Binafsi ni mdau mzuri wa facebook (hasa kipande ya usomaji zaidi wa kile wadau wengine wanachopost). Kwa ufupi kule watu walio wengi ni wema sana, full kuposti mistari ya biblia na kukemea uovu yani kule unaweza kujiona wewe ndio shetani peke yako duniani. Wnawake wengi walio single (hasa wale walioko kwenye 30's na hakijaeleweka) ndio usiseme kwa injili. Yani ni kama dozi (asubuhi mchana na jioni).
Mtu amekula dunia wee hadi dunia imemchoka, mtaani alishachakaza sasa anaona usiku unakaribia suluhisho ni mwendo wa kuposti verse tu