Umasikini wa Watanzania chanzo chake ni kupenda kujenga nyumba ya kuishi kwanza badala ya kuanzisha biashara

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,908
51,904
Hakuna watu wanapenda kujenga nyumba za kuishi duniani kama Watanzania.

Ndoto kuu ya kwanza ya Mtanzania yeyote ngozi nyeusi ni kuwa na kwake hivyo akipenda vihela huvipeleka site kujenga nyumba ya kuishi hapa ndio siri ya umasikini wa Watanzania ngozi nyeusi kuanzia.

Wenzetu Wahindi hupanga hata miaka arobaini pesa zake akiweka na kukuza biashara yake. Wazo lake la kwanza huwa nikipata pesa natafuta nyumba ya bei rahisi ya kupanga halafu hela inayobaki naanzisha biashara. Wote mashahidi Wahindi matajiri hasa lakini maisha yote wanaishi nyumba za kupanga za National Housing. Sisi Waswahili tunashindana kujenga nyumba za kuishi za kulala na kuamka za mamilioni.

Waswahili hatushindani kwenye uwekezaji tunashindana kwenye nani kujenga nyumba kali kuliko mwingine! Hata waswahili wakiuziana wakianza kutukanana isi mojawapo huwa kwani wewe una nini? Mimi Nina kwangu nimejenga nyumba za kuishi moja hapa mjini ingine kijijini.

Nchi ziliizoendelea watu huwaza kuwekeza kwanza kama ndoto ya kwanza akipata pesa.

Hapa ndio siri ya umaskini wa waswahili ilipo. Ndoto za kwanza ni kwenye vitu visivyozalisha pesa hasa nyumba ya kulala na kuamka.
 
Hata hao wahindi kwao wana nyumba wamejenga. Huwezi kuwa unaishi say Afrika Kusini ukafikiria kujenga huko. Utapanga na kufanya biashara au shughuli yoyote halali. Hii dhana ndio ipo kwa wahindi, hapa wahindi sio kwao. Kwa baadhi wenye fedha nyingi sana huwa wanajenga maeneo kama Masaki, Upanga n.k na wengi huwa wananunua apartment.

Halafu kujenga sio umasikini, kumiliki nyumba ni jambo bora sana katika maisha maana nyumba ni kitu ambacho kinakupa mengi sana ikiwepo kukupunguzia gharama za kodi, kukuondolea stress za kutokuwa na kwako na pia hata ukipata tatizo la kiuchumi unakuwa na pa kuanzia.

Nyumba ni kitu ambacho hata ukiondoka duniani ghafla familia yako inakuwa na sehemu ya kuanzia kuliko ukiwa huna nyumba.

Nyumba ni muhimu katika ukuaji wa miji na Taifa kwa ujumla. Unavyoona nje yale majengo ni kwamba watu wamewekeza ndio maana kunapendeza. Na sisi tujenge majengo kukuza nchi yetu. Tuachane na wahindi wale hapa sio kwao ndio maana hawajengi. Tena si wahindi tu hata wazungu hawajengi hapa kwa kuwa si kwao hapa watachuma tu ila kujenga wataenda jenga kwao.
 
Hilo ni kweli,
Bahati Sipo kati ya hao watanzania wengi, Sio kujenga tuu, Kwa sasa kutumia pesa yoyote ile ambayo hazalishi Ni mpaka kuwe na ulazima sanaa..
Je, ukilipa kodi ya nyumba inazalisha? Kama unapanga na inakugharimu ni bora kujenga na kuwa na nyumba na kutolipa kodi. Kulipa kodi kwa mtu ni kumtajirisha. Inabidi kila mja awe na kwake yawe makazi bora au ya wastani kwako ni kwako.
 
Je ukilipa kodi ya nyumba inazalisha? Kama unapanga na inakugharimu ni bora kujenga na kuwa na nyumba na kutolipa kodi. Kulipa kodi kwa mtu ni kumtajirisha. inabidi kila mja awe na kwake yawe makazi bora au ya wastani kwako ni kwako
Mambo ya kupanga nayo mtihani tu.

Asili kila mtu awe na kwake bhana.

Lakini kukimbilia kujenga kwa taabu na mikopo sio jambo bora sana kwa upande wangu kuliko kukimbilia biashara.
 
Hii ni tofauti sana mzee. National housing nyumba bei nafuu(bora kupanga kuliko kujenga) mfano nchi zilizoendelea hakuna viwanja vya bei poa.

Hata hivyo sheria za ujenzi ni kali kuliko za Tanzania, yaani huwezi kujenga bila kibali, bila ramani, bila mpango yaani ukipiga hesabu ya ujenzi unaona bora ukapange. Tanzania kujenga ni nafuu kuliko kupanga, kupanga kero nyingi kuliko kuishi kwako. Bora kujenga kuliko kukuza biashara sababu pesa inaweza kufia huko na pesa ya pango ukakosa vile vile.
 
Je, ukilipa kodi ya nyumba inazalisha? Kama unapanga na inakugharimu ni bora kujenga na kuwa na nyumba na kutolipa kodi. Kulipa kodi kwa mtu ni kumtajirisha. inabidi kila mja awe na kwake yawe makazi bora au ya wastani kwako ni kwako

Kama kulipa kodi ni kumtajirisha mtu, huoni hiyo kwake ni biashara?

Na ikiwa ni hivyo basi, hizo biashara unazotaka kila mtu aanzishe, kununua kwako si kukutajirisha!
 
Unajua hao wahindi wanapanga nyumba za sh ngapi alafu ndo utushauri na maskini tukapange huko ili angalau tujiskie tupo nyumbani.

Anyway umesema wanawekeza kwanza mbona hata hao wazee cjaona nyumba zao wamejenga

Huo sio utaratibu wao ni wetu tuendelee kujenga kwetu waungwana.
 
Mambo ya kupanga nayo mtihani tu.

Asili kila mtu awe na kwake bhana.

Lakini kukimbilia kujenga kwa taabu na mikopo sio jambo bora sana kwa upande wangu kuliko kukimbilia biashara
Hapo umeongelea biashara vp kwa mfanyakazi au mwajiriwa? Mie naona ni muhimu ukianza maisha ujipange mipango ikikubali jenga uwe na kwako, utanishukuru baadae
 
Hata hao wahindi kwao wana nyumba wamejenga. Huwezi kuwa unaishi say Afrika Kusini ukafikiria kujenga huko. Utapanga na kufanya biashara au shughuli yoyote halali. Hii dhana ndio ipo kwa wahindi, hapa wahindi sio kwao. Kwa baadhi wenye fedha nyingi sana uwa wanajenga maeneo kama masaki, upanga n.k na wengi uwa wananunua apartment.

Halafu kujenga sio umasikini, kumiliki nyumba ni jambo bora sana katika maisha maana nyumba ni kitu ambacho kinakupa mengi sana ikiwepo kukupunguzia gharama za kodi, kukuondolea stress za kutokuwa na kwako na pia hata ukipata tatizo la kiuchumi unakuwa na pa kuanzia.

Nyumba ni kitu ambacho hata ukiondoka duniani ghafla familia yako inakuwa na sehemu ya kuanzia kuliko ukiwa huna nyumba.

Nyumba ni muhimu katika ukuaji wa miji na Taifa kwa ujumla. Unavyoona nje yale majengo ni kwamba watu wamewekeza ndio maana kunapendeza. Na sisi tujenge majengo kukuza nchi yetu. Tuachane na wahindi wale hapa sio kwao ndio maana hawajengi. Tena si wahindi tu hata wazungu hawajengi hapa kwa kuwa si kwao hapa watachuma tu ila kujenga wataenda jenga kwao
Kabisa mkuu, tena ninapata strong feeling kuwa ww ni zao la ardhi university
 
Kabisa mkuu, tena ninapata strong feeling kuwa ww ni zao la ardhi university
Hapana mie napenda tu ujenzi. Niliona biashara easy kwangu ni kujenga na kupangisha watu (real estate) haina stress kama biashara nyingine na pia unaifanya huku unaendelea na kazi zake za kuajiriwa. All in all mtu ukiwa na makazi yako inakuondolea sana usumbufu ingawa katika stage fulani ya maisha lazima upange ila mambo yakikaa sawa jenga. Wapangaji wangu wengi nawashauri hivi.
 
Back
Top Bottom