Umasikini wa Watanzania chanzo chake ni kupenda kujenga nyumba ya kuishi kwanza badala ya kuanzisha biashara

Kizuri kichukue kibaya achana nacho. Wahindi ni katika watu wenye mafanikio makubwa katika kurithisha watoto wao mali zao tena na tena. Ni kwa sababu wanajua jinsi ya kuitumia pesa kuongeza ziwe zaidi bila anasa. Somo hilo litakufaa wewe na hata wanaokuja baada yako
Mleta mada anazungumzia kujenga nyumba. Stick to the point.
 
Mnaosema kwamba kujenga sio priority nawashangaa. Imagine umepanga nyumba for 10 years huku unafanya biashara. Ghafla umefariki umeacha watoto wa form one na form two kwenye nyumba ya kupanga, hawajui ABC za biashara na mama yao labda hana uwezo au hajabarikiwa karama ya kufanya biashara. Wale watoto unawaacha kwenye hali gani. Watanzania msikubali kudanganywa. Watu wanaowaambia msijenge wamenyoosha miguu kwenye nyumba walizoachiwa na marehemu baba zao. Jipangeni upya tafuteni akiba isiyohamishika. I rest my case
 
Kujenga ni neema, wapo wenye pesa nyingi na hawajajenga na wala hawajawekeza wakipata hela ni starehe tu zikiisha ndio anajuta, hao waindi wengi hawajengi maana huku si kwao, kwa mtanzamo wangu mtu akiwa na uwezo wa kujenga ajenge awe na kwake , pia anaepuka kero za nyumba za kupanga.
 
Mkuu nipo tofauti na ww kimtazamo kwa hoja zifuatazo.
Kwanza kuna mahitaji muhimu makuu matatu ya mwanadamu:
1.Chakula
2.Mavazi
3.Malazi
Ukiacha mahitaji mawili tajwa hapo juu hilo hitaji la tatu MALAZI ni hitaji muhimu sana kwa mwanadamu yoyote. na tunapoongelea MALAZI hatuongelei KITANDA tunaongelea sehemu ambayo mwanadamu anaweza kujihifadhi katika hali zote na apo tunaongelea NYUMBA.
Usipokua na nyumba ww bado ni MASKINI NA MKIMBIZI USIYE NA MAKAZI MAALUMU NA BADO hujakava mahitaji yako muhimu.
Huna pako na mwenye nyumba anaweza kukufukuza muda wowote anaotaka na kukuaibisha kwa sababu ww ni MKIMBIZI NA HUNA PAKO. Ukiugua, kazi ukafukuzwa, biashara zikayumba ukawa huna hela mfukoni mwenye nyumba atakufukuza kama mbwa koko na kukunyang'anya vyombo vyako mali zako na kubaki maskini zaidi na zaid. Utatanganga tanga bila stahaa na watoto na mke wako.
Kwnye context ya uchumi kuna ASSETS NA LIABILITIES. nakubali kweli nyumba ya kuishi ni Liability lakini kuna kitu Tunakisahau nacho ni WELFARE.
WELFARE ni hadhi ya maisha ambacho ni kitu muhimu sana kwenye maisha.
Kama umepanga ww hadhi yako ya maisha still ipo poor.
Mf: Kuna sehemu nilipanga mwenye nyumba hataki wageni waje kwangu eti choo kinajaa. Daah niliumia sana na nikahama ndo maana napambana usiku na mchana nimalizie site yangu nihamie. Sipendi fedheha za nama hii.
Kua kwako kuna raha sana acha tuu..

WATANZANIA TUJENGE NYUMBA BORA KWA MAENDELEO YETU, NYUMBA NI MAISHA JAMANI. HATA MAISHA YAKITETELEKA NYUMBA ITAKUSITIRI SANA. UNAKULA ZAKO MCHICHA UNALALA. LAKIN KOSA KODI UTAJUA NINACHOKIONGEA HAPA KAMA CHA MAANA AU CHA KIPUUZI.
 
Hata mtu mzima kabisa anakosea ktk baadhi ya matendo yake

lakini kukosea kwake hakumaanishi kua anachokifanya yupo sahihi

ukiwa kama mtoto unaetaka kufika mahali,yapasa ujue kuchuja mazuri na mabaya

chukua mazuri acha mabaya,songa mbele Wahindi wana mazuri mengi ila hilo la kupanga HAPANA.
Mentor wangu kaongea mimi nani nibishe.
Wazungu tunaofanya kazi nao wakisikia umejenga wanashangaa.Hii ni kwasababu sheria za ujenzi kwao kwa mtu individual ni ngumu wengi wananunua kwa hao wanaofanya biashara za real estate.
Tanzania nyumba nyingi za kupanga kwa kwa mtu mwenye kipato cha kawaida ni mbaya hazikidhi.Na ambazo ni nzuri ziko nje ya mji.
 
Hiyo inaitwa nina kwangu na kausafiri kangu. Mungu anipe nini? Anipe donda?
Maisha ndio hayo hayo, mambo mengine ni maboresho tu.

Hivi unafikiri jina Elon Musk hawaishi, kwamba wanasubiria mpaka wakienda Mars ??
 
Mkuu Siku zote maisha huwa hayana formula, unaweza ukamuiga muhindi nawewe ukaacha kujenga,, hako ka hela ukakasukumia kwenye biashara kakafia hukohuko ukakosa vyote,, mwisho wa siku mwenye pango lake akakutimua. Fanya kile unachoona kinafaa kwenye maisha yako, Acha kuiga. Unaweza ukakuta huyo huyo muhindi wako amepanga kumbe Kule kwao ameacha mijengo yake na yeye amepangisha, kila mwezi anatumiwa kodi ndio maana unamuona hateteleki. Au Kule kwao ana miradi na mingine huwa wanamtumia pesa, ndio maana hateteleki. Sasa wewe iga tu kama haujajipanga au hauna hata plan b, utacheza segere pale biashara yako itakapokuwa mochwari na mwenye nyumba anataka chake, wakati huo watoto wanataka ada.
 
Mkuu nipo tofauti na ww kimtazamo kwa hoja zifuatazo.
Kwanza kuna mahitaji muhimu makuu matatu ya mwanadamu:
1.Chakula
2.Mavazi
3.Malazi
Ukiacha mahitaji mawili tajwa hapo juu hilo hitaji la tatu MALAZI ni hitaji muhimu sana kwa mwanadamu yoyote. na tunapoongelea MALAZI hatuongelei KITANDA tunaongelea sehemu ambayo mwanadamu anaweza kujihifadhi katika hali zote na apo tunaongelea NYUMBA.
Usipokua na nyumba ww bado ni MASKINI NA MKIMBIZI USIYE NA MAKAZI MAALUMU NA BADO hujakava mahitaji yako muhimu.
Huna pako na mwenye nyumba anaweza kukufukuza muda wowote anaotaka na kukuaibisha kwa sababu ww ni MKIMBIZI NA HUNA PAKO. Ukiugua, kazi ukafukuzwa, biashara zikayumba ukawa huna hela mfukoni mwenye nyumba atakufukuza kama mbwa koko na kukunyang'anya vyombo vyako mali zako na kubaki maskini zaidi na zaid. Utatanganga tanga bila stahaa na watoto na mke wako.
Kwnye context ya uchumi kuna ASSETS NA LIABILITIES. nakubali kweli nyumba ya kuishi ni Liability lakini kuna kitu Tunakisahau nacho ni WELFARE.
WELFARE ni hadhi ya maisha ambacho ni kitu muhimu sana kwenye maisha.
Kama umepanga ww hadhi yako ya maisha still ipo poor.
Mf: Kuna sehemu nilipanga mwenye nyumba hataki wageni waje kwangu eti choo kinajaa. Daah niliumia sana na nikahama ndo maana napambana usiku na mchana nimalizie site yangu nihamie. Sipendi fedheha za nama hii.
Kua kwako kuna raha sana acha tuu..

WATANZANIA TUJENGE NYUMBA BORA KWA MAENDELEO YETU, NYUMBA NI MAISHA JAMANI. HATA MAISHA YAKITETELEKA NYUMBA ITAKUSITIRI SANA. UNAKULA ZAKO MCHICHA UNALALA. LAKIN KOSA KODI UTAJUA NINACHOKIONGEA HAPA KAMA CHA MAANA AU CHA KIPUUZI.
Kweli mkuu kama mm tarehe ishirini anavuta cash inaniuma hatari
 
Hakuna watu wanapenda kujenga nyumba za kuishi duniani kama Watanzania.

Ndoto kuu ya kwanza ya Mtanzania yeyote ngozi nyeusi ni kuwa na kwake hivyo akipenda vihela huvipeleka site kujenga nyumba ya kuishi hapa ndio siri ya umasikini wa Watanzania ngozi nyeusi kuanzia.

Wenzetu Wahindi hupanga hata miaka arobaini pesa zake akiweka na kukuza biashara yake. Wazo lake la kwanza huwa nikipata pesa natafuta nyumba ya bei rahisi ya kupanga halafu hela inayobaki naanzisha biashara. Wote mashahidi Wahindi matajiri hasa lakini maisha yote wanaishi nyumba za kupanga za National Housing. Sisi Waswahili tunashindana kujenga nyumba za kuishi za kulala na kuamka za mamilioni.

Waswahili hatushindani kwenye uwekezaji tunashindana kwenye nani kujenga nyumba kali kuliko mwingine! Hata waswahili wakiudhiana wakianza kutukanana isi mojawapo huwa kwani wewe una nini? Mimi Nina kwangu nimejenga nyumba za kuishi moja hapa mjini ingine kijijini

Nchi ziliizoendelea watu huwaza kuwekeza kwanza kama ndoto ya kwanza akipata pesa.

Hapa ndio siri ya umaskini wa waswahili ilipo. Ndoto za kwanza ni kwenye vitu visivyozalisha pesa hasa nyumba ya kulala na kuamka.
Hata mimi mwaka huu niliweka lengo la kujenga kua namba moja asante kwa kunibrain wash ngoja ni rearrange mipango biashara iikaae juu kabisa nisije anza kukopa ili nile
 
Kama uyasemayo ni kweli, elewa kuwa mahesabu yanakupiga chenga Mkuu. Huwezi kujenga nyumba ukapangisha ukapata utajiri. Nitakupa mfano. Nyumba za NHC huko Dodoma zinauzwa Million 78. Hizo nyumba zinapangishwa kwa 350,000/=.

Kwa mantiki hiyo mmiliki atasubiri miezi 223 kurejesha hela yake! Ambayo ni miaka 19. Wakati huo huo lazima kila baada ya miaka 5 ifanyike repair na akisubiri ifike miaka 10 itakuwa imekula kwake.

Kimahesabu Chumba na sebule Dar ni gharama ya million 10 kukijenga hadi mtu kuingia ndani kimekamilika. Kodo yake ni laki moja. Hivyo ni kama miaka 9 kikiwa na wapangaji utarudisha hela yako. Je, hii ni biashara kweli au biashara kichaa. Jioni njema
Watu wengi TZ wanashindwa kuelewa kuwa biashara ya real estate inaendeshwa kwa mikopo, Mtu anachukua real estate loan benki anaweka down payment ya asilimia kadhaa e.g 20% benji inalipa asilimia iliobaki, kisha anatumia asilimia pesa ya kodi anazokusanya kulipa deni kila mwezi, baada ya miaka kadhaa, jengo linakuwa la kwake huku ameingiza faida kwa miaka karibu yote na finally anamiliki ile nyumba na arudia tena na tena.

Bongo mtu anachukua pesa yake ya mfukoni milioni 50 anajenga nyumba, anapangisha laki 3 kwa mwezi. Yani ikitokea mpangaji yupo miaka yote na analipa anakuja kurudisha hiyo pesa baada ya miaka 14, hapo hajaweka hela za maintainence na mengineyo ndo aanze kuingiza faida. Hiyo milioni 50 angeweka kwenye biashara ndani ya miaka 14 je angekuwa na kiasi kile kile alichoanza nacho?

Tatizo wengi wanacopy paste bila kujua biashara zinafanyaje na wala hajisumbui kuuliza biashara zinaendaje, mtu akiona fulani kajenga apartments anadhani katoa pesa yake mfukoni kujenga, yeye anajitosa kichwa mbele halafu anashangaa kwa nini mahesabu hayaendi
 
Hakuna watu wanapenda kujenga nyumba za kuishi duniani kama Watanzania.

Ndoto kuu ya kwanza ya Mtanzania yeyote ngozi nyeusi ni kuwa na kwake hivyo akipenda vihela huvipeleka site kujenga nyumba ya kuishi hapa ndio siri ya umasikini wa Watanzania ngozi nyeusi kuanzia.

Wenzetu Wahindi hupanga hata miaka arobaini pesa zake akiweka na kukuza biashara yake. Wazo lake la kwanza huwa nikipata pesa natafuta nyumba ya bei rahisi ya kupanga halafu hela inayobaki naanzisha biashara. Wote mashahidi Wahindi matajiri hasa lakini maisha yote wanaishi nyumba za kupanga za National Housing. Sisi Waswahili tunashindana kujenga nyumba za kuishi za kulala na kuamka za mamilioni.

Waswahili hatushindani kwenye uwekezaji tunashindana kwenye nani kujenga nyumba kali kuliko mwingine! Hata waswahili wakiudhiana wakianza kutukanana isi mojawapo huwa kwani wewe una nini? Mimi Nina kwangu nimejenga nyumba za kuishi moja hapa mjini ingine kijijini

Nchi ziliizoendelea watu huwaza kuwekeza kwanza kama ndoto ya kwanza akipata pesa.

Hapa ndio siri ya umaskini wa waswahili ilipo. Ndoto za kwanza ni kwenye vitu visivyozalisha pesa hasa nyumba ya kulala na kuamka.

Hujajua uchungu wa kuishi familia ya watoto watano wote ndani ya chumba kimoja
 
Salam wadau wa JF
Kwa wenye uzoefu wa kupanga Frame hapa Dar Es salam, bei za kupanga kwa maeneo yafuatayo :-
Mwenge
Tegeta
Bunju
Ubungo
Buguruni
Sinza
NB: Nitafurahi kama nitapata bei za kupanga Mkabala na barabara au umbali kidogo (200m toka barabarani)

Ahsante
 
Nenda pale tegeta nyuki stendi ulizia mfanyabiashara yoyote mle ndani ya soko akuelekeze mwenyekiti wa soko utapewa utaratibu wote
 
Hakuna watu wanapenda kujenga nyumba za kuishi duniani kama Watanzania.

Ndoto kuu ya kwanza ya Mtanzania yeyote ngozi nyeusi ni kuwa na kwake hivyo akipenda vihela huvipeleka site kujenga nyumba ya kuishi hapa ndio siri ya umasikini wa Watanzania ngozi nyeusi kuanzia.

Wenzetu Wahindi hupanga hata miaka arobaini pesa zake akiweka na kukuza biashara yake. Wazo lake la kwanza huwa nikipata pesa natafuta nyumba ya bei rahisi ya kupanga halafu hela inayobaki naanzisha biashara. Wote mashahidi Wahindi matajiri hasa lakini maisha yote wanaishi nyumba za kupanga za National Housing. Sisi Waswahili tunashindana kujenga nyumba za kuishi za kulala na kuamka za mamilioni.

Waswahili hatushindani kwenye uwekezaji tunashindana kwenye nani kujenga nyumba kali kuliko mwingine! Hata waswahili wakiudhiana wakianza kutukanana isi mojawapo huwa kwani wewe una nini? Mimi Nina kwangu nimejenga nyumba za kuishi moja hapa mjini ingine kijijini

Nchi ziliizoendelea watu huwaza kuwekeza kwanza kama ndoto ya kwanza akipata pesa.

Hapa ndio siri ya umaskini wa waswahili ilipo. Ndoto za kwanza ni kwenye vitu visivyozalisha pesa hasa nyumba ya kulala na kuamka.
Kama Kuna kaukweli fulani, juzi nimemsikia jamaa anabishana na mwenzie, anamuambia Mimi nakaa kwangu Sina presha ,hata nikihamka saa tano sidaiwi Kodi, nikaona haya Sasa Ni mawazo ya kimasikini
 
Salam wadau wa JF
Kwa wenye uzoefu wa kupanga Frame hapa Dar Es salam, bei za kupanga kwa maeneo yafuatayo :-
Mwenge
Tegeta
Bunju
Ubungo
Buguruni
Sinza
NB: Nitafurahi kama nitapata bei za kupanga Mkabala na barabara au umbali kidogo (200m toka barabarani)

Ahsante
Unahitaji frame kwa ajili ya biashara gani? Ipo moja sinza
 
Tanzania serikali ilikosea kutokuwa na sheria za ujenzi, au kutopanga miji na vijiji.

Urasimishaji nao upo kisiasa, kuna mitaa haipitiki, ikitokea majanga ya koto hakuna atayebakia salama
 
Hapana mie napenda tu ujenzi. Niliona biashara easy kwangu ni kujenga na kupangisha watu (real estate) haina stress kama biashara nyingine na pia unaifanya huku unaendelea na kazi zake za kuajiriwa. All in all mtu ukiwa na makazi yako inakuondolea sana usumbufu ingawa katika stage fulani ya maisha lazima upange ila mambo yakikaa sawa jenga. Wapangaji wangu wengi nawashauri hivi.
Hutakuwa tajiri kamwe. Ila utakuwa mstaafu mwenye aman
 
Back
Top Bottom