ambaye pia ni katibu mkuu wa chadema aliumbuliwa pia na mbunge wa mtera mkoani Dodoma (CCM) mzee John Samuel Malecela kuhusu ni nani hasa aliyeanzisha hoja inayohusu fedha hizo bungeni kati ya Dr. Slaa na wabunge wa chama cha mapinduzi.

  Kimsingi hoja hiyo ilianzishwa na mbunge wa Busega mkoani Mwanza (CCM) Dr. Rafael Masunga Chengeni na “Kudakwa kichwa kichwa” na Dr. Slaa akidhani ingemsaidia kisiasa au chama chake, lakini mambo yanazidi kwenda ndivyo sivyo.

  Namshauri Dr. Slaa aachane na “Umbeya” afanye siasa za kweli kama wanavyofanya wenzake akiwemo mwenyekiti wa taifa wa UDP John Momose Cheyo ambaye ni mbunge wa Bariadi Mashariki mkoani Shinyanga.

  Akionyesha kutokua mnafiki Cheyo ndiye mbunge pekee kutoka kambi ya upinzani aliyeunga mkono bajeti ya serikali ya mwaka 2008/2009 na kutoa ufafanuzi yakinifu kuhusu msimamo wake huo usioyumba na hata kuyumbishwa na wanasiasa “Ucheara” kama Dr. Slaa.

  Pamoja na mambo mengine, Cheyo alisema ameiunga mkono bajeti hiyo kutokana na ukaweli kwamba serikali ya CCM imeonyesha usikivu mkubwa, inashurika na inajitahidi kufanya marekebisho takribabani kila iliporuhusiwa vinginevyo na kamati ya bunge ya hesabu za serikali ambayo mbunge huyo wa bariadi mashariki ndiye mwenyekiti wake.

  Hakika Dr. Slaa hatimaye “Umbea” umemtoka na kama ni mtu wa kujifunza basi amepata fundisho litakalomsaidia huko mbele.
   
 2. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mzee hujatulia, inabidi upepewe na kuombewa ili mapepo ya ufisadi yatoke. Sisi hatujali nani kaleta sisi tunajali mali ya taifa.

  Ushindwe na ulegee kabisa.

  Aamen
   
 3. H

  Haika JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  sasa alieanzisha hoja ndio mshindi?
  mshindi ni yule atakaeleta ufumbuzi wa kweli.
  IN ANY CASE CCM NDIO WALIOANZISHA HII HOJA KWA KUPORAMALI NA HIZO WA WATANZANIA NA KUFICHA TAARIFA HADI WATU WENYE HASIRA ZAO WALIPOANZA KUZIRUSHA KWENYE MTANDAO.
   
 4. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kwa waliopo Tanzania, wasome KULIKONI la LEO, makala ya 'Kona ya Hoja' ya Nyaronyo Kicheere ukurasa wa saba. Nyarongo amemwambia Mzindakaya 'sharaaaap' akiwa na maana anamwambia "shut up"... na wewe antsadism nakwambia sharaaap!!! Watanzania wa leo huwawezi!!! Tena huko kijijini seuse humu JF!!???
   
 5. Mchola

  Mchola Member

  #5
  Jul 1, 2008
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi wewe Antisadism, una chuki binafsi na Dr Slaa au wewe una ubia na mafisadi? Naomba jibu
   
 6. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Punguza ugimbi wa ufisadi, unadhani ni mtanzania gani wa leo ambaye hajui kinacho endelea?

  Hata wanao fanya kazi ya kuspin they are a bit smarter than you!, Nenda walau kwa wenzio wakupige msasa kwanza!
   
 7. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2008
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Your days are numbered!
   
 8. M

  Msesewe Senior Member

  #8
  Jul 1, 2008
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo nayeeeee!!!!! Pashkuna sijui katumwa? mtu mwenyewe hata haelewi anachokisema
   
 9. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  mfa maji haishi kutapatapa ... aibu unaigeuza hasira ... unalo babuuu wee umeshaumbuka ... mwache aseme kwani hayo kama unayaona pumba kwetu yanamaana
   
 10. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Huyu Naye Katutokea Wapi Huy? Bila Shaka Ni Mtoto Wa Malecela, Au Chenge, You Are In The Wrong Truck
   
 11. emedichi

  emedichi Member

  #11
  Jul 1, 2008
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 46
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Baba mdogo jipange upya, naona unangata meno tu. Waliokutuma wamechemka. You are not smart enough to convey what they want. Unatetea hoja yako kwa kuingia kwenye maisha ya mtu. Kuacha upadri kwa Slaa kUNA UHUSIANO GANI NA UNACHOKISEMA.
   
 12. H

  Haika JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  watu wako siriazi hapa unaleta chuki binafsi!
  lazima una matatizo makubwa.
  ina maana wewe unawachukia watu, inabidi uchukie na kukemea matendo yao mabovu,
  hapa tukoo kwenye swala la ufisadi, mtu anayeongoza kwa kuupiga vita badala ya kusapoti issue, unaletamambo nje ya pointi.
  Sasa watu wangeanza hapa kuchambua mambo binafsi ya hawa mawaziri wenye kashfa, hapa si pasingetosha?
  hebu zikumbuke kwa uchache tu, ni chafu na nyingi mno! Lakini watu hapa hawaziangalii hizo wanaangalia mustakabali wa taifa
   
 13. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #13
  Jul 1, 2008
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Antsadism kama unaweza kutuma thread kama hii na wakati kama huu, hunipi kazi sana kukujua udogo wa ustaarabu wako hasa ukiwa maliwato (yaelekea huwa hutumii maji hata ile karatasi)
   
 14. m

  mibavu Member

  #14
  Jul 1, 2008
  Joined: Dec 11, 2007
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani msimshambulie sana hapa inavyoonekana yeye na wao lao moja tumsaidieni ili aelewe anacho kisema (kama mkulo anasema pesa ni zawanya biashara sawa tuna kubali je huyo bwana atupe jibu ukihifadhi pesa benki halafu zikazaibiwa zilizo ibiwa zi zakwako au za benki) ndio maana tuna sema pesa zilizo ibiwa ni za uma kwa sababu bot niya uma
   
 15. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #15
  Jul 1, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hata mafisadi wana wafuasi wao, hivyo huu ni muendelezo wa kifisadi tuu.

  Hakuna haja ya kujadili kitu kama hiki kwani kinatupotezea wakati.
   
 16. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #16
  Jul 1, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  SADISM, What a name, jina lenyewe ni la kukodi. Sembuse mawazo yako. Chini kumekuwa na akili kuliko kichwa.
   
 17. M

  Maskini Mimi Member

  #17
  Jul 1, 2008
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Slaa akiwa mkatoliki au whatever, sisi tunataka kuangalia mtu yoyote anayeweza kuturejeshea hali nzuri katika nchi yetu ili waTZ wafaidike na matunda ya nchi yetu.

  Slaa keep going and you will come out with flying colours!
   
 18. lidoda

  lidoda JF-Expert Member

  #18
  Jul 1, 2008
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 80
  we mbona unakera na kutupotezea mda wetu kwa kusoma huu utumbo wako?? Nafikiri hata ktk magazeti ya udaku wasingekukopesha namna hii.,
   
 19. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #19
  Jul 1, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Ant una haki ya kusema lolote unalotaka. Hiyo ndiyo domokrasia yako. Maana mdomo nimali yako. Lakini hapa tu hata jk akisoma makala yako hii na wewe kama ni mtu wa system atakushangaa sana.
  Ukweli unabaki wazi na uongo unajitenga.
  Pole sana maana bado Slaa ni mkweli na ni shujaa wa nyakati hizi ambaye vitabu vya historia ya Tanzania havitabaki kumsahau.
   
 20. B

  BeNoir Member

  #20
  Jul 1, 2008
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Antsadism, naomba kujua kutoka kwako ni nini maana au tafsiri ya "UMBEA"? Na ukiwa umemtoka mtu anakuwaje?
   
Loading...