Serikali: Hakuna mtu yeyote Tanzania aliyekamatwa au atakuja kukamatwa sababu ya kuikosoa serikali

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Serikali, kupitia Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye imetoa tamko juu ya matamko yanayotolewa na asasi mbalimbali kuhusu kukamatwa kwa Dr. Slaa, Wakili Mwabukusi, na Mdude.

Katika maelezo hayo imeeleza kuwa hakuna Mtanzania aliyekamatwa au atakuja kukamatwa Tanzania sababu ya kukosoa serikali katika jambo lolote lile ikiwemo hili la bandari linalovuma sasa.

Pia imeelezwa kuwa, kukamatwa kwa akina Dr. Slaa hakuminyi kwa vyovyote vile uhuru wa kujieleza Tanzania, ila ni katika kutekeleza sheria na kuzuia machafuko ambayo yanaweza kutokea baada ya wito wa uasi dhidi ya serikali iliyochaguliwa kidemokrasia.

Pia soma: Tamko la Serikali kuhusu Kukamatwa kwa Dkt. Slaa, Mdude, Wakili Mwabukusi
 
Mliowakamata walikosoa serikali mmewabambikiza kesi
Waachieni basi
Hii kesi itawaacha uchi
Iko hivi
Hatunyamazi
Tunataka Bandari zetu Mbuga zetu Maziwa Misitu NA UHURU WETU
UTARUDI HUKU TULIKO SIKU MOJA weh haya
 
Halafu eti usikamatwe wewe umekuwa nani?
 
Kukosoa mbona huwa tunakosoa muda wote but they went too far na kupanga njama za kumwaga damu ya Watanzania
 
Serikali, kupitia Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye imetoa tamko juu ya matamko yanayotolewa na asasi mbalimbali kuhusu kukamatwa kwa Dr. Slaa, Wakili Mwabukusi, na Mdude.

Katika maelezo hayo imeeleza kuwa hakuna Mtanzania aliyekamatwa au atakuja kukamatwa Tanzania sababu ya kukosoa serikali katika jambo lolote lile ikiwemo hili la bandari linalovuma sasa.

Pia imeelezwa kuwa, kukamatwa kwa akina Dr. Slaa hakuminyi kwa vyovyote vile uhuru wa kujieleza Tanzania, ila ni katika kutekeleza sheria na kuzuia machafuko ambayo yanaweza kutokea baada ya wito wa uasi dhidi ya serikali iliyochaguliwa kidemokrasia.

Pia soma: Tamko la Serikali kuhusu Kukamatwa kwa Dkt. Slaa, Mdude, Wakili Mwabukusi
Mbona tumeona mnakamata kamata watu?
 
Wana Arsenal mmeigundua mahali au traditional weapons store Iko mahali na kikundi tayari Kiko Trained Kwa ajili ya kufanya hayo matukio ya kumwaga damu?
Na kama watanzania wote wamekubaliana na wameelewa kuhusu IGA na wote wanaunga mkono kama inavyodhaniwa, je watu Hawa watatu wana capacity Gani ya kuleta machafuko nchi nzima at once washindwe kudhibitiwa? Mtaweza kuieleza mahakama nani alipangwa kuchukua madaraka ya urais?
Mnatia kinyaa na aibu ndani na kimataifa.
 
Kukosoa mbona huwa tunakosoa muda wote but they went too far na kupanga njama za kumwaga damu ya Watanzania
Huo ushahidi unao?

Mbona unageuka mwanasesere usiyejielewa, kuendelea kuitumia clip isiyozidi sekunde kumi kuaminisha umma kwamba Dr. Slaa alitaka kuipindua serikali ni utoto.

Lini na wapi alitamka hayo maneno? walikuwepo wakina nani wakamsikiliza? au kama ni kwenye hiyo video ndipo akatamka, iweje waliofikiwa na hiyo video muwe nyie pekee wenye nia ovu dhidi yake? kwanini tusiamini mmeitengeneza kwa makusudi ili mumfunge mdomo?

Naamini hayo maswali hapo juu yamekuzidi kimo.
 
Huo ushahidi unao?

Mbona unageuka mwanasesere usiyejielewa, kuendelea kuitumia clip isiyozidi sekunde kumi kuaminisha umma kwamba Dr. Slaa alitaka kuipindua serikali ni utoto.

Lini na wapi alitamka hayo maneno? walukuwepo wakina nani wakamsikiliza? au kama ni kwenye hiyo video ndipo akatamka, iweje waliofikiwa na hiyo video muwe nyie pekee wenye nia ovu dhidi yake? kwanini tusiamini mmeitengeneza makusudi ili mumfunge mdomo?
Kuna nyingine hii hapa
 
Waoga hao, wadau wa maendeleo waliotoa misaada yenye masharti tayari wanaibana serikali kwa kukengeuka kuhusu haki za binadamu huku walishasaini maazimio kibao kule Geneva kwamba wataacha udiktekta.



TOKA MAKTABA
Mambo ambayo utawala wa awamu ya sita kwa kiasi kikubwa wamejaribu kuyarekebisha ni pamoja na kuonesha inataka kufungua ukurasa mpya :

Toka Geneva
23 March 2022

Awamu ya 6 ya serikali ya CCM, mmesaini mikataba mingi ya kukubali kufungua milango ya demokrasia, uhuru, haki ya kukusanyika n.k bila kusahau katiba yetu inaruhusu shughulu za kisiasa. Sasa huku kubabaika kunatoka wapi

NGOJA TUKUMBUSHANE
Watendaji wenye dhamana Serikalini na vyombo vyake ikiwemo taasisi, idara zake zifahamu kuwa mwaka huu 2022 huko Uswisi (Switzerland) waziri wa Sheria na Katiba Mh. George Simbachawene mbele ya Umoja wa Mataifa katika Kamisheni ya Umoja wa Mataifa Kuhusu Haki za Binadamu kuwa Tanzania iliridhia kuacha kuandamiza na kubinya haki za msingi nyingi ikiwemo hili la wananchi kuwa na haki ya kuishi , haki ya kujadili, haki mbele ya vyombo vya haki jinai, kushauri na kuelekeza nchi yao iende vipi.

23 March 2022
Geneva, Switzerland

Mikataba 252 ambayo Tanzania iliridhia na inayogusa haki zote ikiwemo UWAZI ni kama ifuatayo



Video : Mh. George Simbachawene akihutubia UMoja wa Mataifa kuhusu haki haki
na kuuhakikishia ulimwengu kuwa haki zote ktk awamu ya 6 zinazingatiwa



Tanzania yaridhia haki ya wananchi kushirikishwa katika ngazi zote, kujadili mustakhabali wa nchi yao, haki ya jumuika, haki ya kuzungumza, wananchi kuwa na haki ya kuwaambia watawala nini wakifanye, uhuru wa habari, kufunguliwa vya vyombo vya online pia magazeti, imeridhia mikutano ya vyama vya siasa kufanyika, , ....

GEORGE B. SIMBACHAWENE, Minister of Constitutional and Legal Affairs of Tanzania, said Tanzania was a strong proponent of the Universal Periodic Review mechanism which brought together State actors, civil society and development partners. As the Government pursued the goal of realisation of human rights for all Tanzanians, the recommendations were given the highest consideration. All 252 recommendations were disseminated to State and non-State actors, including the National Human Rights Institution as well as civil society, in both mainland Tanzania and Zanzibar. As a result of broad-based consultations, Tanzania had accepted to implement 167 recommendations, which were in compliance with the Constitution of the United Republic of Tanzania and the Constitution of Zanzibar.

The recommendations aligned with policies, laws and programmes which called for the promotion and protection of civil, political, economic, social and cultural rights, emerging human rights issues, anti-corruption efforts, environmental conservation and development priorities of Tanzania. The Government affirmed its commitment to implementing all the accepted recommendations, which had been deemed strategic and effective interventions for the promotion and protection of human rights. 65 recommendations had been noted; those were recommendations that were not in alignment with the Constitutions, policies, laws, traditions, beliefs and culture of Tanzania, or which required further consultations before making a conclusive decision. The Government strived to ensure that all Tanzanians were provided with equal civil, political, economic, social and cultural human rights.

Discussion

Speakers applauded the Government of Tanzania for progress made in strengthening its institutional frameworks for the promotion and protection of rights and fundamental freedoms. Strides had been made in the area of social development, including the introduction of fee-free primary education and remote learning during the COVID-19 pandemic. Speakers further commended Tanzania on the establishment of the National Commission for Human Rights, which was in accordance with the Paris Principles. Speakers noted steps taken to curb child labour, as well as the measures taken by the Government toward ensuring freedom of expression and the right to information, which included entering into dialogue with media practitioners and amending some pieces of legislation. Tanzania’s acceptance of close to 75 percent of the recommendations showed real commitment to further promoting and protect the rights of all persons on its territory. The acceptance of recommendations prioritised expenditures in health including specialised care and services for people living with albinism, as well as scaling up investment in education.

Other speakers took note of the challenges faced by Tanzania in implementing some of its human rights obligations under Article 12(3) of the African Charter which recognized the right to seek and obtain asylum in other countries, as well as the 1951 Convention relating to the Status of Refugees. Speakers regretted that Tanzania did not receive any recommendations on the rights of sex workers, urging the Government to repeal the Penal Code provisions criminalising acts associated with sex work, place a moratorium on the arrest and harassment of sex workers under vagrancy laws, and revise and harmonise national legislation in line with regional and international human rights instruments. Tanzanian authorities continued to weaponise the law to target the opposition and critical voices, using non-bailable offence provisions under the Criminal Procedure Act to detain people for unreasonable periods of time. The State should ensure accountability for election-related human rights violations and guarantee post-election human rights reforms to reverse the Government’s increasing repression and crackdown on civic space.

The Vice-President of the Council informed that out of 252 recommendations received, 167 enjoyed the support of Tanzania, while 65 had been noted. Additional clarification was provided on 20 recommendations, indicating which parts of the recommendations were supported and which parts were noted

Concluding Remarks

GEORGE B. SIMBACHAWENE, Minister of Constitutional and Legal Affairs of Tanzania, said Tanzania continued to accord great significance to the Universal Periodic Review, as it played a key role in the promotion and protection of human rights in the country. Tanzania was committed to implementing the accepted recommendations, as they would have a direct impact on the realisation of human rights and sustainable development of the country. The Universal Periodic Review was a continuous process, and the Government would continue to address the remaining challenges through dialogue, in collaboration with all stakeholders. It would also continue to strengthen its internal mechanisms and promote engagement with all non-State actors and development partners. The Government, under the stewardship of Tanzania’s first female President, would meet the aspirations and objectives of the Universal Periodic Review mechanism during the coming fourth cycle.



Link: Conseil des droits de l’homme : Examen périodique

https://www.ungeneva.org › 2022/03
Human Rights Council Adopts Outcomes of Universal Periodic ...

23 Mar 2022 — 23 March 2022 Meeting Summaries. The Human Rights Council in a midday meeting adopted the outcomes of the Universal Periodic ....
 
Umezitoa wapi hizi? unatakiwa kujibu maswali yangu badala ya kuendelea kunitumia vipande vya video, mlivyotengeneza studio na wajinga wenzako.
Clip yenye maneno yasiyozidi hata 20 aisee! Inatia shaka
Unaenda kwa nani
Jukumu la nani
Afanye nini, wapi, lini na kwa njia gani...
 
Back
Top Bottom